Ya mbeya na tume ya uchaguzi!!

Ya mbeya na tume ya uchaguzi!!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Aliekua na miaka 14 mwaka 2000 leo hii ameshakua mtu mzima mwenye miaka 18 na akifanya kosa anafungwa gereza la wa kubwa,na mwenye miaka 19,20,21,22na 23 wanatambulika kua wameshakua watu wazima,ila hawaruhusiwi kuchagua kiongozi anae mfaa wala kujipigia kura kama ataamua kuingia kujinadi mwenyewe ili achaguliwe na awe kiongozi.

katiba ya jamuhuri ya muungano inayasema hayo kua mwenye umri wa miaka 18 anaruhusiwa kuwa kiongozi kama atachaguliwa.tume ya uchaguzi wanayajua haya ila hawapendi kuyatatua kwa kua najua wakithubutu mwajiri wao mkuu atawafukuza sasa wamebaki kutoa mbinu za ujanja ujanja kama zilivyo lipotiwa leo na media huko mbeya.

wamekamatwa watu wakinunua shahada ili kuongeza kura za watawala wao wanabandua picha wanaweka ya kwao ili wawape wakazi wa eneo tofauti wakapige kura,ombi langu kwa tume ya uchaguzi msifanye kazi kipindi cha msimu wa uchaguzi pekee na muache uzembe wa kufikiri maana damu inayo kwenda kumwagika tanzania nyie ndio mtakao jibu duniani na hata kwa allah,kwanini mnacheza mchezo wa kitoto na wa rafu namna hiyo?au mnafikiri kunautawala wa milele?

Yukuawapi nabii adamu alie kaa miaka zaidi ya 900? Kumbukeni hakuna chenye mwanzo kikakosa mwisho,na pesa sio kila kitu na ndio maana tukifa tunazikwa 6fut na pumzi ni bure kwa kua ilionekana hakuna atakae weza gharama.nihayo tu ila ninamachungu sana hii nchi nixetu sote
 
CCM kule Airport hawana chao, usiogope kabisa kwanza uliowaona ni wakuja tu. Mbeya ni yetu na SUGU ndo Rais.
 
wakibandua picha zao na kuweka za hao vijana jee majina yatakuwemo kwenye daftari la wapiga kura hii nchi bila kuchapana hatutajiweka sawa
 
Haya yakiendelea kufanyika tume nayo ndio kama sikio la kufa.....na pia kwa kuwa wanatumika katika hujuma hizi hawasemi kitu nao siku zao si zinahesabika bwana!
 
Back
Top Bottom