Ya Lwakatare Tumeyasikia haya Je?

Ya Lwakatare Tumeyasikia haya Je?

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746
Habari wana JF
Nachukua fursa hii kutoa dukuduku langu kwani tumeshuhudia sakata la video ya Lwakatare lilivyochukua kasi na tupewa uzito wa juu na vyombo vyote vya usalama.
Naomba tulinganishe sakata la Lwakatare na haya ninayoyaweka hapa chini tuchanganue na kupima kwa kina juu ya Lwakatare kufunguliwa kesi ya Ugaidi je ni sawa au si sawa na kama ni sawa haya mengine yamefikia wapi katika kutatuliwa.

1.DIWANI NA KIKUNDI CHA MAUAJI

DIWANI wa Kata ya Mabila Wilaya ya Kyerwa Mkoani KageraChristian Songambele(CCM)anatuhumiwa kufanya mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyakatete Danes Damian(TLP) na Msaidizi wakeJohnson Damian waliofungiwa kwenye nyumba yake na kuteswa kabla ya kufariki.

Mauaji hayo yametokea March 13,baada ya marehemu kutekwa wakiwa shambani na kundi la watu lililoongozwa na Diwani huyoakiwatuhumu kuhusika na kifo cha mtoto wake aliyeitwa Godfrey kilichotokea mwaka jana.
Kijana aliyeshuhudia utekaji huo Kamugisha Damian alisemasiku hiyo jioni akiwa na marehemu wakichimba viazi ghafla walivamiwa na kundila vijana lililoongozwa na Diwani ambaye alitoa amri wakamatwe naye kuambiwaalale kifudifudi.

''Nililala chini na kukanyagwa shingoni nisingewezakuwasaidia nilisikia wakilia baada ya kuondoka nilifuatilia hadi kwa diwaninikakuta wameingizwa ndani na haponilikwenda kutoa taarifa nyumbani''alisema Damian.

Katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja watu sita wameuawakatika Kijiji hicho cha Omukagando mauaji yanayodaiwa kufanywa na kundilinalojiita ‘hakuna kulala'ambalo hufyeka migomba na kuharibu mali zawatuhumiwa likihusishwa na mkono wa diwani.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Philip Kalangi amethibitisha kuwepo kwa mauaji hayo na kuwaDiwani huyo anasakwa na Polisi baada ya kutoroka na gari lake akiwa pamoja nabaadhi ya vijana anaodaiwa kushirikiana nao katika mauaji hayo.

Kwa mujibu wa Kamanda Kalangi amelitaja tukio hilo kama lakikatiri na kuwa juhudi za polisi kumnasa Diwani huyo na kundi lakehazijafanikiwa baada ya kutorokea sehemu isiyojulikana.
Akiongea ofisini kwake Ofisa Mtendaji wa Kata yaMabila Herman Leonard alisema siku ya tukio alipigiwa simu na diwani akimtakaafike ofisini kuwapokea watuhumiwa aliodai alikuwa anawatafuta kwa muda mrefu.

Alisema kutokana na hali mbaya waliyokuwa nayo alikataa kuwapokea watuhumiwa hao na kumshauri Diwanihuyo na kundi lake wakatafute fomu ya matibabu (PF3) na kuwapeleka hospitali.

''Alinipigia simuakisema watuhumiwa niliowatafuta wamepatikana walifika kwenye ofisi saa mbiliusiku walikuwa wamejeruhiwa na kufungwa kamba hali haikuwa nzuri Diwani(Songambele) aliondoka nao kwenye garilake''alisema Leonard

Watelekeza maiti kituo cha Afya Nkwenda
Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kituo cha Afya Nkwenda PonsianMasinde Diwani huyo akiwa na kundi lake kwenye gari alifika na majeruhi haokatika kituo hicho saa sita usiku nakumuomba awape matibabu.

Alisema Diwani huyo alimwambia kuwa aliwaleta watuwaliopigwa kidogo ambapo alimwambia awatelemshe kwenye gari lake kwa ajili yakuwapima na kuwapa matibabu.

Baada ya kuwapima alimwambia Diwani kuwa amempelekea maitimmoja na majeruhi mmoja na kuwawalionekana kuvuja damu nyingi na wote walionyesha dalili za Anemia ambayohutokana na upungufu wa damu.

''Baada ya kumwambia hivyo aliondoka bila kuaga na kundi lavijana ambao walipanda gari na kuondoka,niliandika barua ili majeruhialiyebaki(Johnson Damian)akatibiwe hospitali ya Nyakahanga''alisema Masinde

Hata hivyo majeruhi huyo alifariki asubuhi ya March 14,katika hopitali ya Nyakahanga wakati akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa baadhiya wananchi walioshuhudia miili ya marehemu na kuomba majina yao yahifadhiwe kwaajiliya usalama wao walidai walikuwa wamekatwa visigino na kuchanwa kwa vituvyenye ncha kali sehemu mbalimbali.

Pia wananchi wa Kijiji cha Omukagando wameonyesha hofu yakuendelea kufanyika kwa mauaji ya kulipiza kisasi hasa kutokana na Diwani huyo aliyeyekomafichoni kuendelea kumiliki bunduki ambayo siku ya tukio alitembea nayohadharani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Philip Kalangi alisemawanachunguza kama Diwani huyo Christian Songambele anamiliki silaha hiyokisheria huku wakiendelea kuwabaini wanachama wa kikundi cha hakuna kulala kinachohusishwa na mauaji ya kikatili.

2.MUUAJI WA PADRI MUSHI ZANZIBAR

IMEELEZWA kuwa, mtuhumiwa Omar Mussa Makame (35) anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumuua Padri Evaristus Mushi ni mwanachama wa CUF ambaye aligombea nafasi ya uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika Jimbo la Rahaleo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).

Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Hamad Masoud alithibitisha jana kuwa, mtuhumiwa huyo ni mwanachama wao na alishiriki katika mchakato wa uchaguzi mkuu na kusimamishwa na chama katika kampeni za Uwakilishi Jimbo la Rahaleo.
"Ni kweli mtuhumiwa anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Padri Mushi ni mwanachama wetu na alishiriki katika mchakato wa kuwania Uwakilishi Jimbo la Rahaleo mwaka 2010.

Hata hivyo, Hamad alisisitiza na kusema suala la Omar kamwe lisihusishwe na CUF na kusema suala hilo watalitolea tamko baadaye.
** Kwa upande wa huyu sijajua atafunguliwa mashitaka gani tusubiri tuone***


3.
Slaa, Mwakyembe watishiwa kuuawa

​

Membe, Mengi, Mwandosya nao wamo
IJP: Tuna taarifa hizo, tunachunguza
Sheikh Yahaya Hussein naye ahusishwa
clip_image001.gif

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini, Dk. Willibrod Slaa ametajwa kwenye orodha ya watu wanaotishiwa kuuawa.
Mwingine aliye kwenye orodha hiyo ni aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, MwanaHALISI linaweza kuripoti.

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini (IJP), Said Mwema amethibitisha kuwa ana taarifa kuhusiana na tishio hilo na kwamba ofisi yake inazifanyia kazi.

"Ni kweli, jeshi la polisi linazo taarifa hizo za kuwapo kwa tishio la mauaji. Lakini nafikiri hilo ni jambo la kiupelelezi zaidi," alisema IJP Mwema katika mahojiano yake na gazeti hili juzi Jumatatu.

Hata hivyo, Mwema alikataa kulizungumzia suala hilo kwa undani, badala yake alielekeza gazeti hili kumtafuta Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishina wa Polisi, Robert Manumba.

Naye Manumba alipoulizwa alikiri kuwapo kwa tishio hilo lakini aliishia kusema, "Bado tunafanya uchunguzi."
Alipoulizwa hatua walizofikia katika uchunguzi huo, Manumba alisema, "Unapofanya uchunguzi kuna mambo mengi ya kuzingatia. Kuna kukusanya ushahidi. Kwa jumla, bado tunafanya uchunguzi," alisisitiza na kusema muda ukifika taarifa kamili itatolewa.

Kufichuka kwa tishio la mauaji ya watu hao mashuhuri, kumeibuka kufuatia barua ya kurasa saba iliyoandikwa na Dk. Mwakyembe ambaye sasa ni naibu waziri wa ujenzi kwa IJP Mwema.

Katika barua hiyo ya 9 Februari 2011, iliyobebwa na kichwa kisemacho, "Taarifa ya njama za kuondoa maisha yangu na ombi kwa jeshi la polisi kulinda haki yangu ya kikatiba ya kuishi," Dk. Mwakyembe anataja watu wengine mashuhuri wanaotishiwa kuuawa.
Hao ni mfanyabiashara mashuhuri nchini, Reginald Mengi, waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Melecela.

Dk. Mwakyembe anasema katika barua yake, "Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takribani mwezi mmoja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake – kwa maana ya wahusika na maudhui – hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa."
Anasema pamoja na hayo, bado ana imani kubwa na jeshi la polisi kuwa litaifanyia kazi taarifa hiyo bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa.

Msingi mkuu wa yeye kuamua kuvitaarifu vyombo vya dola, anasema Dk. Mwakyembe, ni taarifa alizozipata kutoka Songea, 22 Januari 2011 zinazolihusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa 21 Januari 2011 wakitumia gari linalodaiwa kuwa la wizara yake.

Gari hilo aina ya Land Cruiser lilikuwa na namba za usajili STK 6868, lakini baadaye namba ilibadilishwa na kusomeka STK 6869.
Gari hilo liliwateremsha "abiria" hao saba sehemu iitwayo Madaba na kisha kuchukuliwa na gari jingine Land Cruiser hardtop, Na. T 768 BDU hadi baa ya Top Inn mjini Songea.

Anawataja baadhi ya abiria waliokuwamo katika gari hilo kuwa ni raia wawili wa Somalia, Hafidh na Faraj, "kijana mmoja wa Kichagga" kwa jina Mustafa a.k.a "Master" Mkusa ambaye imeelezwa kuwa ni ofisa wa idara ya usalama wa taifa na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Ramika kutoka Tanga, ambaye inadaiwa ndiye "mtaalamu" wa kukaba watu.

Dk. Mwakyembe anaeleza katika barua yake kwa IJP, kwamba aliyepokea genge hilo la wahalifu mjini Songea, ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini, Rajabu Mtiula akiongozana na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Manya.
"Usiku wa Jumamosi 22 Januari 2011, kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo kwa gari aina ya Defender STK 2654, likiendeshwa na Zuberi Komba kwa lengo la kukutana na ‘mganga' Majungu (kabila Mdendeule) ambaye anaishi ndani ya mbuga ya wanyama (Selous Game Reserve with impunity,)" anaeleza Dk. Mwakyembe katika barua yake.

Anasema, "Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha wageni hao kwa mganga ambako walikaa siku saba wakitengenezwa. Walirejea Songea 29 Januari 2011 na kesho yake, 30 Januari 2011 wakaanza safari kurejea Dar es Salaam."
Anasema kutoka Songea hadi Mafinga, watuhumiwa wa njama za kuua walitumia gari Na. T 768 BDU ambalo walilitumia awali kutoka Madaba hadi Songea. Anasema walifika Mafinga saa mbili usiku na kukuta magari mawibili yakiwasubiri. Moja, Hilux Mayai ya kampuni ya Vodacom na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro.

Akiandika kwa kujiamini, Dk. Mwakyembe anasema, "…walipofika Morogoro walipokelewa na askari mmoja anayemtaja kwa jina la Sabasita. Hapo kundi likagawanyika: Watu wanne wakiwemo wale wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol T 845 ADH mali ya kampuni ya Caspian, na wengine wakabaki Morogoro."

Kampuni ya Caspian ni mali ya Rostam Aziz, mfanyabiashara, mbunge wa Igunga (CCM) na wakala anayejitaja kuwakilisha kampuni ya kufua umeme ya Dowans ya Costa Rica. Gazeti lilipomtafuta, hakuweza kupatikana.

Anamwambia Mwema kuwa, Mganga Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wake wanaweza kuongea naye kama walivyofanya waliompa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Dk. Slaa na wengine.

Anasema mganga huyo "ametengeneza dawa ya kuwapumbaza waliohukumiwa kifo na kuwa mfano wa mbwa mbele ya chatu" ili kukimbia hasira za wananchi pale mpango wa mauaji utakapotekelezwa.

Dk. Mwakyembe anamueleza IJP Mwema, kwamba awali mkakati wa kumuua Dk. Slaa ulipangwa kutekelezwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, lakini ulisitishwa kwa hofu ya kuingiza nchi katika machafuko.

"…utabiri wa Sheikh Yahya Hussein mwaka jana kuwa mmoja wa presidential candidates (wagombea urais) atakufa, ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makinisa. Utabiri huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango wenyewe," anasema.

Wiki mbili zilizopita, Sheikh Yahaya alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kutatokea vifo vya watu kadhaa mashuhuri wakiwamo wanasiasa na mwandishi mmoja wa habari mashuhuri nchini. Wakati Shekh Yahaya anatoa utabiri wake, Mwakyembe alikuwa katika wiki ya tatu tangu awasilishe malalamiko yake polisi.

MwanaHALISI lilipowasiliana na Sheikh Yahya ili kufahamu iwapo utabiri wake unatokana na kutumiwa na watu maalum waliomlipa fedha ili kufanikisha mkakati huo wa mauaji, mnajimu huyo alisema, "Watu wasubiri matokeo."

Alisema anachokifanya yeye ni unajimu na tayari amefanya hivyo katika matukio kadhaa makubwa ikiwa ni pamoja na kuwako kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

"Nilitabiri Raila Odinga kuunda serikali moja na Mwai Kibaki Kenya. Yametimia. Nilitabiri CCM itapata msukosuko baada ya uchaguzi mkuu, imekuwa hivyo. Sasa hapo unahoji nini?

"…Sijataja jina la mtu, hivyo watu wasijihisi kwa utabiri wangu, ila wao wasubiri matokeo. Halafu ninyi MwanaHALISI mnafanya kazi nzuri. Ipo siku nitawaita hapa kuzungumza nanyi. Ila nayi msihofu, msubiri matokeo."

Naye Dk. Slaa alipoulizwa kuhusu mpango huo, kwanza alicheka, kisha akauliza: "Nani kakuambia?" Alipoelezwa kuwa ni taarifa zilizothibitishwa na jeshi la polisi, Dk. Slaa alisema, "Basi nadhani wao ndiyo wanajua wanaohusika katika suala hilo."

Katika barua yake kwa IJP, Dk. Mwakyembe anasema kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hassani alitumwa kutoka Dar es Saalam kwenda Dodoma, 5 Februari mwaka huu kwa "maandalizi" ya kikosi cha mauaji. Amesema tayari kikosi hicho kimefanya utambuzi wa nyumba yake aliyopangiwa kuishi na serikali.

Anasema, "Tarehe 6 Februari 2011, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkonga (T 360 AKU). Waliokuwa kwenye kikosi hicho ni wasomali wale wawili, mgeni mmoja wa kiume kutoka Uganda, Mustafa a.k.a ‘Master' na kijana mmoja ambaye tarehe 19 Januari 2011 aliwabeba wasomali hao kutoka Morogoro kwa gari aina ya VX Lands Cruiser T 656 APF. Kijana huyo ana shepu ya Kitusi na anaongea Kifaransa."

Jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe anasema, "Wahitimu hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na Kiwanda cha Mohammed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa, chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa MALKAZ na juu ni sehemu ya kuishi."

Anaeleza kuwa tarehe 5 Februari, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda. Mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Anaripoti kuwa walipokelewa kwa magari mawili: moja la polisi, PT 0288 – polisi ujenzi na la pili lenye namba za kibalozi T 69 CD 82 aina ya RAV 4. Anasema, jioni wakawa na mazungumzo ya kina na raia wawili wa Somalia ambao inadaiwa ni kutoka kundi la Al-Shabaab.

Dk. Mwakyembe anasema katika maelezo yake kwamba amepata picha ya kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho wameingizwa nchini.
Anasema, "Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka wanaharakati wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewe hoja kuwa maadaui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu."

Katika barua yake kwa IJP, Dk. Mwakyembe anasema kila siku hupata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili; anazitoa taarifa hizo kwa jeshi la polisi ili ziwasaidie katika upelelezi.

Kwanza, taarifa zinaonyesha raia hao wa kisomali waliingia nchini kutokea Kenya na walikwenda Dodoma kupitia njia ya barabara kwa kutumia gari aina ya RAV 4 (new model- T 816 AQS) tarehe 08 Januari 2011.

Pili, Dk. Mwakyembe anasema walipofika Morogoro walipokewa na askari Sabasita wa jeshi la polisi mkoani humo, ambapo walikaa katika hoteli mbili tofauti – Hillux Hotel na Top Life. Anamtaja aliyewafanyia booking wageni hao ni mmiliki wa Morogoro Hotel aliyemtaja kwa jina moja la Kari.

Tatu, Dk. Mwakyembe anasema magari waliyotumia wakiwa Morogoro, ni RAV 4 T 816 AQS, VX Land Cruiser STK 1287, Mercedez Benz (Station Wagon) T 874 BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T 218 BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T 656 APF na Nissan patrol T 845 ADH.

Wakiwa Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe anataja watu waliokuwa na mawasiliano na waliotumwa kuchukua roho yake kuwa ni "Masuhe wa Central Police Station (polisi kati), Fred Lowassa ambaye inadaiwa aliwapelekea mbuzi watatu huko Kiwalani tarehe 04 Februari 2011 na hata kuwatafutia gari VX Land Cruiser T 656 APF.

Anasema walipokuwa Dar es Salaam, tarehe 13 na 14, Januari wabaya wake walifikia nyumba Na. 551, Mtaa wa Chakechake, Upanga.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, Rajab Mtiula, hakupatikana juzi kuzungumzia kuhusishwa kwake katika mikakati hiyo.

Gazeti lilipowasiliana na Fred Lowassa kueleza juu ya kuhusishwa katika maandalizi ya kifo cha Dk. Mwakyembe na wenzake alijibu, "Kaka katika mazingira ya kawaida tu, hilo jambo ni very serious (hilo jambo zito). Kuua ni tuhuma nzito.
Alisema, "Siku hizi kuna teknolojia ambako ukifanywa uchunguzi, itaonekana tu. Mimi nimekutana na mambo magumu sana maishani, lakini siwezi kufikia hatua ya kuua au kuhusika kuua."

Fred ambaye ni mtoto wa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa alisema, "Yakinipata magumu, mwokozi wangu ni Mungu. Naomba Mungu, halafu huwa nasamehe. Siku zote huwa sipendi kuingia kwenye malumbano," alieleza.

Lakini Dk. Mwakyembe katika barua yake kwa IJP Mwema anasema, "Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyika, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe."

Taarifa zinasema kila aliyetajwa kuuawa amejulisha taarifa hizo na Dk. Mwakyembe kama ambavyo ameeleza katika maelezo yake polisi.
 
Inasikitisha na kuhuzunisha sana Mh. Diwani baada ya kutafuta jinsi ya kuleta amani yeye anakuwa muongozaji wa mauaji. Binafsi imenigusa muda maana hao waliouliwa ni ndugu zangu. Naoungana na mleta mada hii kama ilivyotumika nguvu kubwa kumkamata huyo wanayedai ni gaidi kwa kutumia video ya maongezi yake ya kupanga kuteka sijui kufanyaje, watumie nguvu hizo hizo kuwakamata na hawa ambao wao wameondoa uhai wa watu kabisa na si kupanga kuongoa uhai sijui nini na nini.
 
Huwa Inanisikitisha sana ninapo soma maandiko yanayo lihusisha jeshi la polisi na mauaji, na vitisho, na siasa chafu kama hizi., hua najiuliza ningefanya nini kama mimi ndiye ningekua katika nafasi ya Inspector General Mwema? ni jukumu kubwa na gumu sana alilo nalo Ng. Mwema,. nisingependa ku sema tu kwaurahisi kwamba anashindwa kuyasimamia haya sawasawa., kwa sababu nina imani na utu wake na uwajibikaji wake., lakini kwanini haya? kwanini kila kukicha ni jeshi la polisi,. ni usalama wa taifa? why???

inanifikisha mahali nina wasiwasi ipo nguvu inayofanya kazi kuratibu haya mambo na huenda iko juu ya mamlaka ya IGP Mwema., kwasababu haiwezekani taarifa hizi ziendelee kutapakaa tu mtaani za kulichafua jeshi la polisi kwa kiwango hiki halafu kuendelee tu kuwa kimya tukishughulika zaidi na vitu visivyo kuwa na uzito na kiviachiliya hivi viendelee kuwepo tu.,

sijui nguvu hiyo ni ipi?? lakini ipo.,
 
Hii habari mbona imeninyong'onyeza sana, Tanzania ndo tumefikia hapa kweli?
 
Hapo ndipo tulipolifikisha taifa, na bado hatupo tayari kukubali kuwa hali ni mbaya ili tuweke nguvu zaidi katika kuliokoa taifa hilo. Ukifuatilia kwa undani mfano tukio la diwani waliotekeleza mauaji hayo ni watanzania waliodanganywa na huyo diwani kwa ujira mdogo sana, inawezekana ni chakula na pombe, sasa maisha yao yamekuwa ya kukimbia hovyo na hawatakaa wawe na amani katika maisha yao. Ukifuatilia kwa undani matukio mengi yanatokea yanatekelezwa na sisi wenyewe kwa ujinga na njaa zetu tunakubali kutumiwa kwa ujira mdogo. Mwisho wa siku mzunguko huu tuliouanzisha utakurudia wewe ambaye leo unadhani umefanikiwa kwa njia chafu. Leo utaua lakini kumbuka mzunguko huo au mauti uliyoanzisha hatakuacha na huenda ikiwa yako yakawa ya mateso zaidi, hakuna atakayesalimika iwe unhusika leo au haujahusika na ndiyo maana suluhu ya yote yanayoendelea lazima yatoke kwetu wenyewe ssiyo kwa watalawa au polisi. Wewe polisi/mtu yeyote mwenye dhamana ambayo leo unaitumia nafasi hiyo kuangamiza wenzako, kumbuka unajiandalia mazingira mabaya zaidi pindi utakapoondoka katika nafasi hiyo hautakuwa na amani hata kidogo kwa kuwa umeondoka ukiwa umeishaiharibu amani.
 
Mmmh! Kazi ipo, mbona hatuko salama! Maana michongo yote inafanywa na wanausalama. Na kama maelezo yapo wazi namna hii, hao jamaa 'wakachukuliwe' tu tayar kwenda kwa pilato. Hapa ndo maana MwanaHALISI halitafunguliwa, halipepesi macho wala kutikisa masikio. Lwakx aachiwe tu.
 
Hayo kwa kuwa yalikuwa yakiratibiwa na serikali na watu wao wa karbu, walkaa kimya wala hawakuuita ugaidi.
 
Mmmh huyo diwan alishinda uchaguz kwel au aliiba kura?
Walimchagua kwa lipi?

Ni ajabu sana polis kushindwa kumkamata mtu maarufu kama huyo mpaka leo.

Picha, familia, ndg, jamaa na marafik, vyote hvyo bado mnashndwa kumkamata??

Kwel serikal imekuwa na mkono mfup na wenye kilema cha kujitakia.

Ule mkono mrefu wa serikal umeenda wap siku hiz??
Hatar kubwa inakuja TZ.
 
Habari wana JF
Nachukua fursa hii kutoa dukuduku langu kwani tumeshuhudia sakata la video ya Lwakatare lilivyochukua kasi na tupewa uzito wa juu na vyombo vyote vya usalama.
Naomba tulinganishe sakata la Lwakatare na haya ninayoyaweka hapa chini tuchanganue na kupima kwa kina juu ya Lwakatare kufunguliwa kesi ya Ugaidi je ni sawa au si sawa na kama ni sawa haya mengine yamefikia wapi katika kutatuliwa.

1.DIWANI NA KIKUNDI CHA MAUAJI

DIWANI wa Kata ya Mabila Wilaya ya Kyerwa Mkoani KageraChristian Songambele(CCM)anatuhumiwa kufanya mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyakatete Danes Damian(TLP) na Msaidizi wakeJohnson Damian waliofungiwa kwenye nyumba yake na kuteswa kabla ya kufariki.

Jina halisi la huyo diwani ni "Christian Selestine Kanyoro" Songambele ni jina la kikazi ila limezoeleka sana.
 
Huwa Inanisikitisha sana ninapo soma maandiko yanayo lihusisha jeshi la polisi na mauaji, na vitisho, na siasa chafu kama hizi., hua najiuliza ningefanya nini kama mimi ndiye ningekua katika nafasi ya Inspector General Mwema? ni jukumu kubwa na gumu sana alilo nalo Ng. Mwema,. nisingependa ku sema tu kwaurahisi kwamba anashindwa kuyasimamia haya sawasawa., kwa sababu nina imani na utu wake na uwajibikaji wake., lakini kwanini haya? kwanini kila kukicha ni jeshi la polisi,. ni usalama wa taifa? why???

inanifikisha mahali nina wasiwasi ipo nguvu inayofanya kazi kuratibu haya mambo na huenda iko juu ya mamlaka ya IGP Mwema., kwasababu haiwezekani taarifa hizi ziendelee kutapakaa tu mtaani za kulichafua jeshi la polisi kwa kiwango hiki halafu kuendelee tu kuwa kimya tukishughulika zaidi na vitu visivyo kuwa na uzito na kiviachiliya hivi viendelee kuwepo tu.,

sijui nguvu hiyo ni ipi?? lakini ipo.,
haupo mbali na ukweli tambua tu nchi yako haipo salama na inanuka damu iliyomwagika na itakayomwagika kuna shida kubwa sana ndugu.
 
Huyo diwani songambele angekuwa CHADEMA......
Serikali ya akina mwema ingekuwa na mkono mrefu, kwa 7bu ni diwani wa CCM ya akina Mwigulu Mchamba, Nepi na familia ya akina Ritz1 serkal inakuwa na mkono wa brka?? Mungu ucwasamehe hao wanajua waltendalo
 
Mkfumo ime collapse kabisa Tz wakati mwingine unaweza usiamini yale yanaandikwa na kusikika lakini ndiyo ukweli wenyewe!
 
Hivi kama kila mtanzaia angekuwa na uwezo wa kupata hz habari namna hii jiulize ingekuwaje? nadhani kuna viongozi wasingeweza tata kusimama mbele ya wananchi tena lakini ipo cku ukweli utajiani na mwenyekuona ataona na mwenyekusikia atasikia na kutambua kuwa tunaongozwa na watu majambazi.
 
Mtu kuwa mafichoni na gari?!!! Ngumu kumesa... Hebu wekeni namba za gari hapa...
 
Hii habari mbona imeninyong'onyeza sana, Tanzania ndo tumefikia hapa kweli?

Miye nasubiri kuona michango ya akina- Ritz, Chriss, Utaifa Kwanza na wengineo hawa tuone wanasemaje katika uzi huu, maana naona kimya kama vile hawapo. Hatari sana hawa jamaa.
 
Si walidai Pengo awaonyeshe alipo aliyemuua Padri Mushi ili wakamkamate kama kondoo? ...haya Mwakyembe kawaonyesha mbona wapo kimya? Dr Ulimboka kawatajia kabisa ni Ramadhani Ighondu mbona hawamkamati?
 
kwa kweli nchi hii inaitaji raisi anayejitambua ili akomeshe tabia zote chafu hasa zinazofanywa na viongozi, watendaji wa serikali na matajiri wanaodhamini vikundi vinavyotesa na kuua watanzania wasio na hatia, iv aya yote yanafanyika na kuendelea kunyika usalama wa taifa unakuwa wapi? tatizo usalama wa taifa umegeuzwa kuwa usalama wa viongozi wa juu.
 
Mmmh huyo diwan alishinda uchaguz kwel au aliiba kura?
Walimchagua kwa lipi?

Ni ajabu sana polis kushindwa kumkamata mtu maarufu kama huyo mpaka leo.

Picha, familia, ndg, jamaa na marafik, vyote hvyo bado mnashndwa kumkamata??

Kwel serikal imekuwa na mkono mfup na wenye kilema cha kujitakia.

Ule mkono mrefu wa serikal umeenda wap siku hiz??
Hatar kubwa inakuja TZ.

Watanzania tutajadili mengi sana na huenda haya ni trela tu. Kiufupi serikali imekuwa na mkono wa birika
 
Mmmh huyo diwan alishinda uchaguz kwel au aliiba kura?
Walimchagua kwa lipi?

Ni ajabu sana polis kushindwa kumkamata mtu maarufu kama huyo mpaka leo.

Picha, familia, ndg, jamaa na marafik, vyote hvyo bado mnashndwa kumkamata??

Kwel serikal imekuwa na mkono mfup na wenye kilema cha kujitakia.

Ule mkono mrefu wa serikal umeenda wap siku hiz??
Hatar kubwa inakuja TZ.

Muuaji akiwa polisi au mwanas sisiemu hana kesi - itatafutwa njia mpaka akwepe kushitakiwa au aachiliwe!!!.. Hata akishitakiwa askari magereza hawana uhuru naye atapelekwa mahakamani kwa magari ya kifahari kama muuaji wa MWANGOSI!!!
 
Back
Top Bottom