Ya Glazas na manchester united, ni mfano wa mahusiano yanayochosha

Oct 16, 2015
20
56
YA GLAZAS NA MANCHESTER UNITED, NI MFANO WA MAHUSIANO YANAYOCHOSHA.

Kalamu ya Nasri kulemba..

Baada ya washabiki wa Manchester United kuandamana jana,kulikua na mijadala mingi sana . Tukio hilo limezua hoja mchanganyiko kutoka kwa wadau mbali mbali .

Hoja kubwa kutoka kwa wadau hasi katika mtazamo, ni juu ya kwanini washabiki wanasindikiza kuondoka kwa glaza ikiwa familia hiyo kwenye suala la usajili haijawahi kuwa na mkono wa birika

"Kama wangekua hawaijali timu wasingewaleta makocha kama Louis Van Gal,Jose Mourinho na sasa Erick Ten Hag. wamesajili wachezaji wakubwa kama Paul Pgba, Cr 7,Sancho bruno fernandez na wengine wengi. Glaza wametumia zaidi ya £ 1.5 BL ."
Hizi ni pesa nyingi, kwa mtazamo wa matumizi ya pesa.wanaouliza wanahoja ya msingi sana.

Lakini twende kwenye uhalisia, hakuna asiepinga juu ya kile kinachoendelea kwenye klabu ya Manchester utd hasa kwenye suala la usajili chini ya utawala wa glaza, lakini kwanini watu wameonekana hawalidhishwi juu ya mwenendo wa utawala wa wa glaza?.

Timu haina mipango juu ya matumizi ya pesa.

Kusajili sio inshu ,ni vipi unasajili, sajili zako zinaakisi uhalisia wa mahitaji ya timu..? Upi mrejesho kwa wachezaji baada ya usajili.

United imesajili sana lakini jiulize ni mchezaji gani unayeweza kumuweka sokoni na akauzika,Klabu inatakuwa na mtazamo wa kuuza na kununua, ni vipi unaweza msajili mchezaji ambae ndani ya msimu mmoja tu hakuna klabu inayoweza kumasajili.

Jibu ni moja, pesa zilienda sehemu ambayo sio sahihi, hili limejionyesha kwa baadhi ya wachezaji waliopelekwa kwa mkopo sehemu na kushindwa kuonesha uwezo (Antony Martial, Eric Baily) ulitumia pesa nyingi kununua lakini hakukua na Uchambuzi wa kina, hii inamaana pesa nyingi zinaenda sehemu sio sahihi.

Bili ya mishahara kwa wachezaji .

Klabu ya Man United ndio inaongoza kwa kulipa mishahara mikubwa Epl, lakini jiulize kwa wachezaji gani waliopo, hii inaamana hakuna sera bora ya menedeleo ya soka yanayoweza mshawishi mchezaji tofauti na kumuahidi kumlipa pesa nyingi. Yaani unakua na kikosi ghali chenye wachezaji wa kawaida. Aibu.

Hakuna mpango mkakati wa maendeleo ya soka.

Nini vision ya United ndani ya hii miaka 10 iliyopita, sera yao ni kuzalisha wachezaji au kununua wachezaji bora kuimarisha timu.. Je mbona hakuna hata kimoja kati ya hivyo kilichofanikiwa. Sera ya Man city ni kununua mchezaji bora sokoni, na imewalipa .

Barca kuna kipindi walitumia zaidi timu za vijana, ikawalipa..nyakati zikapita La masia ikawa hazilishi tena wachezaj mahili, wakatoka nje ya sera hiyo wakaona haiwalipi na sasa wamerudi tena La masia na imeanza kuwalipa.

Maana iliyoshiba ya kuwa na mipango Halisi ya soka.. Kubadilika kutokana na mazingira.Vipi kwa United chini ya Glaza? klabu inaenda tu kama kondoo!!

Madeni yanazidi ongezeka..

Sio kweli pesa za usajili zinatoka kwa Glaza, hawa jamaa huchukua kiasi chao chote cha faida na kisha kiasi kingine kinachobakia katika mgao ndicho utumika United kujiendesha, hii inamaana matunizi yanapokua makubwa kuliko kipato hulazika timu kwenda kukopa ili kufidia bajeti.

Glaza wanakula kuku,hawausiki kabisa na madeni, klabu inabakia inahaha tu na madeni kwenye kuyalipa.

Kwanini washabiki hawautaki uongozi wa Glaza.

Sababu kubwa sio kusajili, ila ni namna timu inavyoendeshwa,kungekua na walau mwanga katika maendeleo ya soka hata bila kusajili hakuna mtu angelalamika, ni wazi glaza wanajali zaidi maslahi yao kuliko ya timu.

Kuna kipindi Rio Ferdinand aliwahi lalamika kuna baadhi ya maeneo katika uwanja wa Old traffold yana vuja pindi mvua inaponyesha.

Uwanja upo vile vile miaka na miaka, hata kupiga lipu baadhi ya ameneo hakuna, Inasikitisha sana klabu inayoingiza pesa nyingi zaidi dunian haina kiwanja kizuri kama walichonacho Tottenham au westham. Aibu sana.

Hakuna namna Glaza waiachie hii timu,kama watabahatika kuendelea kubakia hapo,United inaelekea kubakia katika historia kama ambavyo walivyo Nottigham forest kwasasa.

Glazers Out.

Nasri Kulemba
FB_IMG_1687894827125.jpg
 
Wanasajili watakapojisikia wao na sio umuhimu wa potentional requirements kwa klabu. Hivi mtu kama Mbappe tunashindwa kweli kuweka mkono pale Psg mpaka tuuze kwanza wachezaji??
 
Siku chache zijazo hatutakuwa nao hao.

Tena mmiliki mpya amrudishe Ralf Rangnick kitengo cha juu aanze kazi ya kujenga system ya uendeshaji bora.

Hata Murtough na Arnold hawafai ni majipu mengine ambayo mwakani hayatakiwi kufika.

Watafutwe watu wa soka waiinue tena timu,kuhusu visions baadhi Sheikh Jassim atafanyje kazi hasa uboreshaji wa miundombinu ya uwanja n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom