Dunia nzima ilitega masikio kusikilizia nini kingetokea baada ya KATIBA ya Burundi kutolewa tafasiri kipengele cha ukomo wa mihula ya uraisi na mwanasheria mkuu wa Burundi.
Kwa mjibu wa sheria (According to AG wa Burundi), raisi Nkurunzinza aliruhusiwa kikatiba kuwania kipindi kingine....cha tatu ingawa "kikatiba kama ilivyofasiriwa na AG ni mara ya pili.
Binafsi mpaka leo nakuna kichwa na sheria siijui,nabaki kusikiliza na kuchambua kichwa kichwa mpaka leo nimebaki na maswali kichwani.
Hivi katiba ya nchi ni mali ya nani? Hivi katiba ya nchi ni kwa manufaa ya nani? Katiba ni kwa ajili ya wananchi au wananchi kwa ajili ya katiba?
Kwa ninavyofikiria,hawa watu wanaoitwa wanasheria wanauwezo wa kubadirisha mbili kuwa moja kwa korejea vifungu na wakahalalisha kabisaaaa. Siamini kama kweli AG wa Burundi alitafsiri sawa,kama alikuwa sawa sasa kwa nini umma wa warundi waliingia barabarani,je hawaijui katiba yao?
Hili la Burundi nalilinganisha na hapa kwetu,upande wa Tanzania visiwani nashindwa kuelewa nani yuko sahihi kwa tafsiri ya katiba. Kuna pande mbili zimekuwa zinakuja na uhali au kutokuwa na uhalali wa Rais Shein kuendelea kuongoza serikali ya Zanzibar.
Upande unaosema yuko halali kikatiba wanarejea na vifungu vya katiba na kwa tafsiri ni kweli vinamruhusu, upande wa pili unadai hayuko kikatiba na vinakuja na rejea ya vifungu vya katiba hiyohiyo ya Zanzibar na vinakuwa sawa kuwa haruhusiwi!
Binafsi nashindwa sasa kupata jibu, je,nani yuko sawa maana kila u[pande kuna wanasheria wa kutafsiri vifungu na wanatumia katiba hiyo hiyo moja, hivi sasa hizi katiba ni za nani na zimewekwa kwa faida ya nani?
Je, Tanzania tutakuwa na nguvu ya kusuluhisha mgogoro wa Burundi wakati na hapa kwetu bado suala la kutafsiri katiba moja yenye maana mbili tofauti tunalo?
Wanajamvi mnaojua kutafsiri vifungu nisaidieni,mie nimegota.