Ya Magufuli "Common Man's Charter" na Azimio la Arusha linalorejea

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
* YA MAGUFULI "COMMON MAN'S CHARTER" NA AZIMIO LA ARUSHA LINALOREJEA..

Mwalimu Nyerere na wenzake wenye uelewa wa aina moja, waligundua mapema kwamba katika dunia ya ubebari uliokomaa, raia wa kawaida wa nchi zinazoendelea kama Tanzania, wananchi wake hawawezi kufaidi matunda ya Uhuru. Na kwamba leo hii wizi, ubadhirifu uliokithiri kwa zaidi ya miaka 30 ni matokeo ya kukosekana kwa misingi ya Azimio la Arusha lililochochewa na kuingia kwa ubebari uliokomaa nchini.

Kwa zaidi ya miaka 30 (tokea, 1985) tumebahatika kuona hasara kubwa ya mfumo unaonadiwa sana na marafiki zetu wa nje, mfumo mbadala wa ujamaa na kujitegemea, ambao leo umesababisha kuibuka kwa pengo kubwa kati ya matajiri na masikini nchini. Mfumo ambao kwa tafsiri yangu unaendelea kuzua chuki iliyoandikwa katika kila uso unaopishana nao. Mfumo ambao rafiki yako mkubwa ni yule unayepanga naye dili za uwizi, ubadhirifu na kukwepa kodi na sio yule mnayeshauriana jinsi ya kuboresha huduma kwa jamii. Ndio mana leo hii, hasa awamu ya nne tumeona kila aina ya wizi na ubadhirifu e.g Escrow, Richmond, StanbicGate, Sukari, Bomba la Gesi, Bandari, NSSF, TRL huku jamii tukikaa na hao wezi na kuwashangilia pale wanapotununulia bia. Kwa maana nyingine mfumo huu umetufanya kuwashangilia na kuwasifi wezi na wabadhirifu wa mali za umma badala ya kuwachukulia hatua..

Rais Magufuli, mpaka sasa ameonyesha dhamira kubwa ya kurudisha nchi katika misingi mikubwa ya Azimio la Arusha ambacho kiini chake ni hiki "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonye ili tusionewe tena na tusipuuzwe tena" (26~29/1/1967, AZMA). Hili litawezekana kama tukipata kiongozi imara na wa kusimamia maslahi ya wanyonye. Rais Magufuli kaonyesha hilo na karejesha matumaini ya wanyonge, kwamba atafanya mapinduzi katika kurejesha mfumo ambao utawapa wananchi wote fursa ya kufaidi matunda ya jasho lao

Hivi hatushangai kwamba katika Tanzania matajiri wakubwa ni wanasiasa na baadhi ya watumishi wa umma. Na wengi wa hawa wanapoingia katika nyadhifa zao za siasa wanakuwa hawana kitu, hawana biashara (hata vibanda vya kuku), hawamiliki makampuni, wape miaka 5 tu katika siasa au miaka 3 katika utumishi wa umma, basi ndio watakuwa wenye hodhi na miliki ya kila aina ya mali...

Rais Magufuli kwa hizi siku 28, kwa kiasi kikubwa kaanza kuonyesha dira asilia ya taifa ya Tanzania, kitu ambacho kilikuwa kigumu kwa watangulizi wake tokea 1985~2015. Kimsingi Magufuli ana dhima ya kutufanya wananchi tuamini ya kwamba "Siku moja (kwa sasa) tutaishi katika Taifa lenye serikali ambayo, kwa kuzingatia kanuni ya ruzuku, inafanya kazi usiku na mchana ili kukuza na kuhami usawa wa binadamu kwa kutekeleza siasa za ujamaa na kujitegemea katika namna ambayo inakuza maslahi ya pamoja na kulinda maslahi ya kila mtu binafsi".

Magufuli kaanza kwa kufuta posho zisizo za msingi kwa wabunge na bodi kama ilivyowekwa wazi katika Azimio la Arusha, katenganisha wabunge na bodi za uendeshaji wa mashirika ya umma, kaondoa matumizi yasio ya lazima na kupeleka huduma kwa jamii "Philosophical Distribution of Social Services"; Amekuwa ni mtu wa kuchukua maamuzi ya haraka na kubwa zaidi kaanza kuwashughulikia wabadhirifu na wezi wakubwa wa mali za umma, ambao wametuibia kwa zaidi ya miaka 30. Na ndio hawa na wengine ambao tunaamini bado watachukuliwa hatua, kwa namna moja na kwa matendo yao waliongeza gap ya walionacho na wasionacho.

Njia pekee ya kufanikisha haya na mengine yatakayotokea ni sisi wananchi kumuunga mkono Rais, ambaye tayari kaonyesha kwa dhati kabisa kwamba analielewa na kulikubali Azimio la Arusha lenye misingi ya falsafa ya ujamaa. Dhamira hii ya kuwarudisha wanasiasa na baadhi ya watumishi wa umma katika misingi ya kuwajali wananchi lazima tukiri kwamba haitakuwa kazi rahisi, mabebari wamejaa ndani ya serikali na pasipo shaka wameweka mizizi ndani ya serikali (hasa baada ya Azimio la Zanzibar) na bila shaka hawa ndio watajaribu kila namna kumuangusha Rais katika kutekeleza majukumu yake. Ili mabebari wasifanikiwe kabisa, ni jukumu letu wananchi wote na kwa ujumla wetu tushikamane huku tukimuunga mkono Rais Magufuli ambaye tayari kaonyesha dhamira ya kufuata misingi mikubwa ya ujamaa...

Mchambuzi Huru: P. Kasera (BA, Sociology. MA Development Managemnet, Phd (on progress)....
 
Kila rais anaeingia wapambe wa ccm lazima mseme huyo ndo chaguo la mungu,mara ni kama nyerere,mlifoji mpaka Jakaya Mrisho Kikwete akawa JK ili afanane na JK Nyerere lakini wapi!Na sasa hivi mnamtukana,sasa hivi mnamuimbia Pombe nyimbo zilezile mlizokuwa mnamuimbia Kikwete alivyoingia.Acheni uzuzu!
 
Mh yangu macho na masikio. Huyo unayemsema kwamba angalau anaonesha njia ndo huyohuyo anayeambiwa amejaa ukabila. Angalia alivyowabadilisha viongozi mbalimbali na kuwaweka akina mabula, masanja, makonda, mtaka, luhaga, maganga n.k. 'Kiongozi anayeendekeza ukabila hatufai' (marehemu baba wa Taifa). Kwa maana hiyo hata angefanya usanii wa namna gani, kiongozzi mwenye sifa ya ukabila hatufai.Tusijidanganye watanzania wanaweza kukaa kimya lakini wanaona unayoyafanya iko siku watakupa haki yako. Anayefikiria sifa hii si ya kiongozi wetu ajitokeze hadharani na kumtetea akitoa ushahidi na vielelezo
 
Mkuu tulia.... Watu wamelewa.....
 
Kila rais anaeingia wapambe wa ccm lazima mseme huyo ndo chaguo la mungu,mara ni kama nyerere,mlifoji mpaka Jakaya Mrisho Kikwete akawa JK ili afanane na JK Nyerere lakini wapi!Na sasa hivi mnamtukana,sasa hivi mnamuimbia Pombe nyimbo zilezile mlizokuwa mnamuimbia Kikwete alivyoingia.Acheni uzuzu!
Mkuu ni Watz wachache sana wasio danganyika hakuna mwanaccm aliye na uchungu na nchi hii
 
Back
Top Bottom