Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Hakika Tanzania tuna safari ndefu katika kufanya siasa za kweli. Wanasiasa wengi hapa Tanzania ni waigizaji na ndo maana kwa hakika inakuwa rahisi kutumika.
Wiki moja iliyopita, mjadala ulikuwa mkali sana juu ya Lugumi. Wanasiasa wote na hasa wa upinzani pamoja na vyombo vya habari mjadala mkuu ulikuwa juu ya LUGUMI. Magazeti mengi ukisoma front pages zake jina la Lugumi lilikuwa halikosekani.
Hata hivyo, baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutumbuliwa kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa, mjadala wa Lugumi umesahaulika. Hii inanikumbusha ya Prof Muhongo na ESCROW. Wakati Prof Muhongo anatangaza kujiuzulu, alitamka hivi. "INAVYOONEKANA HILI SUALA LA ESCROW MLENGWA HASA NI MIMI. NAAMINI KUWA MIMI NDIYE MWENYE UWEZO WA KUPOZA JOTO HILI LA ESCROW. HIVYO BASI ILI KUZIMA MJADALA HUU WA ESCROW, NATANGAZA RASMI KUJIUZULU NAFASI YANGU ILI TAIFA LIPATE MUDA WA KUSHUGHULIKIA MAMBO MENGINE BADALA YA KUJIKITA NA MJADALA WA ESCROW TU". Mwisho wa kunukuu.
Kosa la Kitwanga ni kushindwa kutafsiri mayowe ya Lugumi. Hakujua kuwa kama angeamua kujiweka pembeni mjadala huo usingeendelea. Kwa sisi tunaojua siasa za Tanzania na fitina zake, hakika ilikuwa ni rahisi kutafsiri kila mayowe yanayopigwa na wanasiasa wetu.