Ya mcc, symbion na hela kurudi zilikotoka: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya mcc, symbion na hela kurudi zilikotoka:

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MILKYWAY GALAXY, Jun 22, 2011.

 1. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu,

  Hii habari nimeikuta gazeti la Mwananchi (21/June/2011). Hapa nahisi kuna kamchezo fulani.
  Hela za MCC zimetoka USA (alipokuja Bush junior). Symbion ni ya USA (imepata baraka tele na mama Clinton).
  Tenda ya umeme wapewe wao. I smell something fishy here.
  Nawasilisha.
  Ā‘Serikali haitaingiza umeme majumbaniĀ’ Send to a friend


  Tuesday, 21 June 2011 21:22
  0diggs
  digg
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Adam Malima
  WIZARA ya Nishati na Madini imesema haina mpango wowote wa kuingiza majumbani umeme wa MCC na kwamba wananchi wanapaswa kufanya hivyo baada ya kupelekwa karibu na makazi yao.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima alilimbia Bunge jana mjini Dodoma kuwa kazi kubwa ya miradi ya umeme wa MCC ni kuhakikisha unafika katika maeneo ya wananchi licha ya jukumu la kuingiza majumbani kuwa la Serikali.

  Malima alikuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa mbunge wa Lolesia Bukwimba katika Jimbo la Busanda CCM ambaye alitaka kujua iwapo Serikali itakuwa tayari kuwaingizia umeme wananchi majumbani kwa kuwa uwezo wa wananchi ni mdogo.
  Awali katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itaanza utekelezaji wa miradi hiyo.

  Malima alisema Serikali iliahidi kukamilisha utekelezaji wa miradi ya umeme katika vijiji Bukoli, Nyarugusu, Rwamgasa na Katoro katika jimbo hilo katika mwaka 2011/12.

  Alisema utekelezaji wa shughuli hiyo umeanza katika hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa taratibu za ununuzi na kwamba zabuni zilitangazwa Machi 15, mwaka jana na kufunguliwa Julai, mwaka huo.

  Alisema katika zabuni hiyo, mkandarasi wa kutekeleza kazi hiyo ni Kampuni ya Symbion Power LLC kutoka Marekani na kwamba upimaji wa kina wa njia za umeme na kuweka alama, umeanza.

  Kwa mujibu wa Malima shughuli za kusafisha njia, kuchimba, mashimo na kusimika nguzo zimeanza tangu Mei, mwaka huu na kwamba kazi ya ujenzi katika maeneo ya Jimbo la Busanda, utaanza Agosti, mwaka huu.
   
Loading...