GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,016
John F. Kennedy aliwahi kuseama kua. ” A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is fraid of its people”. Yaani “Taifa linaloogopa kuwaacha watu wake kuuhuoji ukweli na uwongo katika hali ya uwazi ni taifa linalowaogopa watu wake”.
Kwa mtazamo wangu Viongozi wetu wengi wa Africa ni waoga wa kua tayari kuwapa uhuru wanaowaongoza kuhoji mafanikio na matatizo ya viongozi hao kutokana na matatizo wanayoyasababisha viongozi hao kua mengi zaidi ya mafanikio. Hapa ndipo msingi wa viongozi hao kutumia silaha na vyombo vya dola kuwazima wanaowaongoza unapoanzia, utaona wananchi wakinyimwa uhuru wao wa kujieleza kwa mitutu, vyombo vya habari kufungiwa n.k
Buddha aliwahi kusema ” Even death is not to be feared by one who has lived wisely”. Yaani mtu alieishi kwa busara (kufanya mema)hata kifo hakiogopi. Msingi wa kuepukana na hofu ni kutenda mema na msingi huu ukikosekana kinachojitokeza ni hofu ambayo hupelekea viongozi kutumia nguvu nyingi kujihami na hofu zao hizo.
Si kweli kua kuna viongozi wasiotaka mafanikio (mabadiliko) bali wako viongozi wanaogopa mafanikio lakini viongozi wengi huogopa zaidi madhambi yao waliyoyafanya wakiwa madarakani na hata pale unapoona kiongozi anaogopa mafanikio kama ilivyo kwa CCM ambao wao wana hofu ya mambo yote mawili (madhambi waliyoyafanya na mafanikio) kiongozi huyo anaweza kulitia taifa katika huzuni kama alivosema Plato. ” We can easily forgive a child who is afraid of the dark, but the real tragedy of life is when men are afraid of the light”. Yaani “Tunaweza kumsamehe mtoto anaeuogopa usiku (kiza) lakini huzuni ya maisha ni pale watu wanapouogopa mchana (mwangaza)”.
Usiku hapa unaweza kutafsiriwa kama ni dhambi ambazo si jambo la kushangaza kuona mtu akiogopa dhambi zake lakini mchana ni mafanikio ambayo itashangaza pale kiongozi anapoamua kujieka madarakani kwa mitutu akihofu kumuachia kiongozi mwengine madaraka kwa dhana tu ya kua akimuachia atafanya mambo mazuri ambayo yeye hakuwahi kuyafanya katika uongozi wake.
Pia dhambi kubwa wanayoifanya viongozi wetu wa Africa ni kuwarithisha wanaowaongoza woga huu kwani ni vyema kama woga huu ungebakia kwao wao tu viongozi kwasababu kuwarithisha wanaowaongoza woga kwa mbinu na njama za mabavu ni kutengeneza taifa la watu waoga ambao pia wanaweza kushindwa kusimamia maslahi ya taifa lao hata pale viongozi hao watakapokua wameondoka madarakani (wamemaliza muda wao wa uongozi).
Mwanafalsafa mmoja anasema “The only thing to fear is fear itself”. Yaani Kitu pekee cha kuogopa ni woga wenyewe. Woga tunapaswa kuogopa kushinda kitu chochote kile lakini inashangaza viongozi wetu wanapotumia mda mwingi kutafakari namna ya kuwatengezea mazingira ya kuwatia hofu wanaowaongoza.
Bila ya shaka viongozi wetu wa Africa (Zanzibar) wanaamini katika maneno ya Niccole Machiavelli ambayo kwa mtazamo wangu sioni kua ni sahihi pale aliposema kua ” It is better to be feared than loved”. Yaani “Ni bora kuogopwa kuliko kupendwa”. Hapa ndipo walipopashika viongozi wa CCM na ndio maana leo mitutu na madhila si tu inatumika kulinda dhambi za viongozi hao bali pia inatumika kama ni nguzo muhimu ya kuwajenga watu hofu ili viongozi hao wapate kufanya wanachojiskia.
Mwisho nimalizie kwa kusema kua kipimo cha kiongozi bora ni nguvu, ushawishi, nia, dhamira na uwezo wake wa kutatua matatizo (migogoro) na sio kuanzisha migogoro na kuhofu dhambi za kuanzisha migogoro hiyo na kuamua kuzilinda dhambi hizo kwa mitutu na kila hila. Bruan Tracey anasema. ” Leaders think and talk about the solutions. Followers think and talk about problems”. Yaani “Viongozi hufikiria na kuzungumzia suluhu. Wananchi hufkiria na kuzungumzia matatizo”. Hivyo ni jukumu la viongozi kutafta suluhu pale migogoro inapojitokeza na sio wananchi hasa pale wanapowataka wananchi wafanye kazi pamoja na kushirikiana wakati wao viongozi wenyewe hawajawahi hata kutafakari na hawana hata nusu ya chembe ya nia ya kutafta suluhu katika nyoyo zao. Viongozi wa namna hii hawawezi kua viongozi waadilifu.
Written by
Abdalla Dadi.