World Poverty Clock: Watanzania Milioni 21.2 - 37.1% wanaishi katika hali ya umaskini wa KUTUPWA

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Wana JF hii si ripoti nzuri sana. INAHUZUNISHA, INAKASIRISHA na INASIKITISHA.
Katika ripoti yake iliyotolewa na WORLD POVERTY CLOCK iliyoko Vienna Austria MWEZI HUU ikishirikiana na mpango wa UN's Sustainable Development Goals (SDGs) iliyolenga nchi mbali mbali na HASA za Afrika na Afrika Mashariki,

Tanzania inasemekana Tanzania ina Maskini millioni21.1 ambayo ni ASILIMIA 37.1% ya population nzima ya Watanzania ambao ni maskini SANA.
Hili ni lazima WANASIASA wa PANDE zote waliangalie hili kwa MAKINI bila kujali vyama vyao. Na WALIJADIRI bila kuegemea upande wa kisiasa. Ni HUZUNI sana kusikia jambo kama hili.


Pamoja na ripoti hiyo ya kusikitisha,
Hata hivyo kuna HABARI NJEMA kuwa katika mtazamo wa World Poverty Clock,

Tanzania sasa:
IMEAANZA KUUONDOA UMASKINI katika kipimo/RATE SPEED ya idadi ya WATU 66 kwa kila SAA moja TOFAUTI na ZAMANI ilivyokuwa.

Yaani ina maana kwa kila saa moja Watanzania 66 WANAOKOLEWA toka UMASKINI huo.

Hi ni kusema Watu 66 kwa sasa ni idadi kubwa japo juhudi ziongezwe ili hatimaye tutoke huko.
Katika nchi za Afrika Mashariki Tanzania iko zaidi ya JUU zaidi ya jirani zetu wa Kaskazini ambao yao ni watu 30 kwa saa.

Report hiyo inasema GDP za nchi mbali mbali kwa muda mrefu zimeonekana kwenye makaratasi tu lakini HAZIWAFIKII wananchi mashinani.

Nchi zilizoonekana kuwa na UMASKINI MDOGO sana AFRIKA ni:
1.MAURITIUS ni 0.2% PEKEE ya watu maskini katika population yake. Ikifuatiwa na
2.MISRI: 0.4% na
3.MOROCCO ni 0.4%
USHAURI wangu kwa wanasiasa ACROSS the POLITICAL DIVIDE/ Bila KUJALI CHAMA.

Waweke PEMBENI mambo ya MASIASA SIASA yasiyo na misingi ili TUWATOE to ka umaskini HAWA Watanzania million 21.1 ambao ni asilimia 37.1% ya IDADI ya Watanzania wote WANAOTESEKA kwa UMASKINI wa kutupwa.

Badala yake Wanasisa WAJADILI MAENDELEO na ni namna gani UCHUMI wetu utakuwa BORA na kuwezesha UTAJIRI wake UTIRIRIKE mpaka VIJIJINI

Nafikiri mwanasiasa kama huyo HATASAHAULIKA milele na Mungu na Watanzania wote WALIOTESEKA na umaskini kama huu kwa MIAKA zaidi ya 50 tangu tupate UHURU wetu.
Mungu ibariki Tanzania
CHANZO: Link ni kutoka Vienna Austria
www.world poverty clock
 
Tunatakiwa tuwasaidie watu, ndugu wenzetu. Serikali inaweza kuwapa pesa ndogo za kuishi Kama Nchi nyingine nyingi zinavyofanya kuwasaidia wananchi wao.
 
BONGOLALA,
NBS watakataa utafiti wa hawa jamaa, tunasubiri taarifa ya Ofisi ya Taifa Ya Takwimu (NBS) baada ya ile ya leo kuhusu GeoPoll. Sasa itakuwa zamu za takwimu za World Poverty Clock kukataliwa
World Poverty Clock
The World Poverty Clock provides real- time estimates until 2030 for almost every country in the world. It monitors progress against Ending Extreme Poverty, which is the UN's First Sustainable Development Goal (SDG1) . The escape rate calculates the current rate of reduction in poverty in the world
Source: World Poverty Clock
 
Sizonje ni kivyake vyake hataki wanasiasa wengine.and you know it.
Hataki SIASA SIASA anachotaka ni KUWATUMIKIA wananchi. Na kuwatumikia si kukaa na KUPINGA, KUTUKANA, KUKEJELI na hsta kuingiza siasa hata katika mambo ya kitaalamu.

Ndo maana watu 66 kwa saa Huyo unayemwita hilo jina anajaribu kuwatoa watu katika huo mzigo wa umaskini
 
Umasikini mbaya kuliko wote ni ule wa fikra.
Tunatakiwa kuwafungua wananchi wote kutoka kwenye nira za utegemezi kwa wafadhili na hata kwa viongozi.
Wananchi ni lazima wajue kuwa matendo yao ndiyo yatakayowakomboa, na kwamba wengine wote wakiwemo viongozi wafadhili wanaonesha njia tu, na wanategemea nguvu na jasho la wananchi katika kufanikisha shughuli za kimaendeleo.
 
Du! Kwa hiyo ata kesho watu 66 watauaga umaskini ee mola naomba niwemo.
Ndani ya Serikali ya Magufuli Huenda ukawa mmoja wa watu watakaouacha umaskini.
Hii ni kutokana na ubunifu wa AJIRA, KUJIAJIRI, MIKOPO, KUWEZESHWA nk. Kila kitu kinawezekana.
 
Tunatakiwa tuwasaidie watu, ndugu wenzetu. Serikali inaweza kuwapa pesa ndogo za kuishi Kama Nchi nyingine nyingi zinavyofanya kuwasaidia wananchi wao.
Kuwapa pesa si suluhisho.
Bali ni
KUWAFUNDISHA mbinu za biashara,
Ufundi,
Ufugaji wa SAMAKI,
KUKU,
KILIMO BORA UFUGAJI WA NYUKI nk then WAPE MKOPO ndo hapo tutazidi KUWATOA katika umaskini huo?
 
Back
Top Bottom