Wizi wa mtandao wa tigo kupitia tigobima

Wizi wa mtandao wa tigo kupitia tigobima

Shixi889

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2012
Posts
338
Reaction score
208
Kama sijakosea nilipigiwa simu na kampuni ya tigo mwezi June na kuambiwa kuhusu bima ya tigo na kuelezwa kuwa kama niitapenda kujiunga niende kwenye tigo shops nikajaze form. Kwa kuwa sikuona umuhimu wa huduma hiyo sikwenda na wala sikujiunga na hiyo bima.

Juzi nimepokea meseji kutoka tigo kuwa nina bima ya Tzs 50,000/= kwa ajili ya Pona (ambayo sijui ni kitu gani) & TZS 100,000/= kwa ajili ya Bima na makato ya mwezi yalikuwa Tzs 750.

Huu ni wizi kweupe mbona wanalazimisha wateja kujiunga na huduma?
 
Wapuuzi hawa tena sana,walishanipigia simu na kuniambia niingize number fulani kwenye simu yangu then niipige.

Nikamwambia huyo dada ntaingizije hiyo number wakati sina bima kama hiyo na sijasoma terms za hiyo bima?

Nikamwambie ndio hivo mlivosomea kuwahadaa wananchi wakubaliane na terms ambazo hawazijui?

Akajikanyaga basi kama ni terms nkazisome katika ofisi zao
nilimpa vidonge vya kutosha akakata simu.
 
Huu ni wizi wa wazi kabisa na ni kero kwa watumiji wengi wa tigo.Hii mitandao ya simu hata aibu haioni?mimi nitawapeleka mahakamani.Tigo...tutakutana huko.
 
wapuuzi hawa tena sana
walishanipigia simu na kuniambia niingize number fulani kwenye simu yangu then niipige
nkamwambia huyo dada ntaingizije hiyo number wakati sina bima kama hiyo na sijasoma terms za hiyo bima?
nkamwambie ndio hivo mlivosomea kuwahadaa wananchi wakubaliane na terms ambazo hawazijui?
akajikanyaga basi kama ni terms nkazisome katika ofisi zao
nlimpa vidonge vya kutosha akakata simu.

Wanakera sana hawa..!!embu imagine wanawaibia wateja kiasi gani halafu bado serikali inataka watukate tena kodi ya sim kwanini huyo mswada usingewapa wao jukumu la kutulipia hiyo kodi??halafu eti kuna TCRA wat the f...k are they doing???
 
Huu ni wizi wa wazi kabisa na ni kero kwa watumiji wengi wa tigo.Hii mitandao ya simu hata aibu haioni?mimi nitawapeleka mahakamani.Tigo...tutakutana huko.
mi wamenipigia cm zaidi ya mara 3 wanacctiza nijiunge na hyo bima ni akamwambia siihitaji hyo huduma akasema sawa huyo mdada nashangaa jana natumiwa sms nimekatwa 750 kwaaji bima.yaani hu mtandao umekuwa kero kweli
 
mi wamenipigia cm zaidi ya mara 3 wanacctiza nijiunge na hyo bima ni akamwambia siihitaji hyo huduma akasema sawa huyo mdada nashangaa jana natumiwa sms nimekatwa 750 kwaaji bima.yaani hu mtandao umekuwa kero kweli

Mi nadhani hawa jamaa tuwashitaki!Hili linawezekana!Huu ni wizi wa wazi wazi.
 
Na nyie mutakuaje na line za TiGo? Hilo jina lenyewe limeshapakazwa matope kumaanisha mambo ya aja u. Mnajitakia saingine, line toka enzi za boom hadi leo unapata salary!! Mh
 
Kama sijakosea nilipigiwa simu na kampuni ya tigo mwezi june na kuambiwa kuhusu bima ya tigo na kuelezwa kuwa kama ntapenda kujiunga niende kwenye tigo shops nikajaze form. Kwa kuwa sikuona umuhimu wa huduma hiyo sikwenda na wala sikujiunga na hiyo bima.Juzi nimepokea meseji kutoka tigo kuwa nina bima ya Tzs 50,000/= kwa ajili ya Pona(ambayo sijui ni kitu gani) & TZS 100,000/= kwa ajili ya Bima na makato ya mwezi yalikuwa Tzs 750.Huu ni wizi kweupe mbona wanalazimisha wateja kujiunga na huduma?
Nami pia nilipigiwa kipindi hicho na kusema ukweli yule mdada hakuwa proffesional kabisa, iliyonipelekea nimtwange maswali hadi akaniuliza "au huniamini?" I hope aliiitoa namba yangu kwenye hio bima yao
 
Pesa za kampeni wanatafuta! Mm wamenipigia mara saba...na nimewaambia mimi nina bima ya afya tayari lakini hawaelewi. Wanatafuta kutukanwa
 
Matapeli wakubwa ukitaka kujiroga weka salio alafu usijiunge kifurushi dk mbili tu utaona msg umekatwa 750 kwa ajili ya tigobima cjui. Mbaya zaidi mtu hata hujajiunga na iyo kitu izo hela cjui wanazipeleka wapi km sio wizi wa machomacho.
 
Back
Top Bottom