Wizi wa taarifa za ATM card yako

UCD

JF-Expert Member
Aug 17, 2012
7,608
5,439
Wana JF,

Kuna wizi wa taarifa za ATM Card yaani Card Namba pamoja na CVV namba (herufi tatu zilizoko nyuma ya ATM Card. Wizi huu unafanywa na kundi la wizi hapa mjini wakishirikiana na wafanyakazi wasiowaaminifu wa Benki, mahoteli na Supermarkets. Hawa wizi wakishirikina na hao wafanyakazi wasiowaamiifu hunakili namba za card yako mara uendapo kufanya transations kwenye kaunta za Benki, Mahoteli na Supermarkets kaunta. Baadaye ATM Card na CVV namba hizo wanazitumia kununulia tiketi za ndege hasa Fastjet kupitia mtandaoni na kuziuza kwa watu mbalimbali hapa mjini.

Hivyo watu muwe maakini na ATM Card zenu hasa mkienda kufanya transactions kwenye Benki, Mahoteli na Supermarkets hasa muda huu wa Sikukuu za mwisho mwa mwaka. Pia msinunue tiketi za ndege ovyo ovyo mitaani mnaweza kuja pata matatizo yasiyowahusu.

Nawasilisha Waheshimiwa wa Bunge wa JF.
 
Kwani unaweza kufanya manunuzi bila no. ya siri?!
 
Jibu la swali Ndiyo.

Alichosema UCD ni kweli kabisa. MOTO (Mail order Telephone Order) haitaji pin. Pia kuna POS nyingine hazihitaji pin ila physical card lazina iwepo.
 
Sasa tutakuwaje makini cz wafanyakazi wa benki ndio wenye access na bank info.zetu zote.
 
Back
Top Bottom