GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Wizi wa Kimafia Kampuni za Simu Tanzania Unadaiwa kuwapo mtandao mkubwa wa watu mkao makuu au katika matawi ya taasisi husika ambao hushiriki katika matukio ya wizi wa fedha za wateja wanaozihifadhi katika simu benki (Mfano ZAP, MPESA, Z-PESA, TIGO PESA) Mkasa uliotikisa zaidi ni ule ambao hivi karibuni umeikumba kampuni moja ya Simu (Jina limehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi) baada ya kuhamishwa shilingi milioni 15 katika akaunti ya mteja mmoja na kutumia huduma ya kuhamisha na kupokea fedha kwa njia ya mtandao. Tukio kama hilo limewahi kutokea na kusabishia mabenki matatu makubwa hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 300. Source (Mwananchi 13[SUP]th[/SUP] Juni 2011) Maswali ya kujiuliza hapa: · TCRA wanataarifa na matukio haya? ama hawapo tena hapa Tanzania, au wao ni kwa masilahi ya siasa tu kuzifungia Radio ambazo zinaikosoa serikali kama walivyofanya kwa Radio SAUT ya Mwanza? · Usalama wa pesa za mlala hoi uko wapi, maana huduma hii ya simu Benki imechukua umaaruufu Tanzania na kutishia uhai wa baadhi ya mabenki madogo kwa sasa yasiyokuwa na matawi kwingineko Tanzania. · Lakini kinachokera zaidi ni ubovu wa mitandao ambayo mara kadhaa imekuwa ikikorofisha na kujikuta akaunti hizi za simu benki pesa zimezidishwa mara mbili ya salio au kutokuwepo kabisa. · Dududuku kama hizi mbona hazizungumzwi na wahusika na kutolewa ufafanuzi wa Kina, au kwa kuwa ndio watangazaji wakubwa katika maradio na TV kwa hivyo wakiguswa tu wanaondosha ulaji. Hii inatuchanganya wadau Nawasilisha