Ya DC na makanisa wilayani Mbeya

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
230
[h=3]DC atoboa siri nzito kuhusu waombaji[/h]

*Ataja chanzo cha kuungua kwa soko

Na Charles Mwakipesile Mbeya

MKUU wa Wilaya ya Mbeya Bw. Evans Balama, amewashangaza umma uliojitokeza kumsikiliza katika Kanisa la Moravian Yerusalem Jijini hapa baada ya
kutoa tuhuma nzito dhidi ya Kanisa moja kuwa viongozi wake wanawaombea akina mama tasa kisha kupata ujauzito na kujifungua watoto wanaogeuka kuwa nyoka.

Akizungumza katika ibada ya mazishi ya Bw. Ferick Cheyo (92), ambaye ni baba mzazi wa Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo, mkuu huyo wa wilaya alisema viongozi wa makanisa wanayo changamoto ya kudhibiti uhalifu mkubwa ambao umekuwa ukizaliwa Mkoani Mbeya kila kunapo kucha.

Mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa amepewa nafasi ya kusalimia alisema hivi karibuni alifuatwa na kundi la kinamama ambao miongoni mwao ni wafanyabishara wa soko la sido lililoungua ambao walimweleza kuwa wao wamekorofishana na kiongozi wao wa kanisa walilokuwa wanasali awali kutokana na kumweleza wazi kuwa ni mshirikina asiye na Mungu kama anavyojitangaza.

Bw. Balama ambaye ni Ofisa wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ) mstaafu alisema akina mama hao walimweleza wazi tukio kubwa katika kanisa hilo ambalo alisema jina analo na kiongozi mhusika anayetuhumiwa.

Alikinuu akina mama hao mkuu huyo wa wilaya alisema siku moja mama mmoja mwenzao ambaye hakujaliwa kupata mtoto alinda kupata maombi maalumu katika kanisa hilo na baada ya kuombewa alipata ujauzito lakini baada ya kujifungua alipewa shrti na mtume huyo kuwa asithubutu kumnyonyesha mtoto huyo maziwa yake.

Alisema badala yake alielekezwa siku zote ampatie mtoto wake maziwa ya ng’ombe sharti ambalo alitii kwa kumtumia binti yake wa kazi kutokana na yeye kuwa mfanyabiashara asiyeshinda nyumbani.

Hata hivyo alisema binti wa kazi alishangaa kuona kila anapomwacha mtoto huyo kwenye kiti ama kitandani akiwa ameacha chupa ya maziwa lita moja akitoka na kurudi maziwa yote yamekwisha huku akiwa hajui ni nani aliyekuwa amembeba mtoto na kumfungulia maziwa.

“Ndugu zangu si utani yametokea hapa Mbeya, binti huyo wa kazi aliamua kutega mtego kwa kuacha maziwa kisha kuweka maziwa pembeni na kufunga mlango, akwa anachungulia kwenye tundu dogo lililopo mlangoni, nawaambia ndugu zangu alishangaa kuona mtoto amegeuka kuwa nyoka mkubwa na kuanza kunywa maziwa kwa kasi ya ajabu,”alisema huku waumini wakizizima kwa mshangao.

Alisema alisikiliza maelezo ya akina mama hao kwa umakini na wakawa tayari kumpeleka kwa kiongozi huyo wa kanisa hilo ambaye amekuwa akikusanya watu wengi wakiwemo wagonjwa wenye matatizo mbali mbali ambapo alisema kuwa aliwataka kutilia na kuiacha serikali kufanya uchunguzi wake.

Aliwaeleza viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na wachungaji kuwa
imefika wakati tabia hiyo kwa Mkoa wa Mbeya inapaswa kukomeshwa ili kuepuka laana kubwa ambayo ingeweza kutokea wakati wowote kutokana na hasira ya Mungu kuweza kutokea kwa wanaofanya dhambi hiyo mbaya.

Alisema mbali na matukio hayo pia kiongozi huyo ndiye anayedaiwa kuwa aliwaahidi wafanyabishara hao kuwa atahakikisha anachoma soko hilo jambo ambalo lilitokea kama alivyoahidi na kuteketeza mali za wajasiriamali wengi waliokuwa wanafanya biashara katika eneo hilo .

Kiongozi wa ibada hiyo Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi mMhungaji Nosigwe Buya, alilaani matukio hayo ya kishirikana yanayowahusisha watumishi wa Mungu na kuongoza maombi makubwa ya kutubu kwa ajili ya Mbeya na kuwaonya waumini wenye tabia ya kukimbilia makanisa yanayoibuka kama uyoga bila kujua msingi wake.

Hivi karibuni kumezuka huduma moja ambayo imekuwa ikilalamikiwa na watu wengi kutokana na kukusanya watu wengi wakiongozwa na wagonjwa ambao wamekuwa wakilazwa kwenye majani wakidai kusubiri kuombewa ambapo baada ya kupata huduma huwa hupewa masharti ya kutorudi katika makanisa yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom