WTM: Kampuni iliyomponza Chami na Ekelege...

MDOSI

Member
Joined
Aug 24, 2012
Posts
22
Reaction score
8
Habari tulizozipata kutoka gazeti la raia mwema lililotolewa leo ni kwamba waziri huyu amekatiwa mshiko wa nguvu kiasi cha kukubali kampuni iliyosababisha ekelege afukuzwe kazi.
Inasemekana kuwa baada ya kupewa kitita cha $50,000 Kigoda alisahau yote yaliyosababisha wenzake wafukuzwe kazi akaamua kuishinikiza bodi ya wakurugenzi ya TBS kipatia tenda ya ukaguzi wa magari WTM kampuni inayomilikiwa na mtoto wa aliekuwa mkurugenzi wa zamani wa TBS na kumrudisha kazini ekelege.
Inaaminika kuwa licha yahizo hela kigoda aliahidiwa gari aina ya bmw x5 na mambo mengi mengine.
Hii inakatisha tamaa sana hasa baada ya kigoda kuingia kwa mwara mzito kwa kumtimua Ekelege halafu leo anataka kulamba matapishi yake. kweli tutafika na huyu ndo aliekuwa akisema atafufua kiwanda cha general tyre
sie twaangalia kwa macho ati.
njaa mbaya sana
 
Mkuu hii habari yako haijakaa sawa,em gagadua vizuri ieleweke ili wadau tupate pa kuanzia.
 
Hii sumary yako imepindapinda. Tafuta full electronic information mwaga hapa watu tusome tupate pa kuchangia. Hii yako ni kama DRY BONES.
 
Habari




Waziri, Bodi watishiana










Mary Victor

Toleo la 273
19 Dec 2012













  • Ni kuhusu TBS, maagizo yatolewa Dk. Kigoda aburuzwe kortini





WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda anatuhumiwa kuibeba na hatimaye kushinikiza ipatiwe kazi ya kufanya ukaguzi wa magari nje ya nchi kampuni ambayo Bodi ya Shirika la Viwango nchini (TBS) iliikataa kwa sababu ya kutokidhi masharti na vigezo vya zabuni, Raia Mwema, limebaini.
Kutokana na hali hiyo, Bodi ya TBS imeiagiza menejimenti ya shirika hilo kumfikisha waziri huyo katika Mahakama ya Biashara, ili pamoja na mambo mengine, Mahakama hiyo ibatilishe uamuzi wa Dk. Kigoda unaodaiwa kuingilia mchakato wa zabuni wenye lengo la kupata kampuni makini zitakazofanya kazi hiyo ya ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini kutoka nchi za nje.
Kwa mujibu wa habari tulizonazo, kampuni ambayo Dk. Kigoda anadaiwa kuishinikiza Bodi ya TBS iipatie kazi ya ukaguzi wa magari nje ya nchi imetajwa kwa jina la W.T.M ambayo Agosti mwaka huu, ilisimamishwa na Bodi ya TBS kuendelea na majukumu yake ya ukaguzi.
Kati ya sababu za kuisimamisha kampuni kuendelea na majukumu yake ni pamoja na tuhuma zilizosababisha aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS, Charles Ekerege, kusimamishwa kazi na pia kutokuwa na ufanisi katika utekelezaji na usimamiaji wa majukumu yake hayo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya TBS zinasema uongozi wa Bodi ya Shirika hilo, umegomea shinikizo hilo la Waziri Dk. Kigoda kwa kuipatia kazi kampuni hiyo nje ya utaratibu wa zabuni, hali ambayo imeilazimu Bodi kuitaka menejimenti ya TBS kumfungulia mashitaka waziri katika Mahakama ya Biashara ili pamoja na mambo mengine iweze kutengua shinikizo hilo la waziri.
Vyanzo kadhaa vya habari hizi, vimeeleza kwamba uamuzi huo wa Dk. Kigoda umetokana na mambo mawili. Mosi, ni uwoga wa Waziri Kigoda kwa wabunge, na pili, ni kumpa upendeleo maalumu mmiliki wa kampuni hiyo, Mtanzania, ambaye anadaiwa kuwa mtoto wa kigogo mmoja ambaye amewahi kufanya kazi ndani ya shirika hilo.
Kampuni hiyo ya W.T.M ilikuwa katika orodha ya kampuni ambazo huko nyuma, chini ya Mkurugenzi Ekerege, zilipewa kazi ya kukagua magari nje ya nchi kabla ya kuyasafirisha kuja nchini, kama moja ya njia ya kudhibiti nchi kugeuzwa dampo la magari mabovu.
Hata hivyo, kampuni hiyo na baadhi ya nyingine, zinadaiwa kufanya kazi chini ya ufanisi, huku nyingine zikidaiwa kuwa kampuni hewa, na hivyo kulisababishia hasara kubwa shirika hilo, hali iliyoamsha mjadala mzito bungeni ambao ulisababisha kusimamishwa kwa Ekelege ili kupisha uchunguzi wa suala hilo.
Sakata hilo la kuwapo kampuni hewa na zinazofanya kazi ya ukaguzi wa magari chini ya ufanisi, ndiko kulikosababisha kung'olewa pia kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, na badala yake Rais Jakaya Kikwete kumteua Waziri Kigoda katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri aliyoyafanya Mei, mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi wa TBS, Dominic Mwakangale, amethibitisha kuwapo kwa mgangano huo wa uamuzi kati ya Dk. Kigoda, Bodi ya TBS na Menejimenti yake.
Aidha, Mwakangale ambaye pia ni Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora ndani ya TBS, alikiri kupokea agizo la Bodi ya TBS, la kuitaka Menejimenti yake kumshtaki Dk. Kigoda katika Mahakama ya Biashara.
"Hatujakataa kutii agizo la Bodi (la kumfikisha Dk Kigoda katika Mahakama ya Biashara). Tulipopokea agizo lile tulimpelekea mwanasheria wetu, kwa hiyo hadi sasa hatujapata ushauri wake, na tunasubiri," alisema Mwakangale.
Raia Mwema lilifanya juhudi za kumtafuta Waziri Kigoda, ili pamoja na mambo mengine aweze kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo.
Juhudi hizo za kumpata Dk. Kigoda kwa njia ya simu yake ya mkononi zilifanikiwa juzi Jumatatu, baada ya ujumbe mfupi aliokuwa ametumiwa wiki iliyopita kuonyesha kwamba umemfikia.
Baada ya kupokea ujumbe wetu, Dk Kigoda aliomba apewe dakika tano mbele ili kutolea ufafanuzi suala hilo. Hata hivyo, Dk Kigoda hakuweza kujibu lolote hata baada ya dakika 30, na alipopigiwa na mwandishi wetu kumkumbusha juu ya ahadi yake hiyo, aliomba apewe muda zaidi akisema angejibu kupitia ujumbe mfupi wa simu yake ya mkononi.
"Naomba nikujibu baada ya dakika tano, nitakujibu kwa ujumbe mfupi wa simu (sms),"alisema Kigoda.
Mwakangale alizitaja kampuni ambazo zilikuwa kwenye mchakato wa mwisho wa zabuni ya kuomba kazi ya ukaguzi huo wa magari nje ya nchi, kabla ya Waziri Dk. Kigoda kuingilia kati na kushinikiza iingizwe pia katika orodha hiyo kampuni hiyo ya W.T.M. ni Japan Auto Appraisal- JAAI (Minato-Ku, Japan), Wilna International (Tokyo, Japan), Auto Terminal Japan Ltd (Japan), East Africa Automobile Services Co. Ltd (Watanzania wenye ofisi Japan).
Jabal Kilimanjaro na Auto Elect. Mech (Sharjah, U.A.E), Serengeti Freight & Forwarders Ltd (London, Uingereza), Unit 92 Thames (Industrial Park, Princess Margaret Road, East Tilbury-Uingereza).
Akielezea kwa nini kampuni ya W.T.M, inayomilikiwa na wazalendo haikuweza kuchaguliwa na menejimenti ya TBS, Mwakangale anasema: "Yapo masuala mengi, lakini kubwa zaidi kampuni hii imeshindwa kulipa fedha TBS kwa wakati."
Kabla ya Waziri Dk. Kigoda kuagiza kampuni hiyo ya W.T.M. iingizwe katika kampuni hizo zilizopatikana katika mchakato wa mwisho, habari zinasema kampuni hiyo ndiyo iliyokata rufani kwa Waziri huyo ikilalamikia hatua hiyo ya menejimenti na Bodi ya TBS kuiondoa katika orodha ya kampuni zilizoingia hatua ya mwisho.
Mmoja wa wajumbe wa Bodi mpya ya TBS aliyezungumza na gazeti hili kuhusu sakata hilo kwa sharti la kutotajwa jina lake kutokana na sababu za wazi kabisa, anasema:
"Sisi kama Bodi ya TBS, hatukukubaliana katika suala la kuipatia kampuni yenye tuhuma (W.T.M) na tayari ilishafungiwa tangu Agosti (mwaka huu) kutokana na utendaji usioridhisha. Mbali na hilo, yapo pia masuala mengine ambayo tusingependa kuyaweka wazi yaliyomfanya Waziri (Dk. Kigoda) avunje Bodi.
"Hata hivyo, tumeiagiza menejimenti (ya TBS) ilifikishe suala la Waziri Mahakama ya Biashara. Kinachofanywa na Waziri ni kutokana na hofu ya kuwaogopa wabunge, ndiyo maana baadhi yao wanafanya uamuzi unaokinzana.
"W.T.M , ni kampuni ya Mtanzania, taarifa ambazo tunazo, ni kwamba mama wa mmiliki wa kampuni hiyo ambaye kwa sasa ni marehemu, alikuwa ni mtumishi wa TBS kwa miaka kadhaa iliyopita. Kijana huyo anapewa kazi hii kama heshima kwa marehemu mama yake mzazi.
"Hivyo basi kijana huyo ndiye aliyeanza kazi ya kukagua magari nje ya nchi hadi pale TBS ilipoamua kumsimamisha Agosti mwaka huu kutokana na ufanisi wa shughuli zake kuwa mdogo, na pia kuchelewesha malipo pamoja na masuala mengine.
"Baada ya kusimamishwa , aliamua kukata rufaa kwa Waziri , ndipo Dk. Kigoda alipoiagiza TBS kuwa mfanyabiashara huyo arudishwe kwa kutumia taratibu za zamani. Menejimenti ya TBS ilipoleta suala hili kwenye Bodi, tulilikataa kutokana na kwamba kwa sasa hatutumii taratibu hizo za zamani katika utoaji wa zabuni za Serikali.
"Kwa kuwa tayari tulishatangaza tenda (zabuni) kwa kampuni kuomba kazi hiyo, yeye (W.T.M) hakuomba, na kwa kuwa amechelewa asingeweza kuomba tena...zipo taarifa ambazo Bodi ilizipata kwamba amekuwa akitoa vyeti nchini Uingereza kwa waagizaji magari nchini pasipo magari hayo kukaguliwa.
"Yapo baadhi ya magari ya wafanyabiashara wakubwa yameingizwa nchini kwa utaratibu huo. Kwa misingi hiyo, Bodi iliona hakukuwa na sababu ya kumrudisha mtu wa namna hiyo."
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Deo Filikunjombe , alipotakiwa kuzungumza mgogoro huo mpya baina ya Waziri na Bodi ya TBS, alisema:
"W.T.M ni kampuni mbovu haifai hata kupewa kazi tena na TBS. Kwanza ni kampuni ambayo ilishafungiwa kukagua magari. Namheshimu sana Dk. Kigoda, lakini katika hili nitamshangaa sana kama anaikingia kifua kampuni yenye tuhuma lukuki kwa kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo."
Dk Kigoda, mara tu baada ya kukabidhiwa wizara hiyo, alichukua hatua kadhaa, zikiwamo za kumsimamisha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Ekelege ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake kuhusu uendeshaji wa shirika hilo. Hadi sasa, uchunguz huo bado unaendelea.
Aidha, Dk Kigoda ndiye aliyevunja iliyokuwa Bodi ya TBS, chini ya Mwenyekiti, Oliva Mhaiki. Wajumbe wengine wa Bodi hiyo na maeneo wanayowakilisha yakiwa kwenye mabano, ni pamoja na Donald Chidowu (Katiba na Sheria), Rashid Salim (Viwanda na Biashara Zanzibar), Dk Bertha Maegga (Afya na Ustawi wa Jamii), Odilo Majengo (Viwanda na Biashara) na Profesa Ntengwa Mdoe (Chuo Kikuu cha Sokoine- SUA).
Wengine ni Peter Machunde (Taasisi ya Sekta Binafsi -TPSF), Dk. Godfrey Mariki (Tume ya Ushindani wa Bidhaa-FCC), Suzy Laizer (SME's), Elpina Mlaki (Fedha na Uchumi) na George Simbachawene (Mbunge wa Kibakwe, sasa Naibu Waziri, Nishati na Madini
 
Nimeyakuta haya mjengwa blog na sikuamini macho yangu kuwa haya madudu bado yapo
Raia mwema




MRABA WA MAGGID

Kioja cha kufunga mwaka: Dk Kigoda anapoibuka na ‘madudu' ya Ekerege


Maggid Mjengwa

"EX Africa simper aliquid novi." Maana yake; "Kila kukicha kitazuka kioja kingine Afrika." (Ptolemy, Mwanafalsafa wa Kiyunani alipata kuandika.
Kwa hakika, kilichoandikwa ukurasa wa kwanza kwenye gazeti hili, Toleo lililopita, huenda kitakuwa ni kioja cha kutufungia mwaka huu wa 2012. Toleo lililopita la Raia Mwema, liliandika: Waziri, Bodi watishiana. Kisha likaendelea:
"Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, anatuhumiwa kuibeba na hatimaye kushinikiza ipatiwe kazi ya kufanya ukaguzi wa magari nje ya nchi kampuni ambayo Bodi ya Shirika la Viwango nchini (TBS) iliikataa kwa sababu ya kutokidhi masharti na vigezo vya zabuni.
"Kutokana na hali hiyo, Bodi ya TBS imeiagiza menejimenti ya shirika hilo kumfikisha waziri huyo katika Mahakama ya Biashara, ili pamoja na mambo mengine, Mahakama hiyo ibatilishe uamuzi wa Dk Kigoda unaodaiwa kuingilia mchakato wa zabuni wenye lengo la kupata kampuni makini zitakazofanya kazi hiyo ya ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini kutoka nchi za nje.
"Kwa mujibu wa habari tulizonazo, kampuni ambayo Dk Kigoda anadaiwa kuishinikiza Bodi ya TBS iipatie kazi ya ukaguzi wa magari nje ya nchi, imetajwa kwa jina la W.T.M ambayo Agosti mwaka huu, ilisimamishwa na Bodi ya TBS kuendelea na majukumu yake ya ukaguzi.
"Kati ya sababu za kuisimamisha kampuni kuendelea na majukumu yake ni pamoja na tuhuma zilizosababisha aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS, Charles Ekerege, kusimamishwa kazi na pia kutokuwa na ufanisi katika utekelezaji na usimamiaji wa majukumu yake hayo.
"Habari za uhakika kutoka ndani ya TBS zinasema uongozi wa Bodi ya Shirika hilo, umegomea shinikizo hilo la Waziri Dk Kigoda kwa kuipatia kazi kampuni hiyo nje ya utaratibu wa zabuni, hali ambayo imeilazimu Bodi kuitaka menejimenti ya TBS kumfungulia mashitaka waziri katika Mahakama ya Biashara ili pamoja na mambo mengine iweze kutengua shinikizo hilo la waziri."
Kwa maoni yangu, haya si mapya, maana yalipata kuwekwa wazi na kuna tulioandika makala. Itakumbukwa kwamba Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ndiyo iliyobaini madudu makubwa kwenye Shirika letu hili lenye dhamana ya udhibiti wa viwango vya bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinazoingizwa kutoka nje ya nchi.
Kashfa hii inamhusisha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Udhibiti wa Viwango nchini (TBS), Charles Ekerege. Kilichobainika ni wizi na ubadhilifu mkubwa, ukiambatana na hujuma za mapato ya kodi za viwango. Wajumbe wale wa Kamati ya Bunge walifika hadi Hongkong na Singapore.
Huko wakayaona madudu waliyoyaona. Kumbe, madudu yale ya TBS ya Ekerege yalitambaa hadi kwenye kona nyingine za dunia. Kuna Watanzania wazalendo wa nchi hii waliosaidia kubainisha ukweli huu. Ona hapa kinachosemwa mtandaoni na Watanzania wenzetu walio ughaibuni.
"Bwana Mjengwa; hapa UK kuna kampuni moja mimi nasema ni ya kitapeli kwani bila shaka imeanzishwa na wakubwa fulani kwa manufaa yao na vijana wao wanaoishi hapa UK. Hii kampuni inajiita WTM UTILITY SEVICES LTD (TBS no: TZS 698.2003). Hawa ukitaka kusafirisha gari kuja Bongo, wanasema lazima walikague ubora wake, lakini kitu cha ajabu hakuna ukaguzi huo unaofanyika.
"Wewe unawapigia simu (unawambia) una gari, kisha una wafaksia kadi ya gari wanakuandikia ‘certificate' au kama una haraka, unakutana nao mitaani maeneo ya ‘East. Hapo wanakubandikia papo hapo! Kwa kweli inakera.
"Watu wana tengenezeana michongo na Serikali haipati kitu. Sijui hao watu wa TBS waliowapa kibali cha shughuli hiyo kama wana jua chochote? Nadhani na wao wana fungu lao. Naomba wahusika wizarani wachunguze suala hili, basi kama kuna ulazima wa ukaguzi, ufanyike nyumbani angalau walalahoi nao watapata ajira na Serikali itaambulia (kitu), na si pesa si kidogo. Mwenyekiti, nawasilisha. Shukrani, Whistleblower, UK."
Kwa hakika, nchi yetu inapoteza mapato makubwa yanayotokana na uhuni na utapeli unaofanywa na watendaji wetu, na kioja kingine kwenye kampuni iliyopewa uwakala wa ukaguzi na TBS ya huko UK inayoitwa WTM Utility Services Ltd ni kwamba kwenye tovuti yao ya:http://www.wtmutilityservices.com, wanaonyesha kuwa wana ushirika na kampuni zifuatazo; Great Western Railway,
Binafsi, nichtkue fursa hii kuipongeza Bodi ya TBS kwa kuonyesha msimamo katika hili. Naamini Waziri mhusika naye ataelewa haraka juu ya utata uliopo kwenye suala hili, na hivyo kulinusuru taifa na kupoteza mapato makubwa kutokana na biashara hizi za kihuni.
Watanzania tunapata hofu kwa kuona hata tuliowakabidhi idara nyeti kwa maisha ya Mtanzania, wanashiriki vitendo vya utapeli. Maana tulipata hata kuambiwa kwamba TBS hawana ofisi Singapore na Hong-Kong. Wana ofisi hewa. Hivyo basi, na makusanyo ya dola mia tatu za gharama za kuangalia viwango kwa gari moja, yanaishia kwenye mifuko ya wajanja. Hewani!
Tuliambiwa kwamba hata wabunge wetu walipokuwa huko, waliweza kununua stika feki za TBS kwenye mitaa ya huko Singapore. Hiyo yaweza kumaanisha pia kwamba hata baadhi ya bidhaa tunazonunua hapa nchini zimewekwa stika feki za TBS. Wahusika wachukue hatua sasa, wakichelewa sana, basi, hatua zichukuliwe dhidi yao. Heri ya Krismasi












​
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo na italiwa na wenye meno!.
Kwa vile kuna "wenye nchi", "wala nchi" na "wananchi", kama shinikizo la kampuni hiyo ni ya "wenye nchi", basi hiyo bodi ya TBS iliyoweka kauzibe ndio itangoka, na tenda itaendelea!.
P.
 
Hii ndo Tanzania
Mkuu inasikitisha sana pale waziri bila aibu anashinikiza kikampuni ambacho hata ofisi hakina kipewe tenda , huu ni upuudhi uliokithiri na kama ikitokea kweli kapewa basi moto wake hautakuwa mdogo kwa sababu kuna jamaa wa zile kampuni ambazo tayari zimeshinda wanajipanga kumwaga mboga kama walivyofanya hapo mwanzo kwa ekerege na chami
 
inawezekana kabisa waziri hayajuia haya madudu hapa chini
[h=3]Mjumbe Mwenye Hasira Kali Sana: " Mwenyekiti, Nakuomba uufikishe Ujumbe Huu Kwa Waziri Kigoda"[/h]
 
Kaka pole sana, chejea Davis MoshA WEWE, hujui nani yule? huyo mlinzi wa mali za mama BMW :majani7:😛op2:😛op2:
 
Kaka pole sana, chejea Davis MoshA WEWE, hujui nani yule? huyo mlinzi wa mali za mama BMW :majani7:😛op2:😛op2:
mkuu hiyo ilikuwa zamani ambapo hela itatumika kimabavu lakini sasa watu hawaogopi kumuumbua mtu, wakileta mchezo patachimbika, Nadhani unamkumbuka chami na ekerege??
 
Habari imeharibu furaha yoote ya krismas hata mwaka mpya sidhan kama ntaula kwa furaha. Nimekumbuka! Ndo maana salary haijatoka hadi leoooh! Wajanja washakula chao mapema sis twahangaika tu hapa. Huko serikali kuu hebu amkeni mnatutesa huku kitaa life gumu, kila k2 bei juu kuko_mpaseti madudu yenu!? Loh!
 
siamini macho yangu,
Na humu pia????????????????????????????!!!!!!!!!!!!!!!
 

[h=2]
Kimenuka TBS, baada ya POAC kuvunjwa waziri Kigoda anaiendesha TBS kama kijiwe cha kupigia deal[/h]
WAKATI kamati mbalimbali za Bunge zikiwa zimevunjwa, umejitokeza mwanya kwa baadhi ya mawaziri hasa wenye mivutano kati yao na bodi zinazoendesha baadhi ya mashirika yaliyoko katika mamlaka zao kucheza rafu, Raia Mwema, limeelezwa.

Tangu Spika wa Bunge kupitia Kamati ya Kanuni za Bunge, Ijumaa wiki iliyopita, kuamua kuvunja na kuziunda upya kamati hizo ambazo hata hivyo bado hazijapata wajumbe na kuchagua viongozi wake, Bunge halina tena usimamizi katika taasisi, mamlaka au wizara hali hiyo ikidumu hadi mkutano ujao wa 11 wa Bunge, Aprili, mwaka huu.

Taarifa za hivi karibuni ambazo gazeti hili limezipata zinadai, shaka hiyo inaweza kujionyesha kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, ambako kuna madai ya uongozi kuingilia mchakato wa utoaji zabuni ya ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini kutoka Uingereza.

Vyanzo vya habari kutoka London, Uingereza vinaeleza ya kuwa uongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara umeunda timu ya watu wanne waliokwenda huko kwa ajili ya kukutana na Kampuni ya W.T.M Utility ili baadaye kutoa taarifa kuhusiana na uamuzi wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuisimamisha katika shughuli yake ya awali ya ukaguzi wa magari.

TBS iliisimamisha kampuni hiyo ya ukaguzi wa magari Agosti, mwaka jana, kutokana na kudaiwa kutokuwa na uwezo wa kazi hiyo lakini ni kampuni hiyo hiyo ilirejeshwa tena katika mchuano wa zabuni katika dakika za mwisho kupitia kwa maagizo ya uongozi wa Wizara.

Pamoja na pingamizi la Bodi ya TBS, kampuni ya W.T.M Utility ilirejeshwa kuchuana na kampuni nyingine ambazo ni Serengeti Freight & Forwarders Ltd (London, Uingereza), Japan Auto Appraisal- JAAI (Minato-Ku, Japan), Wilna International (Tokyo, Japan), Auto Terminal Japan Ltd (Japan) na East Africa Automobile Services Co. Ltd (Watanzania wenye ofisi Japan).
Kampuni nyingine kwenye kinyang'anyiro hicho ni Jabal Kilimanjaro na Auto Elect. Mech (Sharjah, U.A.E) na Unit 92 Thames (Industrial Park, Princess Margaret Road, East Tilbury-Uingereza).

Vyanzo vya habari ndani ya TBS vinaeleza ya kwamba bado uongozi wa Wizara umeendelea kuwashinikiza baadhi ya viongozi wa TBS wairejeshe kampuni ya W.T.M Utility katika kazi ya awali ya ukaguzi, kinyume cha uamuzi wao wa awali wa kuisimamisha kampuni hiyo.

Juhudi za kumtafuta Waziri Kigoda, kwa njia tofauti ikiwamo kupitia simu yake ya mkononi na hata kumjulisha nia na aina ya maswali ya mwandishi wetu kuhusu kadhia hiyo ili ayatolee ufafanuzi, hazikuzaa matunda.

Pale alipotafutwa Kaimu Mkurugenzi wa TBS, Dominic Mwakangale, naye alijibu suala hilo kwa sasa lipo ngazi ya waziri na kwa hiyo hawezi kuzungumza chochote zaidi ya kumtaka mwandishi wetu kuwasiliana na waziri.

Kati ya mambo yanayohitaji ufafanuzi ni pamoja na madai yaliyopata kutolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma kwamba, ukaguzi wa magari umekuwa haufanywi na W.T.M Utility bali kinachofanyika ni kutoa vyeti vya uidhinishaji kwamba ukaguzi umefanyika.

Inadaiwa pia ya kuwa Watanzania wamekuwa wakitozwa paundi za Uingereza 140 kama gharama ya kukagua gari lakini namna ya uwasilishaji wa mapato yanayotokana na ukaguzi huo yamekuwa yakitiliwa shaka na baadhi ya wabunge, hususan, waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Taarifa nyingine iliyohitaji kupata ufafanuzi kutoka TBS au kwa Waziri kwa mujibu wa maswali ya mwandishi wetu ni kufahamu ukweli kuhusu usahihi katika utozaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wateja wao, utozaji ambao umehusishwa na tuhuma nyingine mbalimbali.

Kuhusu undani ya kadhia hiyo, chanzo chetu cha habari kimedokeza; "Baada ya Waziri kuivunja Bodi ya Wakurugenzi wale waliobaki TBS wamekwishapewa maagizo wairudishe kwenye kazi kampuni ya W.T.M na ili ionekane kama sheria imefuatwa, basi TBS wameamriwa na watume wakaguzi kwenda Uingereza na wakirudi tu W.T.M waanze kazi."

Lakini chanzo chetu kingine cha habari kutoka wizarani kinaeleza; "Kuna wakaguzi wanne wakiongozwa na mwanasheria wa TBS wamekwenda Uingereza.

"Lakini kuna taarifa huru zinadai wakaguzi hao hawana utaalamu wa kutosha kwa kazi hiyo, wako kwenye ofisi ndogo kwenye Jengo la Harbour House, Rainham UK. Itabidi waziri awe makini zaidi na hawa watu, mwenzake aliyemtangulia (Dk. Cyril Chami alipoteza uwaziri kwa sababu hiyo naye alimwondoa kazini Charles Ekelege (aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS) kwa hilo hilo, lakini leo anarudia waliyokosea wenzake. Ngoja tuone," kilieza chanzo chetu hicho cha habari kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

Chanzo kingine kutoka Uingereza kinaeleza kwamba kuna uchakachuaji mkubwa wa baadhi ya nyaraka zinazohusiana na ukaguzi wa magari jijini London kwa ajili ya kuletwa Tanzania.
Raia mwema
Pia tumeambiwa kwamba yule mzee wa muvi kali EKELEGE anarudishwa wiki hii kazini bila hata aibu
​
 
Kwa mtindo wa ccm huwezi kumpata kiongozi 'IMPARTIAL' isipokuwa wale walioonja mauti kama Magufuli na Mwakyembe! Maana kila kiongozi kwa mfumo wa serikali ya ccm ilivyo lazima ale, asipokula anafukuzwa kazi au anapewa demotion. Tuulize sisi maticha tulivyolazimika kuwalisha maafisaelimu, wahandisi wa wilaya, waratibu, kamati za shule ili wasaini check zetu za shughuli za mmem; chezea ccm wewe! Uliza leo shughuli za tender katika taasisi yeyote ya umma utaambiwa 10% ni lazima lkn haingii kwenye taasisi bali kwa bosi. Ukweli pesa inayopotea kwa njia za panya inaweza kuwa 40-50% ya fungu lote la maendeleo. Hii ni live experience sijasimuliwa: kwa maneno mengine ukiwa mtumishi halafu bosi kwenye taasisi za umma chini ya serikali yenu sikivu ya magamba lazima uwe fisadi vinginevyo utapoteza nafasi. Ndiyo maana dawa ni kuwang'oa kwa nguvu ya (umma) kura zetu vingine tukubali kuandaa taifa mufilisi kwa kizazi kijacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…