X and Y Katiba mpya na Ya kale

Ras John I

Member
Oct 3, 2017
39
22
X: Kwani nyie mnataka nini?
Y: TUNATAKA KATIBA MPYA.
X: Katiba ni nini?
Y: SISI HATUIJUI.
X: Kwani ile ya zamani ina Tatizo gani!?
Y: HATUJUI ILA TUNATAKA KATIBA MPYA?
X: Sasa kwa nini mnataka katiba mpya?
Y: HATUJUI PIA.

Mimi kama mtanzania ni kweli katiba ni jambo la msingi, je mtanzania wa kawaida anaijua katiba? Hebu jaribu kuuliza wazazi wako juu ya hilo na utafakari.

Kupata katiba mpya sio dawa ya kuinua maisha ya mtanzania yawe bora, kwanza lazima tufanye ukombozi wa akili na fikra za kila mtanzania ili kila mmoja aeelewe nini maana ya katiba, katiba ya zamani na kwanini tunataka katiba mpya.

Upatikanaji wa katiba mpya na kuwa na watanzania wenye ufikiri ule ule , Akili zile zile bado hautomkomboa mtanzania sana sana utaleta shida kwa mtanzania wa kawaida.

Lazma tuamue kwa dhati kumpatia mtanzania elimu ya ukombozi wa kweli bila kutumia vyama vya siasa, wala umaarufu wetu kumdanganya na kumteka mtanzania ambaye yeye muda wote anasubiri kutafutiwa yeye ameze.

BILA HIVYO BADO WALE WACHACHE WASIOFANYA KAZI WATAZIDI KUNEEMEKA HUKU TULIO WENGI NA WACHAKARIKAJI TUKIFA NA KUFUNJWA VIUNGO BILA KUJUA KWANINI TUMEAMUA KUPIGANA VITA TUSIYOIJUA SABABU YAKE.
b88941a90a1a8172514e093d7264f753.jpg
76d9750c377e46676f2e1bc2e7d041ed.jpg
 
We umehamia kutoka nchi gani? Mbona kama ni issue ya awareness tume ya Jaji Warioba ilishamalza hyo kazi maoni yakakusanywa tena kuanzia ngaz ya vijiji, wataalamu wakayachambua na rasimu tayri ipo.
 
We umehamia kutoka nchi gani? Mbona kama ni issue ya awareness tume ya Jaji Warioba ilishamalza hyo kazi maoni yakakusanywa tena kuanzia ngaz ya vijiji, wataalamu wakayachambua na rasimu tayri ipo.
Pole kaka hebu waulize wakina mama wanaotembea na ndo za maji km 12 uwaulize
 
Back
Top Bottom