Kama EWURA walizuia wanajua madhara wateja wanayoyapata? Nikizimikiwa gari njiani mafuta yameisha niwaite EWURA kusukuma liende petrol station? Je TANESCO nao niwaombe lori lao lijazwe wakafaulishe kwenye jenerata yangu?Watoe ufumbuzi na siyo kuwajengea mazingira ya kutuibia na kutukomoa.EWURA walikataza vidumu, ila hakutoa ufumbuzi kwa wanaonunua kwa ajili ya jenereta au kukatikiwa mafuta njiani.
Huku Arusha ndiyo usiseme huo uchakachuaji ndiyo imeshika kazi. Kwa mfano kwa wenyeji wa hapa Arusha wanaoielewa ile ki2o kongwe hapa mjini cha Bamparass kilichopo mtaa wa Mianzini ni hatari wanaweza kukuwekea hata hewa. Ila nitajifanya siku moja mi ni afisa wa EWURA halafu ha2taelewana kabisa. Wizi mtupu!
nakujibu kama meneja wa kituo cha mafuta jijin dar es salaam.
Sheria ya kuzuia vidumu ilipitishwa na ewura mwaka huu na imejieleza wazi kabisa, haviruhusiwi vidumu vya maji ya uhai na jamii hiyo,sababu surface yake ni ndogo,sio hivi vidumu vingine nyenye surface kubwa,hii ni kwa sababu vidumu nyenye surface ndogo haviwez kukabiliana na density ya petrol vinaweza kupasuka endapo kitapata mtikisiko mkubwa. Nazungumzia surface area to volume ratio.
Nimependa na kufurahia neno hili "pomoni" ni aghalabu kulisikia au kusoma mahala limeandikwa. Hongera Mkuu! Sina hakika kama vijana walowengi wanalitumia.Ulijaza pomoni ndo maana. Inapezekana hujaibiwa.