WWIII

WWIII

Kufuatia Vitisho Vya Nyuklia Vya Korea Kaskazini, China Imesogeza Majeshi Yake Kwa Wingi Kwenye Mpaka Wake Na Nchi Hiyo. Wakati Huo Huo, China Imesogeza Makombora Yake Matatu Aina Ya Dong Feng - 41. Kombora La DF-41 Lina Uzito Wa Tani 80 Na Urefu Wa Mita 21. Lina Uwezo Wa Kwenda Kilomita 8.5073 Kwa Sekunde Likifyatuliwa. Lina Uwezo Wa Kubeba Vichwa Vya Nyuklia. Kombora La DF-41 Pia Lina Uwezo Wa Kwenda Kilomita Za Jumla 15,000.
123a06ba1f598690ec1c516a0639b227.jpg

2f512a10bb16d62ebfc6d8f958a17456.jpg

2998bfc0a2132541fc5b376d0dc93732.jpg
Sipati picha siku linarushwa afu liangukie 2M kutoka yalipo. Siku hiyo ndo watajua kucheza reggae wakati wimbo ni RnB.
 
Yote safi, kama vipi wakinukishe tu, hii dunia ichafuke mapema tuchambue zipi mbichi, hamna haja ya kuishi kwa wasiwasi kila siku.
Huyo dogo wa Korea kichwa cha mwenda wazimu, siku hizi hamsklizi Mchina, ilhali huyo huyo Mchina ndiye alikua akimkingia kifua.

Dogo alivyo chizi, kafanya majaribio ya kiuchokozi juzi wakati Marekani na Uchina wamekutana kumjadili, hiyo ni baada ya chizi mwenzake bwana Trump kusema atafanya kweli iwapo Uchina hawatamtuliza dogo.

Ipo siku hayo makombora ya dogo yatakosa njia na kujichanganya yatue Japani, na hapo ndio patakua patamu maana itakua mwendo wa popcorn na kutazama movie.
Aisee we jamaa umeanza kiswahili kirefu namna hii[emoji2] [emoji2] [emoji2]

Angalia sana siku ukienda Kenya watakufukuza kwa hivi vi misemo vyako[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]

(Kidding)
 
Back
Top Bottom