Wodi ya wagonjwa mahututi Mwaisela yazinduliwa Muhimbili

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,796
Serikali imesema kwa sasa itakuwa ikihudumia wagonjwa wote ndani ya nchi ikiwemo wale wagonjwa Mahututi ambao awali walikuwa wakipelekwa nje ya nchi. Hii ni baada ya kuendelea kuimarisha huduma hizo pamoja na kuwa na wataalam wa kutosha ambaio watapatiwa mafunzo zaidi.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 3.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa kuzindua rasmi wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) iliyopo katika jengo la Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Dk.Kigwangalla katika uzinduzi huo, amewapongeza watendaji wote waliofanikisha ikiwemo uongozi uliopita na ule wa sasa, Serikali pamoja na wadau wa sekta hiyo ya afya walioguswa na kuchangia upanuzi wa huduma za tiba ya wagonjwa hao Mahututi ambayo imewezeshwa kuwa na vifaa tiba vya kisasa huku ikiongezwa vitanda kutoka 8 hadi 25 kwa sasa.

Aidha, Dk. Kigwangalla ametoa shukrani ya kipekee kwa wadau waliojitolea kwa moyo wao kuchangia huduma hiyo ya wagonjwa Mahututi ikiwemo Shirika lisilo la Kiserikali la Gastrenterology Foundation kutoka Ujerumani na wadau wote kwa kuweza kufanikisha huduma hiyo kuweza kupatikana hapa nchini na kupunguza safari za nje ambazo zimekuwa zikiigharimu Nchi fedha nyingi.
 
Sasa tuanze kuona utekelezaji, tusiendelee kuona wagonjwa wanaendelea kupelekwa nje ya nchi
 
Sasa tuanze kuona utekelezaji, tusiendelee kuona wagonjwa wanaendelea kupelekwa nje ya nchi
Katika sekta ya afya Tanzania tuko nyuma sana, kuanzia vitendea kazi mpaka wataalam. sasa kupeleka wagonjwa nje kwa hivi sasa mpaka miaka 10 ijayo haliepukiki..Na hiyo miaka 10 mbele tutaweza kuanza kuona mafaniko once tukianza ku invest heavily katika sekta ya afya kuanzia hizi sasa na kuanza usanii.. la si hivyo tutaendelea kuuwa wananchi na kuwadanganya ya kuwa tuna uwezo wa kuyatibu magonjwa yote hapa.....
 
1.jpg
 
Back
Top Bottom