Wizi UDSM si siri tena, ushahidi wapatikana

Wizi UDSM si siri tena, ushahidi wapatikana

SIRI YA KUCHOTWA KWA MAMILIONI YA DARUSO YAFICHUKA, RAIS NA WAZIRI MKUU WADAIWA KUONGOZA UFUJAJI WA FEDHA HIZO.
View attachment 237664



"WanaUDSM walia, wasema Mungu atawalipia kisasi"

Baada ya kufichuka kwa siri ya kuchotwa kwa fedha taslimu kiasi cha milioni 11 za serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam(DARUSO) hatimaye mambo zaidi yamezidi kuwa wazi kuhusiana na wizi huo wa "kalamu" uliofanya dhidi ya fedha za wanafunzi.

Mambo yako wazi kwa sasa kuwa Rais wa Daruso Nickson Filbert na waziri mkuu wake Gibson George ndio walioidhinisha fedha hizo baada ya kuiomba ofisi ya Dean of Students ambayo iliwaruhusu huku waziri wa fedha Innocent Mboya akitekeleza kwa haraka maamuzi hayo.


Tayari waziri mkuu amethibitisha kuwa fedha zimechotwa ila ameeleza kuwa ni mradi CRDB bus umetoa hizo fedha,

kweli njia ya waongo ni fupi, wizi umethibitika kwa kuwa mradi wa CRDB ni wa Daruso basi ni wazi fedha za umma zimechotwa na kuibwa huku baraza la mawaziri likibariki kwa kisingizio cha kumalizia uongozi. Huku wachotaji wakijua matumizi yote ya fedha za Daruso huidhinishwa na bunge na hakuna kikao cha bunge kilichoidhinisha fedha hizi kutumika kwa starehe za viongozi na marafiki zao.

Hongera waziri mkuu Daruso kwa kuwa mkweli kuwa kuna fedha za umma zimechotwa kutoka kwenye mfuko wa wana UDSM kinyume na bajeti iliyopitishwa na bunge.

Hii dhambi itawamaliza, haitawaacha salama.

Ndo hao wanaokuja hapa kudharau vyuo vingine oooooh tunaosoma udsm tulipata one cjui tunaufaulu mkubwa,Sasa dunia imejua leo hkna kitu udsm wezi tuu na watu wasio nauwezo wa kureasoning.
Udsm jina tuuu sahiv chuo ni udom
 
Ndo hao wanaokuja hapa kudharau vyuo vingine oooooh tunaosoma udsm tulipata one cjui tunaufaulu mkubwa,Sasa dunia imejua leo hkna kitu udsm wezi tuu na watu wasio nauwezo wa kureasoning.
Udsm jina tuuu sahiv chuo ni udom

Eti chuo ni uDom??? Hahah we jamaa utakuwa una kichaa??? Unapacompare udsm na udom?? Duuu au leo ni siku ya wajinga duniani nn
 
Back
Top Bottom