Ya Mtulia hayana tofauti na ya Lowassa

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Mhe. Maulid Mtulia alikuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CUF kuanzia mwaka 2015 na kuja kujiuzulu mwishoni mwa mwaka 2017 kwa kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kukoshwa na utendaji kazi wa Serikali ya Rais Magufuli.

Mapema mwaka 2018 Kamati Kuu ya CCM iliketi na kupitisha jina la Maulid Mtulia kugombea tena ubunge kwa tiketi ya CCM kutokana na Tume ya Taifa ya uchaguzi kutangaza upya uchaguzi jimbo la Kinondoni.

Kitendo cha CCM kumpitisha Mtulia kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kimewapa maneno washindani wenza (Chadema) kuanza kuhoji kitendo cha CCM kumpitisha Mtulia kugombea tena ubunge tena akiwa mgeni na kunyima fursa wenyeji!

Wakati wakihoji hilo Chadema wanasahau kitendo walichokifanya mwaka 2015 kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa.

Tuweke kumbukumbu sawa kidogo. July 28, 2015 Edward Lowassa alikabidhiwa rasmi kadi ya Chadema na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam na hapo hapo akaingizwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Haikupita siku mbili, yaani July 30, 2015 Chadema wakampa fomu ya kugombea urais kupitia kupitia Chadema. Lowassa alikuwa mgombea pekee kupitia Chadema na baadae akateuliwa rasmi kupitia mwavuli wa Ukawa kugombea urais.

Leo hii Watu wa Chadema wanapoishangaa CCM kumpitisha wanayemuita mgeni, Mtulia kugombea Ubunge wanasahau namna walivyompitisha Lowassa kugombea urais ndani ya siku 2 tangu ajiunge na Chadema.

Sio tu Lowassa, bali ni Chadema hao hao walimpokea Fredrick Sumaye Agosti 22, 2015 na ilipofika July 14, 2016 alichukuwa fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti kanda ya Pwani.

Mifano ipo mingi mno ambayo sioni sababu ya Chadema kuhoji juu ya Mtulia uhalali wa Mtulia na kusahau ya Lowassa.

Ukweli unabaki pale pale Mtulia hajavunja sheria wala utaratibu bali ameongeza nguvu, wafuasi katika kujihakikishia ushindi kupitia CCM.

Mtulia anagombea kupitia CCM, chama chenye sera, muundo, siasa za kistaarabu na gwiji wa kutekeleza ilani ya uchaguzi.

Mtulia anagombea kwenye chama ambacho kinatekeleza sera ya kutoa Elimu bure, kinachojenga miundo mbinu ikiwemo ya barabara, kinachojenga reli kwa standard gauge, kinachoboresha huduma za kijamii, kinachosimamia vyema rasimali za kitaifa (yakiwemo madini) yawanufaishe Watu wote, kinachopiga vikali vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

Wapinzani wanazidi kuweweseka kwenye uchaguzi wa marudio wa ubunge jimbo la Kinondoni kutokana na mambo makuu mawili. Mosi; Haiba ya mgombea wa CCM, Maulid Mtulia kwa jamii. Pili; Chama alichosimama kugombea ubunge, CCM kinachopendwa na wengi, chenye mtandao mpana na kilichopewa dhamana ya kuongoza dola.

Narudia tena kusema, kama hoja ni Mtulia kuingia CCM na kugombea Ubunge, Chadema wasisahau namna ambavyo walivyompitisha Lowassa kugombea urais mwaka 2015.

*Na Shilatu E.J*
Januari 26, 2018
 
Chama chenye miaka zaidi ya 30 kinachoshikilia dola...chenye kujigamba kuwa Na wanachama zaidi ya Million 8 walioiva kiitikadi...chama kilichojengwa katika misingi ya TANU (Hivyo kuwa Na uzoefu wa zaidi ya miaka 50).....kinapofikia kuhalalisha udhaifu kwa kujilinganisha na chama cha "juzi" kisichokuwa na "base" ya kukingiwa kifua na mkono wa dola unajua kuna kutindikiwa na imani na kuwapo kwa tatizo mahali fulani
 
Wewe jamaa ni zero brain kabisa, waliolalamika na wanaolalamika ni wana CCM wenyewe kuwa taratibu hazikufuatwa wewe unakuja na kihoja kama hiki juu ya CHADEMA nahisi akili zako unazijua mwenyewe.
 
Hivi neno "shilatu" kama sikosei limetokana na lugha ya kisukuma likiwa na maana ya viatu sio!
Sasa shilatu, sema hapa :- kipindi EL anaihama ccm alikuwa mbunge wa jimbo gani?
Ni kwanini umlinganishe huyo mchumba wenu aliyejiachisha kwa mume wake wa ndoa na kumkimbilia mme wa mtu kwa tamaa ya mpunga mrefu na mr. Lowasa? Kama una kisa au ugomvi binafsi na Lowasa basi mfuate mwenyewe mmalizane na sio kuandika uzwazwa wako jf! By the way, umeahidiwa kapost gani hapo lumumba?
Kwa taarifa yako EL sio size yenu hapo ccm so, msijisumbe kujilinganisha naye badala yake ishukuruni nec na policcm na wale wasiojulikana kwa kura zile zisizoonekana!
 
Chama chenye miaka zaidi ya 30 kinachoshikilia dola...chenye kujigamba kuwa Na wanachama zaidi ya Million 8 walioiva kiitikadi...chama kilichojengwa katika misingi ya TANU (Hivyo kuwa Na uzoefu wa zaidi ya miaka 50).....kinapofikia kuhalalisha udhaifu kwa kujilinganisha na chama cha "juzi" kisichokuwa na "base" ya kukingiwa kifua na mkono wa dola unajua kuna kutindikiwa na imani na kuwapo kwa tatizo mahali fulani
Kerebesha kauli yako bana!dah yaani chama hakina base !!
 
Kwa hiyo makosa yaliyofanywa na Chadema na nyinyi ndio mmeamua kufanya hayo hayo kisa Chadema walifanya kama hivyo? Kweli we kichwa maji
 
Wewe jamaa ni zero brain kabisa, waliolalamika na wanaolalamika ni wana CCM wenyewe kuwa taratibu hazikufuatwa wewe unakuja na kihoja kama hiki juu ya CHADEMA nahisi akili zako unazijua mwenyewe.
hata sie hasa tusio na bei tulilalamika sana juu ya mamvi kupewa fasta fasta kupeperusha bendera ya chama lakini kamwe hatukusikilizwa!
 
Back
Top Bottom