mkuyati og
JF-Expert Member
- Apr 19, 2011
- 821
- 587
Goodmorning wakuu.
Napenda ku-share na nyinyi jinsi gani matapeli wa mtandaoni (mitandao ya simu) wanavyofanya wizi.
Tarehe 1 mwezi huu nilipokea simu kutoka kwa mtu ambaye alidai yeye ni afisa kutoka Airtel makao makuu (namba iliyotumika ni 0788-024-314). Huyu bwana aliniita kwa majina yangu matatu na kutaja majina yangu matatu. Alidai wamepokea malalamiko kwamba namba nayotumia kuna mtu anadai ni yake, hivyo wanataka kuhakiki kama kweli mimi ni mmiliki halali wa namba hiyo.
Hivyo akaanza kuniuliza tena kuanzia jina na details zangu ndogo ndogo. Kisha akauliza line niliisajili wapi na mwaka gani. Pia akauliza mwaka wangu wa kuzaliwa kama ambavyo nimeandika katika usajili wa namba hiyo.
Kilichokuja kunishtua ni pale alipoanza kuniuliza details zangu za matumizi ya Airtel money. Akataka kujua kama ninakumbuka mara ya mwisho kutumia huduma hiyo, kiasi gani kipo kwenye account na huwa natuma na kupokea kiasi gani kwa makadirio. (Mimi huwa sio mtumiaji sana wa Airtel money, so huwa empty mda mwingi). Mwishowe akadai nimtajie namba 15 ambazo nawasiliana nazo mara nyingi. Hapo nikakonfirm kwamba huyu tapeli, nikaona ni-buy time kwa kumuahidi kwamba naziandika pembeni then anipigie baada ya dk5 nimtajie. Akakubali.
Alipokata tu nikawapigia Airtel, wakanihakikishia fear yangu kwamba huyo ni tapeli, na kwamba wako wengi kwenye mitandao. Anachohitaji tapeli ni kuhakiki jina lako, then anaku-trick umtajie mwaka wako wa kuzaliwa. Akipata vitu hivi viwili anaweza kufunga/ku-swap namba yako na akaichukua yeye na kuanza kuitumia.
Nikawauliza Airtel kuwa wao wanaweza kunisaidiaje ili huyu mtu asitimize malengo yake, mtu wa customer care hakuwa na majibu. Akasema niangalie kama mtandao utakata ghafla kwenye simu basi hiyo ni dalili kuwa namba imekuwa hacked. (mind you hapo nilikuwa nimewatajia mpaka namba ya huyo mtu, nikaomba wamshughulikie).Basi nikaomba afunge account yangu ya Airtel money, akaifunga.
Basi jamaa akapiga tena, nikamchana akajidai anashangaa. Akanihakikishia yeye ni mfanyakazi halali Airtel, ila nikamwambia huwezi niibia,, wewe ni Maskini mwenye akili ndogo. (Katika mazungumzo yetu, taarifa alizofanikiwa kuzipata kwangu za msingi ni ku-confirm jina na mwaka wa kuzaliwa.
Sasa jana mchana niko na-browse JF mara mtandao wa mnara na Internet ikakata ghafla. Nikasubiri dk2 hamna kitu. Nikazima na kuwasha simu pia hamna kitu. Kuchukua simu ya wife mtandao umejaa tele. Nikashtuka, nikaipiga namba yangu ikaita akapokea mtu ila kukawa kuna chenga chenga simsikii. Akakata then akatuma sms yuko katika bad spot, nimtext. Nikapiga tena akapokea, nikamwambia naona umefanikiwa kunihack maskini wewe,nikamtukana na mengine. Akasema, "wewe si ulijifanya mjanja, so tunakufanyizia. Na hiyo namba yako nyingine naichukua pia". Nikamwambia chukua fala wewe, namba naweza badilisha na wewe huwezi pata kitu.
Nikawapigia Airtel nikaomba waifunge namba yangu, wakakubali. Cha ajabu ile namba bado iko hewani mpaka sasa, jamaa anawatext watu wote niliowahi/ninao wasiliana nao na kujidai nimepata shida naomba niazime 50-100 thousands nktairudisha asubuhi, ni dharura. Lakini kwakuwa nili-block Airtel money, hawezi kutoa hizo fedha. Instead anadai kuwa ameshindwa kutoa, anaomba atumiwe kwa namba nyingine ya Voda maana yuko karibu na huduma ya Voda pesa. Hapo wengi humshtukia.
Nikimpigia anaongea confidently, kwamba hawezi kushikwa na atahakikisha anamtoa pesa mpaka mke wangu,nyang'au kweli kweli.
Mimi maswali yangu kuhusu security mtandaoni ni haya:
1. Hivi inakuwaje mtu Akipata jina na namba ya kuzaliwa tu anaweza ku-hack line ya mtu? Only these two parameters? Hii ni security policy mbovu sana, it's too easy. Kuna watu ambao hutumia mwaka wao wa kuzaliwa katika sim-banking, tapeli anaweza kuingia katika account yako akakomba kila kitu. Usalama uko wapi wa pesa zetu?
2. Kwa kutumia IT inteligensia, naamini polisi na watu wa IT Wanaweza kum-pin point huyu mtu alipo na kumkamata,sidhani kama ni ngumu kiasi hiko. Cha msingi awe hewani tu. Sasa kama matukio kama haya ni mengi, mbona hamna kinachofanyika kukamata watu Hawa. Halafu, eti Mtu wa customer care ananijibu kuwa hata wao hawajui wafanyeje kuhusu watu Hawa! Haha, sijui yule mtoa huduma ni Intern ama yuko field,, maana alikuwa hana majibu ya maswali yangu,, akakakimbilia kuuliza kama nina concern nyingine then kukata simu.
3. Hawa watu ni watu aina gani, wako so confident. Yaani anaongea na mimi na ku-boast kwamba yeye anapata pesa kwa wizi, na hatakaa akamatwe. Na kwamba anatembelea makalio, na sasa anataka kujenga. Kuna wafanyakazi wanalinda watu Hawa?
4. Inachukua muda gani kufunga line ya mtu aliyetoa malalamiko kama haya, maana nimeshapiga mara mbili Airtel service, lakini toka jana jioni mpaka sasa namba bado iko hewani. Ugumu uko wapi?
SAMAHANI KWA MAELEZO MAREFU, JUST WANTED TO SHARE AND ALERT WOTE ILI YASIWAPATE NINYI PIA.