Women...........!

Kama mwanaume anaona ni lazima mkewe apike na kufua amnunulie hivi vitu, it is easy to multitask kama kunavitendea kazi. Kuna washing machine, rice cooker, kitchen aid, vacuum cleaner (kwa wanaomudu - mnamudu ndio maana mnaweza kusustain vismall house). Kama ni thorough cleaning kuna makampuni kibao unaweza kodi yakakufanyia usafi.

Mpende, mhurumie mkeo. Muwezeshe ataweza.
 
Uko sawa sana. Ni ukweli usiofichika kwamba wanaume hatutimizi majuku yetu ya kuitwa wanaume. Kina mama mnavuka mikapa kutimiza wajibu wa wanaume kwenu. Kuna dini moja inasema wazi kabisa kwamba "Mwanaume anawajibu wa kumtunza mkewe kuanzia chakula, mavazi, malazi, matibabu na mengine yotu yanayomuhusu mwanamke ni jukumu la mume"ikitokea kuwa mwanamke anafanyakazi hiyo basi ni added advantege na wala mwanamke hawajibiki kulipa bili wa kumtunza mume na watoto kimatumizi. Wanaume wote tungelielewa hili, heshima tunayodai kwa wake zenu tungeipata bila kuiomba na swala la kina mama kudai haki sawa lisingekuwepo.

Tuliona tumetimiza haki zetu zote kwenu tena bado mnataka haki zenu kwetu tuzifanye sisi ndio maana tunataka haki sawa, tunapika, tunafua, malezi ya watoto, sasa hivi tunalipa karo za shule,kodi za nyumba ,tunawanunulia magari,
 
hayo yote uliyoyasema
ndio ninayotaka anifanyie kwasababu hayo ndo majukumu yake,kwani wakati
anakubali kuolewa hakujua kuwa atatakiwa kufanya mambo hayo?

Na wewe unafanya nini? Maana siku hizi ada za watoto,bili za maji na umeme na kodi za meza zote tunachangia, kama nyinyi mnasaidiwa kwa nini nanyi msisaidie wenzenu?
 
jamani wanaume ni mafirst born ukiweza kumlea mumeo vzr watoto wenu hawatakusumbua...!haki sawa iwepo ila kwenye kazi lakini mambo mengine wanayodai ni haki yao kufanyiwa labda akiamua mwenyewe kumsaidia mkewe!!mke ukiweka ushindani..nyumba ndogo atafanya!!
 
Ndo maana talaka zinaongezeka, kumbe mnaoa ,mpate watumishi wa ndani, na si mke


kwani wakati nakuoa nilikwambia nakuoa kwa ajili ya chakula cha usiku tuu,hujui kuwa wengine wanaoa ili wafuliwe,wapikiwe sasa ukianza kumwambia ayafanye hayo utakuwa unamkosea.
 
Mhhhh! leo nimegundua kitu..kumbe Remmy ni mdada, siku zote nilidhani ni njemba :):)

Wakati Adamu na Hawa wanatimuliwa Edeni Mungu alimwambia Eva utazaa kwa Uchungu na Adamu utakula kwa jasho. Kwa maana hii ke kazi yake ni kuzaa tu na me kufanya kazi zote. Mmepotosha maana ya Mungu na kuleta ubinafsi wenu, maudhi yenu, masimango yenu ndo yametufanya tujitetee.
 
Wanaume wengine ndani ya ndoa wanajidekeza kupita kiasi!!! hata kusuuza kijiko tu kunaweza kuzaa varangati kubwa ndani ya nyumba. Mama fulani mwanao amekojoa njoo umbadilishe nepi, mama fulani hapa sitting room kuna uchafu njoo upitishe fagio, mama fulani lile shati langu la blue halijapigwa pasi nipigie pasi maana nataka kulivaa leo.

Utadhani lolote kati ya hayo hapo juu akiyafanya basi uanaume wake utapungua kwa asilimia kubwa sana na hivyo kudharaulika na mkewe na labda na jumuiya.

Ndo maana talaka zinaongezeka, kumbe mnaoa ,mpate watumishi wa ndani, na si mke
 
Back
Top Bottom