Wote tupo njiapanda: Tupande gari gani?

Wote tupo njiapanda: Tupande gari gani?

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
20,871
Reaction score
52,689
Humphrey Polepole ametuweka njia panda sote. Anayedhani hayuko njia panda, yawezekana tayari ni abiria wa gari la mbele. Tutafakari:

1. Kuna watu usipowasikiliza, ni hasara. Ukiwasikiliza ni hasara pia. Humphrey Polepole ni mmoja wao. Usipomsikiliza unakosa mengi. Ukimsikiliza, anakushawishi kutenguka katika basdhi ya misimamo yako. Chagua kwa hekima.

2. Nani ni bora? Shetani aletaye habari njema au malaika aletaye habari mbaya?
Tuangalie kwa makini vipa umbele vyetu:
-Mungu/Taifa/Chama
Vs
-Chama/Taifa/Mungu

Chagua kwa hekima.

3. Twaweza kumpuuza Humphrey Polepole. Je tutapuuza madhara ya kumpuuza? Chagua kwa busara kati ya kupuuza huku usiweze kupuuza madhara ya upuuzi wako.
Kama anasema uwongo anamdanganya nani? Mungu? Wananchi? Yeye mwenyewe?

4. Kama ni kweli tufanyeje? Kama ni uwongo tufanyeje? Kwa nini aliyoyasema yanafanana na imani na uzoefu wetu? Kwa nini wanaosema aliyoyasema ni uwongo hata wao wanajiona ni waongo?

5. Viapo vyetu viko njiapanda: kukiuka kiapo kwa kusema kweli au kutunza kiapo kwa kuficha ukweli? Tunapoapa twamwapia mwanadamu au Mungu? Tukishupaza shingo (Impunity), twamfanyia Polepole, Katiba, Katiba, wananchi?

6. Hatujui tumefikaje hapa. Tuna uwezo wa kujua tutokeje. Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reform?
Tupige kura kuamua kama tuchague au tusichague?

Unyenyekevu si udhaifu
TURUDI MEZANI
UKWELI ULIOCHELEWA NI BORA KULIKO UWONGO UNAOFARIJI.
HAKUNA TOBA ILIYOCHELEWA

MWISHO.

ASKOFU B. BAGONZA PhD
 
Bagonza:ilitaliwa kukaa kwenye kichwa cha habari
Unajua nilikuwa nasoma huku najiuliza ni nani huyu ameandika huu uzi mzito wenye sentensi za kupinduka pinduka na zinaleta maana.
Zimeandikwa kwa uweledi mkubwa sana wa kifasihi na kifalsafa.
 
Humphrey Polepole ametuweka njia panda sote. Anayedhani hayuko njia panda, yawezekana tayari ni abiria wa gari la mbele. Tutafakari:

1. Kuna watu usipowasikiliza, ni hasara. Ukiwasikiliza ni hasara pia. Humphrey Polepole ni mmoja wao. Usipomsikiliza unakosa mengi. Ukimsikiliza, anakushawishi kutenguka katika basdhi ya misimamo yako. Chagua kwa hekima.

2. Nani ni bora? Shetani aletaye habari njema au malaika aletaye habari mbaya?
Tuangalie kwa makini vipa umbele vyetu:
-Mungu/Taifa/Chama
Vs
-Chama/Taifa/Mungu

Chagua kwa hekima.

3. Twaweza kumpuuza Humphrey Polepole. Je tutapuuza madhara ya kumpuuza? Chagua kwa busara kati ya kupuuza huku usiweze kupuuza madhara ya upuuzi wako.
Kama anasema uwongo anamdanganya nani? Mungu? Wananchi? Yeye mwenyewe?

4. Kama ni kweli tufanyeje? Kama ni uwongo tufanyeje? Kwa nini aliyoyasema yanafanana na imani na uzoefu wetu? Kwa nini wanaosema aliyoyasema ni uwongo hata wao wanajiona ni waongo?

5. Viapo vyetu viko njiapanda: kukiuka kiapo kwa kusema kweli au kutunza kiapo kwa kuficha ukweli? Tunapoapa twamwapia mwanadamu au Mungu? Tukishupaza shingo (Impunity), twamfanyia Polepole, Katiba, Katiba, wananchi?

6. Hatujui tumefikaje hapa. Tuna uwezo wa kujua tutokeje. Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reform?
Tupige kura kuamua kama tuchague au tusichague?

Unyenyekevu si udhaifu
TURUDI MEZANI
UKWELI ULIOCHELEWA NI BORA KULIKO UWONGO UNAOFARIJI.
HAKUNA TOBA ILIYOCHELEWA

MWISHO.

ASKOFU B. BAGONZA PhD
Screenshot_20250824-113512~2.png
 
Bagonza anajaribu kuwa vuguvugu kwa craft ya maneno.
Atumie acid test kupima kauli za Polepole, mtandao na resources wanazo kama anataka kujiridhisha. Zaidi ya hapo ni kutaka a sound political correct.
 
Humphrey Polepole ametuweka njia panda sote. Anayedhani hayuko njia panda, yawezekana tayari ni abiria wa gari la mbele. Tutafakari:

1. Kuna watu usipowasikiliza, ni hasara. Ukiwasikiliza ni hasara pia. Humphrey Polepole ni mmoja wao. Usipomsikiliza unakosa mengi. Ukimsikiliza, anakushawishi kutenguka katika basdhi ya misimamo yako. Chagua kwa hekima.

2. Nani ni bora? Shetani aletaye habari njema au malaika aletaye habari mbaya?
Tuangalie kwa makini vipa umbele vyetu:
-Mungu/Taifa/Chama
Vs
-Chama/Taifa/Mungu

Chagua kwa hekima.

3. Twaweza kumpuuza Humphrey Polepole. Je tutapuuza madhara ya kumpuuza? Chagua kwa busara kati ya kupuuza huku usiweze kupuuza madhara ya upuuzi wako.
Kama anasema uwongo anamdanganya nani? Mungu? Wananchi? Yeye mwenyewe?

4. Kama ni kweli tufanyeje? Kama ni uwongo tufanyeje? Kwa nini aliyoyasema yanafanana na imani na uzoefu wetu? Kwa nini wanaosema aliyoyasema ni uwongo hata wao wanajiona ni waongo?

5. Viapo vyetu viko njiapanda: kukiuka kiapo kwa kusema kweli au kutunza kiapo kwa kuficha ukweli? Tunapoapa twamwapia mwanadamu au Mungu? Tukishupaza shingo (Impunity), twamfanyia Polepole, Katiba, Katiba, wananchi?

6. Hatujui tumefikaje hapa. Tuna uwezo wa kujua tutokeje. Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reform?
Tupige kura kuamua kama tuchague au tusichague?

Unyenyekevu si udhaifu
TURUDI MEZANI
UKWELI ULIOCHELEWA NI BORA KULIKO UWONGO UNAOFARIJI.
HAKUNA TOBA ILIYOCHELEWA

MWISHO.

ASKOFU B. BAGONZA PhD
Sio njia panda tuu mkuu,katuacha roundabout hutuna mwelekeo,tunazunguka tuu!
 
Back
Top Bottom