Haijaondolewa. Wanaoipigia kelele ni wanaharakati wa haki za binadamu. sababu: wanataka hukumu yoyote ipelekee mtu kujutia kosa lake na kujifunza - wakidai akiuawa anajifunza nini? .. Upo?
Haki za binadamu ni baina ya wote aliyedhulumiwa(aliyeuliwa) na dhalimu (muuaji) na hakimu ni Mwenyezi Mungu aliyeumba roho.
Kuuwa kwa mkausudi kunajulikana na kuuwa kwa ajali au bila ya kukusudia kunajulikana
Nafasi ya Mafunzo/mafundisho kuhusiana na makosa yoyote yale, yawe ya jinai au madai ni kukinga makosa hayo kutokea. Na hili ni jukumu la wazazi, jamii na mazingira (ikiwemo ulimwengu). Inachotokea baada ya kosa kutendeka ni haki- (balanced, just and lawful retribution of the crime), sio mafundisho ya awali. Na kuuwa pasipo na sababu halali (mfano: retribution for murder,au kuzini au ku-turn against the state) basi haki yake ni adhabu ya kifo.
Hatahivyo, hata katika sheria ambapo adhabu ya kifo imewekwa, mfano katika uislamu, bado nafasi ya kusameheana na kulipana fidia ipo, na hii inakuja kutokana kutambua haki za kibinadamu ambapo familia ya aliyedhulumiwa (aliyeuliwa)ikishirikiana na dola huwa na jukumu kubwa katika jamii katika kutoa hayo mafunzo unayoyasema. Inapobidi, kosa hupimwa, majuto ya kosa hupewa uzito unaostahili na kusameheana hutokea. Vinginevyo ni adhabu ya kifo inayofanywa katika sehemu ya wazi ni:
1. Haki iliyo sawa kwa muuaji yenyewe, kwa familia ya marehemu na jamii husika, hata ulimwengu mzima.
2. Mafundisho tosha kwa jamii na ni deterrent hasa kwa wale potential murderers waliobakia, maana adhabu ile hutikisa mpaka nyoyo zao. Sio binadamu wala shetani asiyetikiswa na adhabu ya kifo, yaani maneno mawili: adhabu + kifo
Hao wanaojiita ma-champion wa haki za binadamu ni wanafiki, mfano ni huu huyu aliyepenyeza hii mada: kaanza kwa kupiga kelele hivi "Adhabu ya kifo lazima iwepo" kwanini?
- Huyu ni mmoja ya hao wanaomini hizo haki za binadamu kwa wengine na kuzikataa kwa wengine.
- Huyu ni yule ambae kalishwa kasumba mpaka kabadilishwa imani kwanza (yaani kafanywa aamini kwamba adhabu ya kifo bora isiwepo kwa sababu mbali mbali za kijinga zinazofichwafichwa ndani ya kwapa za haki za binadamu); na pili kabadilishwa ufahamu wake (consciously amefanywa afahamu kwamba hii adhabu haipo tena). Lakini kasahau huo ufahamu wake kapenyezewa tu ndani ya akili yake ili wauwaji wakubwa wa-get away with it huku akiwatizama tuuu bila ya kufikiria kwamba nao wanastahili adhabu ya kifo vile vile.
- Ghafla tu anakurupuka "... lazima iwepo" wakati imekuwepo muda wote, yeye kaikuta, ipo na ataiacha hapa hapa. Kakurupuka hivi kwasababu ya kasumba inayofanywa na walewale wauwaji wakubwa anaowafumbia macho. Kwasababu leo mnyonge katokea kufanya crime kama ile au pengine ndogo ya ile (kwasababu kwa malingano, hii haifanani na yule mjerumani aliyefanya kama hivi, cha kusikitisha zaidi yeye alimfanyia i. mwanamke (mama wa watoto wawili), ii. aliyekuwa mja mzito kwa mtoto wa tatu, iii. eneo la tukio ndio ajabu zaidi:- ni ndani ya mahakama wakati yule mama anatoa ushahidi wa assault aliyomfanyia kabla ya hapo, iv. sababu yenyewe ni kuwa yule dada kavaa hijabu-yaani ni muislamu). Hii hata kama imepita machoni mwake au masikioni mwake, katika mpito uliochakachuliwa na vyombo vya habari vya hawa wakubwa, basi yeye hawezi hata ku-analyse, kushituka na hakukurupuka namna hii, imepita kama haikutokea, kwasababu ameshakuwa de-sensitized dhidi ya jamii fulani.
Ndio mimi nikamuuliza kuwa imeondoka lini? Ninavyofahamu mimi ni kuwa nchi zote ulimwenguni zinazo adhabu ya kifo, isipokuwa zilizoondosha zinajulikana, hizi zilikuwa nayo hii adhabu, na ndizo ambazo zinahitaji ushauri wa jamiiforums ili kuzirudisha. Kama watazitumia ipasavyo, basi kama huyu jamaa anastahili hiyo adhabu, wengine nao ni lazima wapate vile vile. Na haya mauwaji ya namna hii nani anae-justify? na nani kaanza, yeye au hao wauwaji wakubwa?.