Wizi wa mitandaoni

Wizi wa mitandaoni

Mpigadili Tz

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2015
Posts
1,102
Reaction score
2,130
Habari zenu waungwana,

Tarehe 8/7/2017 katika ofisi ninayo fanyia kazi, kulitokea wizi (sikupigwa mimi) ilitokea hivi: Kuna jamaa alikuja kutoa pesa katika mtandao wa voda kiasi cha 270000 baada ya kutoa na kukabidhiwa kile kiasi na yule alikuwepo pale (wakala) yule jamaa akaondoka huku wakala akafanya shughuli zake wakati anataka kufunga hesabu zake (baada ya kazi) akakuta kiasi cha 270000 hakipo.

Akawa anajiuliza sana hatimaye akanipigia simu kunieleza nikamshauri apige simu mitandao yote aliyofanya muamala labda kuna kosa lilifanyika bila kujua.
Akaanza na tigo hola akaja Airtel hola alipofika zamu ya voda jibu alilopewa ni "kuna mtu mishale ya saa 4 asubuhi alitoa pesa kimakosa 270000 ile pesa tumeizuia alitupigia simu" Jamaa akashangaa akawaambia "mbona alitoa na nilimpa cash jamani" voda wakambwambia "subiri tukuunganishe nae".

Yule tapeli akawa akipigiwa simu hapokei kila akipigiwa hapokei ila huyu wakala akipigiwa anapokea na kumuuliza maswali ya kujirudia rudia kila mara mfano; kuna mtu alitoa pesa kimakosa hapo n.k sasa leo asubuhi wakati anafungua ofisi akakuta missed call kutoka voda ambayo ilipigwa saa 2 usiku.

Jamaa alichoamua kuwapigia simu wakamwambia "muamala umerudishwa kwa mteja tulipiga simu hukupokea" sasa nikawa najiuliza mbona mteja siku karibia 3 anapigiwa simu hapokei inakuaje wakala kapigiwa simu mara moja tu na hakupokea wakatoa maamuzi? Yote kwa yote nini kifanyike hapa?

Nawasilisha.
 
Pole mkuu

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Tumieni miamala ya kupita benki hizi za simu tuwaachie wamama zetu kule vijijini kwa ajili ya kupokelea pesa ya sukari na mafuta ya kupikia
 
Jihadharini na namba hizi

+255782067953, 0714934876, 0785246595 na +255713675205

Hawa jamaa ni matapeli chunga sana.

" 0714934876.(0785246595) anajiita dr Isack chiteto Amana Hospital. Kuna jina la nesi mstaafu mama Magreti Sanya linatumika

Biashara yao ni dawa inaitwa ZINAITWA OLODOX B0X 100 ya kuua 'mazalia ya mbu'.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mmoja alikunywa beer pale dagadaga za 70k akalipa kwa M-PESA alimwambia muhudumu hana cash kumbe baada ya kumtumia tu kapiga simu Voda kwamba kakosea muamala, mpaka muhudumu aje kusanda pesa jamaa kisha rudishiwa
 
pole sana, huu mchezo umechezwa kati ya huyo tapeli na mtoa huduma, ndo maana walikupigia usiku wewe haupo, utaratibu ni kwamba wakipiga cm haujapokea na kesho yake wanakutafuta tena muda wa kazi iweje wapige usiku? siku nyingine muhudumu wa mitandao akikupigia muulize jina viziri na yupo wapi ili kukusaidia badaye, nenda ofisini kwao uongee nao na huo muamala uandike uende nao, ukifanya miamala ya kutoa kwa mtu usiyemjua chukua kitambulisho na sahihi aweke
 
Back
Top Bottom