Working Capital.

Working Capital.

Arch Barrel

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2024
Posts
533
Reaction score
1,225
Habari za jioni wanajukwaa au JF Member wote.

Naomba niende kwenye lengo la uzi huu moja kwa moja.

Wakuu mimi ni mjasiriamali mdogo ambae pamoja na wenzangu wawili tulifanikiwa kufungua kampuni yetu ya ujenzi. Toka tumefungua kampuni ina miaka minne sasa, na mpaka sasa tumefanikiwa kufanya na kukamilisha miradi mitatu chini ya taasisi za serikali.

Kwa sasa tuna project mbili ambazo zinapaswa kuendelea lakn tumekwama kwa sababu ya changamoto ya kifedha. Changamoto kubwa ni kuchelewa kwa malipo kutoka kwenye Project zilizotangulia.

Humu ndani najua tunatofautiana uwezo wa kifedha, wapo watu wengi humu huwekeza pesa zao wakisubiri gawio mwisho wa mwaka au baada hata ya miaka miwili. Kwa aina ya project tulizonazo tunaweza kuchukua kati ya miezi 2 hadi 3 kukamilisha mradi. Baada ya hapo tujipe tena miezi mitatu mingine kusubiri malipo baada ya hapo hela yako itarejea.
Kiasi kinachohitajika ni kati ya (80 - 100)M.
Kuhusu usalama wa pesa yako tutafungua akaunt maalumu ambayo wewe na mmoja wa director mtakuwa signatory akaunt hiyo itakuwa ni kwa ajili ya mradi huo tu baada ya hapo itafungwa.
Utashirikishwa katika mchakato mzima wa uendeshaji mpaka kukamilika.

Kuna vitu vingi sijaviweka wazi kwa sababu za kiusalama. Naomba alieko tayari kutupiga tafu kwa riba au agreement tutakayokubaliana aje DM.

Please naomba ushauri we kwenda taasisi za kifedha usiuweke hapa na kuna wale wanaosema unafunguaje kampuni huna mtaji wa kutosha hao pia naomba wapite kushoto. Naomba alieko tayari kutushika mkono aje PM au aulize swali lolote nyeti PM nitamjibu na kutoa majibu sahihi.

Karibuni sana waungwana tuna uhitaji sana. Ahsanten
 
Back
Top Bottom