Wizi wa mwananchi tcra inaujua?

Wizi wa mwananchi tcra inaujua?

seamlessly

Member
Joined
Jun 5, 2013
Posts
38
Reaction score
10
Gazeti la Mwananchi limeanzisha hv karibuni aina ya bahati nasibu inayoliiwa Shs 200 kwa ujumbe wa kushiriki. Hiki ni kiasi kikubwa cha pesa kinachokusanywa toka kwa wasomaji ambao baada ya kukatwa kiasi hicho hutumiwa ujumbe kuthibitisha wameingizwa kwenye bahati nasibu hiyo. Katika moja ya vigezo vyao wamesema makoswa pia yanatozwa. Cha kushangaza ni kwamba toka juzi wanarudisha ujumbe unaosema 'Samahani,huduma hii haipatikani kwa sasa' huku wakiwa wamekata Shs 200. Huu ni wizi wa mchana ambao Mwananchi wanafanya na wanatakiwa kuchukuliwa hatua na TCRA. Nchi hii imefganywa shamba la bibi na wananchi hatuoni vyombo husika vikitetea maslahi yetu.Hatua zozote ziendane na kurejeshwa pesa zilizoibwa kwa njia hii na kuombwa radhi.
 
Daa ni kweli kabisa , nikiwa kama msomaji wa gazeti hili hilo nililiona , na nnajua kabisa yawezekana ilifanyika makusudi , au ni matatizo ya kimitambo , lkn mwanachi kama chombo kikubwa cha habari mnapaswa kukiri kwa hili. Maana mwisho najua kuna watu ambao either walituma sms si chini ya mara tatu!. Isijekuwa ndo mnafidia kwa kiasi ambacho tayari mmekitoa kwa washindi. JIREKEBISHENI.
 
Kwa kuwa zoezi hili linafanyika kupitia mfumo wa elektroniki ni wazi kwamba linapotokea tatizo wanapata taarifa wakati huohuo,pia kama waliweka program ya kukata pesa pale msomaji anapotuma kwa makosa wameshindwaje kuielekeza program hiyohiyo kutokata pesa pale ambapo huduma hiyo haipatikani? Kimya chao wakati wanaendelea kukata pesa huku hakuna huduma ni ithibitsho wa wizi- si waseme basi kama gazeti lao sasa linauzwa sh. 1000 ?
 
Gazeti la Mwananchi limeanzisha hv karibuni aina ya bahati nasibu inayoliiwa Shs 200 kwa ujumbe wa kushiriki. Hiki ni kiasi kikubwa cha pesa kinachokusanywa toka kwa wasomaji ambao baada ya kukatwa kiasi hicho hutumiwa ujumbe kuthibitisha wameingizwa kwenye bahati nasibu hiyo. Katika moja ya vigezo vyao wamesema makoswa pia yanatozwa. Cha kushangaza ni kwamba toka juzi wanarudisha ujumbe unaosema 'Samahani,huduma hii haipatikani kwa sasa' huku wakiwa wamekata Shs 200. Huu ni wizi wa mchana ambao Mwananchi wanafanya na wanatakiwa kuchukuliwa hatua na TCRA. Nchi hii imefganywa shamba la bibi na wananchi hatuoni vyombo husika vikitetea maslahi yetu.Hatua zozote ziendane na kurejeshwa pesa zilizoibwa kwa njia hii na kuombwa radhi.

Binafsi ni mhanga wa wizi huu!

Leo Jumatano, 3rd September nimenunua gazeti na kuingiza namba very correct. Cha ajabu wamenikata hela, then wanarudisha message after 30min et nimekosea na inatakiwa niingize tarakimu 7!

Huu ni wizi, kwani nilikuwa sahihi katika kutuma message.

Tido Mhando, take action immediately, kama si wewe na kampuni yako mnatuibia, tazameni vizuri mkataba wenu na push!
 
Back
Top Bottom