Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
1>laana itaposhuka,nani ataebakia.
Tutaja kumbuka shuka,saa nyumba yaungua.
Wao wameshazinduka,wapi pakukimbilia.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
2>ukishindwa we ridhika,tena pembeni tulia.
Mauti yasijefika,taifa kutuchomea.
Eti haki yaitaka,tumbo waliongelea.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
3>bila kuruka mipaka,kura yako kuchochea
jivu moto litawaka,kuchoma waso hatia.
Taifa tumelishika,utu tusije achia.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
4>kosa tukija lipika,mwiko tutaujutia.
Pishi lilolanika,wanao kuwalishia.
Washiba wataabika,kaa kuwapakulia.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
5>jivu litatawanyika,kichwani litaingia.
Kwa mola tutaepuka,njema dua kuombea.
Upendo kutuzunguka,daima milele pia.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
Shairi=WOSIA WA MWISHO.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 Au 0655519736.
eeee mungu mwenyezi mwenye kurehemu,ujalie uchaguzi wa Tanzania uwe wa amani na utulivu.
Tutaja kumbuka shuka,saa nyumba yaungua.
Wao wameshazinduka,wapi pakukimbilia.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
2>ukishindwa we ridhika,tena pembeni tulia.
Mauti yasijefika,taifa kutuchomea.
Eti haki yaitaka,tumbo waliongelea.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
3>bila kuruka mipaka,kura yako kuchochea
jivu moto litawaka,kuchoma waso hatia.
Taifa tumelishika,utu tusije achia.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
4>kosa tukija lipika,mwiko tutaujutia.
Pishi lilolanika,wanao kuwalishia.
Washiba wataabika,kaa kuwapakulia.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
5>jivu litatawanyika,kichwani litaingia.
Kwa mola tutaepuka,njema dua kuombea.
Upendo kutuzunguka,daima milele pia.
Wangu wosia wa mwisho,kura siyo uadui.
Shairi=WOSIA WA MWISHO.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 Au 0655519736.
eeee mungu mwenyezi mwenye kurehemu,ujalie uchaguzi wa Tanzania uwe wa amani na utulivu.