Wizi mkubwa kivuko cha Magogoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi mkubwa kivuko cha Magogoni

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Las Mas Bobos, Jun 18, 2012.

 1. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu juzi nimepita kivukoni nikienda Mjimwema na baadaye kurudi tena mjini, kwa kweli ni balaa. Pale kwenye maeneo ya kupumzikia kusubiri kivuko pamenifanya nishangae na kujiuliza ikiwa hii nchi ina serikali.

  Nafikiri wakuu mnakumbuka si muda mrefu sana uliopita, nauli za kivuko pale ferry zilipandishwa na serikali kwa madai ya kujiimarisha katika kukabili gharama za uendeshaji. Pakazuka malumbano yaliyofuatia kejeli zilizotolewa na waziri wa miundombinu Mh. Magufuli.

  Katika hali ya kushangaza, utaratibu niliouona miaka 6 iliyopita bado nimeukuta unaendelea. Wale wakatisha tiketi wamekuwa vinara wa kuuza tiketi moja mara mbili. Unapokabidhi tiketi yako ichanwe, jamaa anayepokea huangalia upepo na endapo akibaini hakuna macho yanayomuelekea, bunch la tiketi alizoshika halichwani badala yake hutupwa kwenye pipa kama zilivyo. Navyofahamu, baadaye hutolewa na kuuzwa tena.

  Ikiwa huu ndio uendeshaji wa kivuko, kulikuwa na haja gani kupandisha nauli kwa kisingizio cha mapato ikiwa yanaishia mikononi mwa watumishi wa kivuko? Hivi wizara na serikali kwa ujumla haliyajui haya? Mwaweza kuona ni ulalamishi wangu tu usio na sababu, lkn wakuu kila anayepita pale achunguze, atakubaliana na mimi kuwa hawa jamaa wanagawana mapato na kivuko kwa almost 50/50 na huu ni utaratibu wa miaka mahali pale
   
Loading...