YA MRWARA NA UTAJIRI WA MALIASILI ZETU
Baada ya Mtwara sijui ni wapi patafuata. Yaweza kuwa Arusha (Tanzanite), Shinyanga (Almasi na Dhahabu), Mwanza (Samaki), Mara (Dhahabu) na kwingineko kwingi. Ni viongozi wenye utashi wa kutoa maaamuzi ya busara tu wanaweza kutunasua na tope hili. Nafikiri itakuwa sahihi nikisema kwamba viongozi waliopo wameshindwa na hawana uwezo tena wa kutanzua mzozo wa mtwara na mizozo mingine yenye asili ya namna hiyo. Viongozi waliopo ni wepesi wa kutoa majibu na suluhu nyepesi kwa hoja nzito na matatizo makubwa. Rejea kauli ya mh. Stphen Wassira kuhusu mgogoro wa kuchinja kule kanda ya ziwa. Wassira alitoa suluhu nyepesi kama vile alikuwa anasuluhisha ugomvi wa wanae waliokuwa wanagombania kiporo cha ugali wa jana usiku. Kimsingi alipotoka sana katika suluhu aliyoitoa katika kutatua mzozo ule. Ni suluhu hizihizi zilizotolewa na serikali pale wanamtwara walipoanza kuonesha kutoridhishwa na mchakato mzima wa ujenzi wa bomba la gesi kuelekea dar.
Rais anasema wanamtwara wanachochewa na wanasiasa kwa maslahi ya kisiasa. Nafikiri hapa aliwalenga wapinzania wake wa kisiasa. Hizi ndizo ninazoita majibu na suluhu nyepesi kwa hoja nzito na matatizo makubwa. Swali la kujiuliza ni je, wanamtwara hawana utashi wa kujua haki zao na kuzipigania hadi wachochewe na wanasiasa? Kwa kauli hiyo, Rais alitakiwa aende mbali na kueleza kuwa viongozi wa serikali wanaotoa kauli za kuwaudhi wananchi wa Mtwara ndo wanaochochea vurugu za mtwara. Mfano, waziri Muhongo alipowafananisha wanamtwara na vyura wanaoruka majini ni dhahiri kuwa alikuwa anawachochea wananchi kufanya na kuendeleza vurugu. Huu ni ushahidi tosha na wapekee ambao Rais Kikwete angeutumia kuthibitisha kauli yake kuwa "wanasiasa wanachochea vurugu za Mtwara."
Rais Kikwete anasema eti serikali itamkamta kila mtu aliyehusika na vurugu hizo. "Hata kama mtu huyo ana pembe lazima zikatwe." Kwa uelewa wangu mdogo alionijaalia Mwenyezi Mungu nafikiri Rais Kikwetev ndiye mwenye pembe zinazostahili kukatwa. Pembe za Rais Kikwete ni udhaifu na uzito wa kuchukua maamuzi ya busara pale mustakabali wa taifa letu unapochezewa na wapuuzi wachache. Rais wetu amekuwa na tabia ya kuchukua maamuzi pale tatizo linapokuwa limefikia katika hali tete kiasi kwamba taifa lianakuwa limeshaumia kwa kiasi kikubwa. Mh. Stephen Wassira amewahi kukiri kuwa serikali ilichelewa (Uzembe) kuchukua maamuzi katika kutatua mgogoro wa kidini unaolitafuna taifa letu. Utawezaje kumtenga Rais Kikwete na uzembe huu ilihali yeye ndiye mkuu wa serikali? Hakika pembe za Rais wetu zimekuwa ndefu na nzito hadi zinatishia usalama na ustawi wa taifa letu.
Kama elimu ilivyo ufunguo, ndivyo gesi ilivyo ufunguo wa maisha ya wanamtwara na taifa kwa ujumla. Serikali inapaswa ilieleze taifa kuhusu faida na hasara za kujenga bomba la gesi kwenda dar na faida na hasara za kinyume chake (Yaani kutekeleza matakwa ya wanamtwara). KILA MWENYE MAAMUZI YA BUSARA NA ATIE MCHANGO WAKE KATIKA KUTANZUA MZOZO HUU. UBABE HAUNA NAFASI TENA. TANZANIA NI YETU SOTE NA ITAJENGWA NASI SOTE.