Ayubu Kivambiro
Member
- Jan 16, 2015
- 21
- 19
SIRI YA KUCHOTWA KWA MAMILIONI YA DARUSO YAFICHUKA, RAIS NA WAZIRI MKUU WADAIWA KUONGOZA UFUJAJI WA FEDHA HIZO.
View attachment 237664
"WanaUDSM walia, wasema Mungu atawalipia kisasi"
Baada ya kufichuka kwa siri ya kuchotwa kwa fedha taslimu kiasi cha milioni 11 za serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam(DARUSO) hatimaye mambo zaidi yamezidi kuwa wazi kuhusiana na wizi huo wa "kalamu" uliofanya dhidi ya fedha za wanafunzi.
Mambo yako wazi kwa sasa kuwa Rais wa Daruso Nickson Filbert na waziri mkuu wake Gibson George ndio walioidhinisha fedha hizo baada ya kuiomba ofisi ya Dean of Students ambayo iliwaruhusu huku waziri wa fedha Innocent Mboya akitekeleza kwa haraka maamuzi hayo.
Tayari waziri mkuu amethibitisha kuwa fedha zimechotwa ila ameeleza kuwa ni mradi CRDB bus umetoa hizo fedha,
kweli njia ya waongo ni fupi, wizi umethibitika kwa kuwa mradi wa CRDB ni wa Daruso basi ni wazi fedha za umma zimechotwa na kuibwa huku baraza la mawaziri likibariki kwa kisingizio cha kumalizia uongozi. Huku wachotaji wakijua matumizi yote ya fedha za Daruso huidhinishwa na bunge na hakuna kikao cha bunge kilichoidhinisha fedha hizi kutumika kwa starehe za viongozi na marafiki zao.
Hongera waziri mkuu Daruso kwa kuwa mkweli kuwa kuna fedha za umma zimechotwa kutoka kwenye mfuko wa wana UDSM kinyume na bajeti iliyopitishwa na bunge.
Hii dhambi itawamaliza, haitawaacha salama.
Eti oh mungu atawalipa badala ya kuwafata na kuwapa vitasa tu, wawaoneshe nguvu ya umma iko vp"Wana udsm wasema Mungu atawalipia" kauli ya kivivu sana hii! Wasomi wa chuo kikuu jasho lenu linaliwa alafu mnasema Mungu atawalipia!? Udsm nayo zero
Revo square imeota nyasi wanafuzi wa sikuizi mnapitia jkt lakini bado ni waoga sijui huko jeshini mlienda kujifunza uoga,. Badala ya kuitisha kunji hapo revo skwea unakuja huku jf unataka sisi tukusaidiaje sasa..
Kwani UDSM nacho ni chuo kikuu, hiyo ni taasisi ya mafisadi njaa. Source wazi wa escrow
Ume quote habari yote? kiazi kweli
Ni upuuzi, wanakuja kulalamika huku wanaacha kwenda level square, na kweli imependeza sana kwa kuota nyasi
Kam Udsm sio chuo kikuu basi Tanzania hamna chuo