Aleyo obebe nchilochilo gete, ango?Wabeja Namhala.
Mjadala na wewe uishe
🤣🤣🤣🤣 watu wana maumivuKiwango cha sukari kwenye hii post kipo juu mnoo
Nini shida mkuu?Mpuuzi wa mwisho
Kuna sehemu nimekuingilia mkuu?We jamaa unataka uingie kwenye ligi pia?
😆😆😆😂🤣PSL god 🤮"Women don't love men."
"They love benefits: your looks, your body, your money."
"The moment you stop serving their needs, they stop calling it love."
"Women don't fall in love, they consume."
"They want money and someone to clean up their emotional mess."
"And the moment you stop feeding that, they call you difficult."
"You wanna know how much a woman really cares, check her effort, not her mouth."
"Because words are free."
"Effort costs something."
"And most women are only generous with words."
Agree???
😂😂 noma🤣🤣🤣🤣 watu wana maumivu
Mimi sio wa masaki ila ndio hivyo rule no 1 🧠 mengine tuta discuss pamojaHaya sasa Manyanza umesikia watoto wa Masaki hawa?
Hapo hapoo.Mimi sio wa masaki ila ndio hivyo rule no 1 🧠 mengine tuta discuss pamoja
Kuishi na mjinga kisa ana hela ni shida sana
Nachagua mwanaume mwenye akili inayoperform vizuri kuliko mwenye pesa kwa sababu zifuatazoHapo hapoo.
Mimi ndiyo ninachokupendea hichoo 😂😂😂
Sasa hapo unikute mjanja halafu hela ninayo hapoo, hapoo...
Umemaliza kila kitu.Nachagua mwanaume mwenye akili inayoperform vizuri kuliko mwenye pesa kwa sababu zifuatazo
👇
Mwanaume mwenye akili, automatically, anajiheshimu na kuheshimu wengine, akiwemo mimi mwenyewe
Mwanaume mwenye akili hata kama hana pesa leo, kupitia akili yake anatembea na wazo na maono
Kwa sababu anaitumia vizuri akili yake, muda wowote mambo yanaweza kukaa sawa
Navutiwa na mwanaume mwenye akili kubwa kwa sababu mimi binafsi huwa nahitaji mtu mwenye akili kubwa ya kunicontrol
I told you qkiwa mjinga, kwa nilivyo, nitamdharau vibaya hata kama ana hela
Cha muhimu na cha mwisho, mwanaume mwenye akili nyingi na anayeitumia vizuri si rahisi kufilisika, kwa sababu anatumia reasoning kufanya maamuzi
Hivyo, uwezekano wa kua na pesa mali na kuendelea kujenga na kuhifadhi mali zake ni mkubwa na hiyo ni faida kwangu mimi na yeye
Mwanaume mjinga na mpumbavu, hata akiwa na hela, kuwa naye ni risk.
Wote tunajua watu wajinga na wapumbavu walivyo mara nyingi hawana staha wala heshima kwa wengine
Pia, uwezekano wa kufilisika unaweza kuwa mkubwa kutokana na maamuzi yao ya kipumbavu
Kwako Kiranga
Relax bwa'mdogo.Huyo anashida mahala huenda ndo yule Mr VAR kwa mavazi tofauti
Haya dogoRelax bwa'mdogo.
Mbona sijakutaja wewe ni shobo zako tu.
Ipo hivi, wanaume ninaowaona kwenye jamii yetu hata hapa jukwaani ni watu waliobeba negative attitude kuhusu wanawakeUmemaliza kila kitu.
Halafu kizuri zaidi, mimi nimeandika sana hapa.
Lakini kulikuwa na swali moja la muhimu halijajibiwa.
Lile la "Kwani wanawake wenyewe wa Tanzania wanasemaje?"
Kwa upande niliokuwa nautetea nilipata tabu kupata mifano ya kwetu ya wanawake wanaojitambua, ambao nilijua mpo hata japa JF.
Sasa wewe umekuja kufanya kazi nzuri sana ya kusema kwa niaba ya wengi.
Nashangaa sana kuona kuna watu bado wana tatizo la kuelewa jambo dogo sana, kwamba wanawake wapo wa aina nyingi tofauti, kufuatana na historia, malezi, socio-economic factors, education, experience, etc.
Kwa hiyo kiwalindika kundi moja ni Hasty Generalization Logical Fallacy, pamoja na Composition Gallacy
Nasikitika sana mtu anapokuwa na kasumba za kizamani za kuandika kijumlajumla "wanawake...." or for that matter "wanaume..." while that is oversimplification and generalization.
Zaidi, naona kama hii habari nzima ni wanaume kuwa gaslight wanawake tu.
Kwa sababu, hata wanaume siku hizi wapo wengi Mario wanaopenda mishangazi iwatunze.
Kuna wanaume wengi wana objectify wanawake, wanataka wanawake wenye matako makubwa na maziwa makubwa. Hawa pia tunaweza kusema hawawapendi wanawake kama watu, wanapenda matako yao na ngono etc.
Lakini mwanamme akifanya hivyo inaonekana kawaida, mwanamke ni kesi.
Zaidi, suala la mwanamke anapenda nini ni suala lake yeye, maamuzi yake binafsi. Apende hela, apende six pack, apende mbeba vyuma, apende kibabu, ni haki yake. Kivyake.
Ilimradi hajakulazimisha kitu wakati wewe hutaki, tatizo liko wapi?
I mean, why is it even a question mwanamke fulani akipenda mwanamme mwenye hela au mwenye six pack? Si uchaguzi wake mwenyewe?
Tatizo liko wapi? Kama mwanamme hataki mapenzi ya pesa si atafute mwanamke wake anayeendana naye tu, dunia yote hii wanawake wote hawa, badala ya kutafuta mtu mnayeendana utulie naye, kwa nini unaenda kushambulia mtu ambaye hamuendani?
Do I detect some level of insecurity somewhere?
Mbona mimi sipendi wanawake wajinga wanaopenda pesa tu, lakini sijaona haja ya kuwashambulia, sijui historia zao na poverty anxieties zao na trauma zao zilizowafanya wawe hivyo, who am I to judge them?
Sasa kwa nini wanaune wengine wanaona lazima dunia iende kama wanavyotaka wao tu hawawezi kuwapa wengine uhuru wa kuishi wanavyotaka?
That reeks of insecurity to me.
Umeandika vizuri sana.Ipo hivi, wanaume ninaowaona kwenye jamii yetu hata hapa jukwaani ni watu waliobeba negative attitude kuhusu wanawake
Ikitokea mwanaume akaanzisha uzi, let's say mke wake anamjali na anajivunia kupendwa utaona zitakuja negative comments
Watamshambulia na kumwambia kwamba hawajui wanawake vizuri
Yaani kwa maana nyingine, haruhusiwi kufurahia hizo moments nzuri na mke wake kwa sababu tu wengine wana mtazamo hasi kuhusu wanawake
Baadhi ya wanaume wa jamii yetu wanamchukulia mwanamke kama tishio kama mtu mwenye complications nyingi
Lakini ukweli ni kwamba mleta mada anaweza kuwa yupo sahihi kutokana na experience yake, ila kukusanya wanawake wote na kuwaweka kwenye kapu moja ni makosa
Watu tumetofautiana kuanzia maumbile muonekano na hata hobbies zetu ni tofauti
Kuna mwanamke anapenda pesa kuliko chochote
Kwa mtazamo wake, hilo ni sawa, lakini haimaanishi kwamba wanawake wote ni gold diggers
Na hata mimi ninayesema hivi haina maana kwamba sipendi pesa
Napenda pesa, lakini napendelea zaidi pesa zangu kwa sababu ego yangu hairuhusu niwe kwenye uhusiano wa kumsujudia mtu kwa sababu tu ana pesa
So, kama mpenzi wangu akinipa kitu, anipe tu na nitapokea
Ila pesa si kitu cha kwanza ninachozingatia kwa mwanaume ninayemtaka
Nina vigezo vyangu ambavyo mwanaume akikosa, hata kama ana pesa haitoshi kuwa sababu ya mimi kuwa naye
Halafu anaweza akawa yupo Mshikaji hana hela wala nini, lakini nikamkubali kwa sababu ana vitu vingine ambavyo vinanivutia na vinakidhi vigezo vyangu.
Mwisho wa siku, wanawake hatufanani. Kile ambacho mwanamke mmoja anakiona cha muhimu kinaweza kisiwe na uzito wowote kwa mwingine
Hivyo, tusitumie experience zetu binafsi kuwahukumu wanawake wote
My take : Huu ni mtazamo wangu binafsi sio msimamo wa wanawake wote
Kwako Kiranga
Kuna umri mtu ukifika, huitaji tena kutumia uzoefu wa pale mtaani ulipokulia, kwa sababu mtaani kwenu kuna muingiliano wa nyie kwa nyie, hakuna jipya yaani kanzu jipya sheikh yule yuleUmeandika vizuri sana.
Na mimi niliona hii Hasty Generalization Fallacy na Composition Fallacy ililetwa maalum kuwa gaslight wanawake.
Mimi sina tatizo kuwasema wanawake wa aina fulani, hapa mara nyingi tunakuwa brutally honest tu, so this is not some chivalrous defense of women. Ila nina tatizo kuwaweka wanawake wote kwenye kapu moja kijumlajumla kijingajinga tu.
Kuna wanaume wanakuwa kama wanashindana na wanawake, which I find absurd and bizarre. Mwanamme unashindanaje na mwanamke? Ni kama wanataka kuwa put down wanawake ili wao wawe juu, mambo ya kizamani sana.
Watu, niseme tu baadhi ya wanaume, wana some deep seated wounds and insecurities ambazo wengine hata sijui kama wanajua wanazo. Some of that "you need therapy" shit.
Yani ile samaki anaogelea ndani ya maji tangu anazaliwa, kashayazoea hayo maji mpaka hajui haya ni maji, ukimwambia wewe ni samaki, na haya ni maji, na upo duniani, na kuna ngamia yupo jangwani huko jangwani hakuna maji, yule samaki anakuangaliaaa, hakuelewi, anasema maji gani? Hakuna maji hapa. Kashayazoea yale maji mpaka hayajui.
Yani unajibizana na mtu unaona kabisa huyu anaelewa lakini haelewi, anakuwa na kitu wanasaikolojia wanakiita cognitive dissonance, yani ni kama achukue muda fulani kutafakari mambo ya wazi kabisa ndiyo ayakubali. Yani hapo hapo anakubali kwamba amefanya generalization vibaya, halafu hawezi kuacha, hapo hapo anarudia 😂😂😂
Unamwambia hayo mambo yote unayoona matatizo ya wanawake kwa kiasi kikubwa ni matatizo ya utamaduni, elimu, uchumi, exposure, si matatizo ya mwanamke per se, kwa sababu mbona sehemu nyingine wanawake hawana matatizo hayo, mbona hata wewe ShesRise_1 Mtanzania umejieleza vizuri tu, na maelezo yako yapo consistent na tabia zako za hapa JF so sio kitu ulichorusha leo tu.
Ila unajua tena mazungumzo ya JF. Unaweza kuona unajibizana na mtu kwa hoja na mantiki, kumbe mwenzako anapigania "team ya kiumeni", by any means necessary, hata haangalii hoja.