Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Akinamama wajawazito waliolazwa chini wameshahamishiwa wodi mpya yenye vitanda vipya ambao wamemshukuru sana Mh Raisi JPM kwa kusikia kilio chao na kutekeleza mara moja ahadi yake ya kutatua tatizo la kulala chini. Wakiongea wakiwa katika vitanda vyao vipya wameonyesha nyuso za furaha kama walivyorekodiwa na ITV.
WODI YA MAGUFULI MUHIMBILI YAANZA KUTUMIKA
Jengo ambalo lilikuwa linatumika kama ofisi za wafanyakazi kwenye Hospitali ya Muhimbili, ambalo Rais Dk. Magufuli ambalo alisema liwekewe vitanda ili kuweza kuwalaza akina mama wazazi waliokuwa wanalala chini kutokana na uhaba wa majengo limeanza kutumika rasmi.
Rais Dk. Magufuli alitoa agizo hilo wiki iliyopita alipofika Muhimbili kwa madhumuni ya kumwona Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu. Hata hivyo wakati anaondoka Rais alizuiwa na akina mama waliomsihi akaangalie shida wanayoipata kwa kulala kwenye magodoro yaliyokuwa yamewekwa sakafuni.
Pamoja na wasaidizi wake kumzuia kwani tukio hilo haikuwa katika ratiba yake ya siku hiyo, Rais aliamua kuitikia wito wa akina Mama na kwenda kwenye wodi ya akina Mama wazazi ambapo alishuhudia msongamano wa wagonjwa kiasi cha wengine kulala kwenye magodoro yaliyokuwa yamewekwa sakafuni huku wengine wakilazimika kulala zaidi ya mmoja kwenye godoro moja. Alipouliza chanzo cha tatizo alielezwa kuwa hospitalini hapo kuna tatizo kubwa la uhaba wa majengo.
Ndipo Rais alipoagiza kuwa kama hatua ya muda mfupi kuliko akina mama wazazi kulala sakafuni basi ni vyema jengo la ghorofa mboili lililokuwa linatumika kama ofisi ya wafanyakazi liwekewe vitanda na kutumika kama wodi ya akina mama wazazi.
Chanzo: ITV