Wizi na ubadhirifu unavyozitikisa nyumba za ibada nchini Marekani...!

Wizi na ubadhirifu unavyozitikisa nyumba za ibada nchini Marekani...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
preacher.jpg


Ukipita nje ya nyumba hizo za ibada na kusikia sauti inayopazwa kwa nguvu na msisitizo ikisema "Bwana Yesu Asifiwe" na waumini wakiitikia kwa shwangwe na vigelegele "amen" unaweza kuhamasika na kuona kweli watu wameamka na wanamtafuta Mungu kupitia kwenye makanisa haya yanayochipua kila uchao, lakini kumbe nyuma ya kauli hizo kuna matendo ya dhulma kwa wanyonge wanaojinyima na kumtolea Mungu ambapo jasho lao hilo linaishia kwa viongozi wao waliojivika utukufu wakati ni mbwa mwitu waliojivika ngozi ya kondoo.

Kwa nchini Marekani wenzetu wana mfumo mzuri wa kufatilia sadaka zinazotolewa na waumini katika makanisa ya jamii yao na katika utafiti ulifanywa hivi karibuni umebaini ubadhirifu mkubwa uliofanywa katika makanisa kumi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika nchini humo.

Katika utafiti uliofanywa na taasisi moja ya BSL Consumer Expenditure Survey ilibaini kwamba Wamarekani wenye asili ya Afrika hutumia kiasi cha dola 683 kwa mwaka kwa ajili ya michango ya kiimani ambapo yaweza kuwa ni zaka na sadaka. kwa hiyo katika utafiti huo taasisi hiyo imebaini kwamba tangu mwaka 1980 makanisa ya Wamarekani wenye asili ya Afrika nchini humo yalijikusanyia kiasi cha dola 420 bilioni kutoka kwa waumini wake, na kama unaamini kwamba michango hiyo imetumika katika shughuli halali za kanisa, bila shaka utakuwa unajidanganya.

Hapa chini kuna makanisa kumi nchini humo yametajwa kuwa yamefanya ubadhirifu mkubwa katika matumizi ya fedha za zaka na sadaka kutoka kwa waaumini wake.


Screen-shot-2013-08-06-at-4.37.47-PM.png


Goodwill Baptist Church (South Carolina)

Pasta John Albert Jackson Sr. 63, hajasalimika katika kashfa hii, waumini wa kanisa hilo lililoko katika viunga vya Madison S.C waligundua upotevu wa dola 66,657 wakati wa kipindi cha uongozi wake katika kanisa hilo uliodumu wka miaka 19. baada ya kubanwa na wazee wa kanisa hili kuhusu upotevu huo wa kiasi kikubwa cha dola, Pasta huyo alijiuzulu hapo mnamo mwaka 2011.
Hata hivyo kujiuzulu kwake hakukumnusuru, kwani mnamo gosti 2013 yeye na mwanaye wa kiume walifunguliwa mashitaka kujibu tuhuma hizo

congregants.jpg


City of Refuge Presbyterian Church (Texas

Kanisa hili lilipata kashfa ya upotevu wa kiasi cha dola 200,000 na Pasta wa kanisa hilo Russeli Thomas, 55, hakuepuka kunywa kikombe hicho, ilibainika kwamba alikuwa ameficha kiasi cha dola 284,503 katika akaunti yake ya siri kwa kipindi cha miaka miwili. Hata hivyo alikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa wizi huo, na sasa anaomba aonewe huruma na baraza la wazee wa kanisa hilo

smiling-preacher.jpg


New Birth Baptist Church (Georgia)

Hapa kulikuwa na ule mchezo wa DECI, bwana mmoja aliyetajwa kwa jina la Ephrem Taylor ambaye awali alitambulishwa katika kanisa hilo na Pastor Eddie Long alianzisha utapeli aina ya DECI ambapo kwa wenzetu huko Marekani wanauita Ponzi Scheme, na jina hilo lilitokana na Muitaliano mmoja huko nchini Marekani aliayeanzisha utapeli huo miaka ya 1930, na kuishia kufungwa. Awali kijana wa kiume wa mchungaji huyo alijizolea kiasi cha dola 11 Milioni, kutoka katika matawi ya kanisa hilo yaliyopo katika majimbo takriban 40. Hata hivyo Taylor naye kwa kutumia utapeli wake wa DECI alimshawishi mama mmoja ambaye alikuwa ni muumini wa kanisa hilo kuwekeza kisi cha dola 122,000 kama mpango wa akiba yake ya maisha kwa ahadi ya kuja kuvuna baadaye, lakini Taylor alitoweka na kiasi hicho kusikojulikana, na taarifa za utapeli huo zilikuja kuvuja mwaka 2012. katika hukumu yake dhidi ya Taylor, Jaji alimhukumu alipe kiasi hicho cha fedha

pastor.jpg


Life Reach Ministries (Illinois)


Mchungaji Howard Richmond, 53, anayemiliki kanisa hilo katika viunga vya mji wa Aurora. Huyu bwana alikuwa na ndoto kubwa kubwa katika malengo yake. Huyu aliwashawishi waumini wake wasaidie kuchangia mradi mkubwa kwa ajili ya kanisa lake, ambapo muumini mmoja alimpa kiasi cha dola milioni moja. walimuamini sana na walijua huyo ndiye kiongozi wao na waliamini kwamba ni mtu muaminifu anayesimamia maandiko matakatifu. wakati waumini wakatarajia mradi huo wa kanisa utakua na kuanza kuwanufaisha, lakini mchungaji huyo aliutelekeza mradi huo na kuanza maisha ya kifahari kwa kujinunulia magari ya thamani, vito vya thamani na sfari za kitalii katika visiwa vya Hawaii huku akiw ana matumizi makubw ana ya fujo katika mahotekli makubw aya kifahari. safari yake ya kustarehe ilikoma baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.


parishioners.jpg


Macedonia Baptist Church (ohio)


Katika kanisa hili Mchungaji Quentin L. Respress, 44, alipatikana na hatia ya ubadhirifu wa kiasi cha dola 54,081, kwa matumizi yake mwenyewe. katika hukumu ya kesi yake aliamriwa kulipa kiasi cha dola 54,000.



bible-preacher.jpg


New Mt. Zion Missionary Baptist Church (Florida)

Hapa Pasta Joe Seephis Hardie, 68, alijizolea kiasi cha dola 100,000 kutoka katika kanisa hilo. mnamo Agosti 2013 alipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya fedha na kusafirisha fedha harama kuanzia mwaka 2007, 2008 na mwaka 2009.

praying.jpg


Bethel Institutional Missionary Baptist Church (Texas)

Pasta Charles Gilford na mkewe Adriane Gilford hawa waliiba kiasi cha dola 430,000 kutoka katika kanisa hilo. Walishitakiwa kwa kosa hilo.


preaching.jpg


St. Paul Christian Methodist Episcopal Church (Illinois)

Pasta Bernard Johnson, 47, huyu alifuja kiasi cha dola 50,000 kuanzia mwaka 2008 hadi mwak 2010 na mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani, hata hivyo aliamriwa kulipa kiasi cha dola 10,000

pews.jpg


New Hope Missionary Baptist Chuch (Florida)

Pasta John Murff, 37, huyu alijichotea kiasi cha dola 5,567 katika kanisa hilo kwa matuimizi yake binafsi ya kulipia bili za umeme na muda wa hewani wa simu zake za mkononi pamoja na matumizi mengine. Aliachiwa kutoka gerezani mnamo May 2014 baada ya kulipa dhamana ya kisai cha dola 1,000.

lone-prayer.jpg


Hilltop Apostolic Church (California)

Pasta Bruce Anthony Stark alifanya ubadhirifu katika kanisa hilo wa kiasi cha dola 100,000 na ubadhifu huo unahusicha pia wizi wa fedha, magari na kipande cha ardhi cha kanisa hilo. Pasta huyu alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela


Kwa hisani yenu naomba Mods msiuhamishie huu uzi katika jukwaa la dini........

CC: Asprin, Nyani Ngabu, Kiranga, snowhite, Fixed Point, Husninyo, The Boss, Mr Rocky, Arushaone, Mungi, ayanda, mwekundu, Pasco, ICHANA, miss neddy, miss chagga, Kongosho, Munkari, MankaM, Tina, Tina, sister, Paloma, Kaizer, Ruttashobolwa, Mentor, kabanga, Elli
 
Mh. So wrote wasemao bwana bwana.though smtymz tuhuma zinalengo la kuwakwaza believers.
 
nipo na amani kwa sababu even biblia imeshasema siyo kila wasemao bwana bwana watamwona Mungu.... na nyakati za mwisho manabii wa uongo wataibuka... so for that case hekima ya mtu mmoja mmoja inatakiwa kufanya kazi... amina
 
aiseee.......
kuna baadhi ya sehemu michango ya ujenzi wa kanisa inaendelea miaka nenda rudi............kanisa halijengwi wala nini!!!
 
asnte mkuu Mtambuzi kikubwa ni ni kufanya yaliyoandkwa kwenye biblia
hatutaingia mbinguni kwa kuyafuata yale ya wachungaji.mapadri or shekhe...
hawa ni binamu kama sisi ila wanatuongoza na siyo yote yle wanayotufundisha ndo wanafanya nooo wana udhaifu kama binadamu wa kawaida

matendo yetu ndo muhimu kwa maana ndio hukumu yetu

maknisa ni mengi wizi sio wa sadaka tuu hapana...kuna michango mingi sana na wamekuwa na tbia ya kuogopesha waamini na sheria wanaweka utasikia HUBARKIWI usipotoa huo mchango unabaki tunajiuliza tangia lini kwa MNGU kukawa na msharti,vitishona sheria na viwango vya pesa.

hawa wakuu wa makanis sasa wanafany kama sehemu za biashara,tuhuma nyingi za ubakaji,kutembea n wake za watu,mabint,wizi wa mali za kanisa nk

kauli mbiu inabaki pale pale kanisa bado ni zuri ni nyumba ya kumwabudu MUNGU ila kama kiongozi wako ni mchafu usihame kanisa or kutokwenda kwa maana huendi kwa ajili yke...bali kwa ajli ya maisha ya mbingun.
 
Na hawa manabii na mitume wa kwetu hapa Bongo si yale yale? Au wame-copy na ku-paste?
 
Mimi naona kama huko wameiba chache, hasa ukizingatia wenzetu na sheria zinafanya kazi.Ukifanyika uchunguzi kuku Bongo watu watazimia maana huku wanajisifu waziwazi kwa utajiri wa magari ya gharama na majumba Pembezoni mwa bahari.
 
Duu utafiti kama huo ukifanyoka tanzania waumini watalia!wajinga ndiyo waliwao.Haya makanisa ya kisasa balaa tupu
 
Tulipotea tulivyo komesholaizi dini, hapo tu, wala sishangai kabisa.
 
aiseee.......
kuna baadhi ya sehemu michango ya ujenzi wa kanisa inaendelea miaka nenda rudi............kanisa halijengwi wala nini!!!
Paloma nina jirani yangu alinilalamikia, anasema anakomweshwa na michango ya kanisa lao kwa uchache aliitaja michango hoyo

-Kuna sadaka hiyo ni lazima
-kuna zaka hii nayo ni lazima
-Kuna michango ya Jumuiya nayo ni laizma na usiposhiriki kwenye jumuia utatengwa
-Kuna minada ya kuchangia ujenzi wa kanisa
-Kuna kuchangia ujenzi na upanuzi wa kanisa
-Kuna kuchangia sijui kitu gani hapo nimekisahau, yaani alilalamika mpaka nikamuonea huruma
 
haaa Mtambuzi hapa nimefikaje sistahili kabisa siye an Eiyer tuna parokia yetu pekee..hawa wamarekani ni kama wetu tu,,,,wanaoongoza haya makanisa ni binadamu kama sisi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom