Wizi katika mashine za TRA za risiti Kariakoo

kemi2011

JF-Expert Member
Dec 25, 2013
735
290
Jamani ebu nisaidieni, kweli Serikali inalijua hili?

Kariakoo ukinunua kitu cha thamani ya Mil 2 unapewa risiti ya laki tatu tena na kufokewa juu! Jamani huu si ni wizi?

Serikali itafanya nini kudhibiti hili?
 
Halitadhibitiwa iwapo halitaripotiwa kwa mamlaka husika...
Cha msingi ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika...
 
Watu washachakachua au ndo wanaprint za hela kidogo? Npm picha ya hiyo lisiti tuanze na huyo alokufokea
 
TRA tafadhali toa namba za kuwasiliana nanyi tuwape taarifa za wakwepa kodi.

Mimi juzi nimepewa risiti kwenye duka la dawa. Nilipoiangalia nikiwa nimeshaondoka penye kiwango cha VAT=ZERO.
 
Ushahidi wa risiti na invoice?
Umechukua maamuzi gani baada ya kupewa hiyo risiti?
Naamini wafanyabiashara hawalalamiki kuhusu hiyo hali
Wewe si mmoja wao
 
Labda hyo dawa ina exemption.
 
TRA tafadhali toa namba za kuwasiliana nanyi tuwape taarifa za wakwepa kodi.

Mimi juzi nimepewa risiti kwenye duka la dawa. Nilipoiangalia nikiwa nimeshaondoka penye kiwango cha VAT=ZERO.

Siyo kila Mashine inatoza VAT
 
TRA tafadhali toa namba za kuwasiliana nanyi tuwape taarifa za wakwepa kodi.

Mimi juzi nimepewa risiti kwenye duka la dawa. Nilipoiangalia nikiwa nimeshaondoka penye kiwango cha VAT=ZERO.
Hujaibiwa bali hiyo bidhaa uliyonunua ipo kwenye class ya zero rated product yani vat imetolewa kwa mtumiaji wa mwisho na mostly wana target bidhaa inayowakuta wanyonge wengi.

Pindi bidhaa inapouzwa mwenye duka anaruhusiwa ku claim vat serikalini

Pia kuna possibility bidhaa hiyo iko exemped kabisa na vat kwahiyo hata wakati wa kuingiza bidhaa hiyo hailipiwi kabisa vat na mwenye duka haruhusiwi kudai au claim vat serikalini (TRA)

Asante
 
Ushahidi wa risiti na invoice?
Umechukua maamuzi gani baada ya kupewa hiyo risiti?
Naamini wafanyabiashara hawalalamiki kuhusu hiyo hali
Wewe si mmoja wao
Auweke mezani ushahidi wake
 
TRA tafadhali toa namba za kuwasiliana nanyi tuwape taarifa za wakwepa kodi.

Mimi juzi nimepewa risiti kwenye duka la dawa. Nilipoiangalia nikiwa nimeshaondoka penye kiwango cha VAT=ZERO.
Huenda hiyo dawa ina msamaha wa kodi
 
Hujaibiwa bali hiyo bidhaa uliyonunua ipo kwenye class ya zero rated product yani vat imetolewa kwa mtumiaji wa mwisho na mostly wana target bidhaa inayowakuta wanyonge wengi.

Pindi bidhaa inapouzwa mwenye duka anaruhusiwa ku claim vat serikalini

Pia kuna possibility bidhaa hiyo iko exemped kabisa na vat kwahiyo hata wakati wa kuingiza bidhaa hiyo hailipiwi kabisa vat na mwenye duka haruhusiwi kudai au claim vat serikalini (TRA)

Asante

Nashukuru kwa kunielewesha.
 
TRA tafadhali toa namba za kuwasiliana nanyi tuwape taarifa za wakwepa kodi.

Mimi juzi nimepewa risiti kwenye duka la dawa. Nilipoiangalia nikiwa nimeshaondoka penye kiwango cha VAT=ZERO.
Nani kakwambia dawa inalipiwa VAT au umekariri tu neno VAT?
 
Jamani ebu nisaidieni, kweli Serikali inalijua hili?

Kariakoo ukinunua kitu cha thamani ya Mil 2 unapewa risiti ya laki tatu tena na kufokewa juu! Jamani huu si ni wizi?

Serikali itafanya nini kudhibiti hili?
yanakuhusu nini hayo,mbona escrow mlikamuliwa vilivyo
 
Jamani ebu nisaidieni, kweli Serikali inalijua hili?

Kariakoo ukinunua kitu cha thamani ya Mil 2 unapewa risiti ya laki tatu tena na kufokewa juu! Jamani huu si ni wizi?

Serikali itafanya nini kudhibiti hili?

Mkuu, juzi Kati nimeenda duka moja la vipodozi kariakoo nimenunua dawa 3 za mswaki nikapewa risiti ya efd imaendikwa Eti nimelipia 75000/- shs wakati dawa moja inauzwa 2500/- shs. Nikapewa risiti nyingine pia ambayo ina ukubwa tofauti na ile ya efd kwa pamoja ambayo Bahati mbaya sikuisoma imaendikwa nini. Nilipofika getini mhudumu alipiga mhuri ile nyingine na kuninyang'anya nikaachiwa ile ya 75000/- shs. Kuna kamchezo flani sio bure.
 
unatakiwa kuwa na ujasiri wa kuhoji, sio kukubali tu kila kitu. jukumu la kujenga nchi ni letu sote, tusiiachie serikali .
 
Jamani ebu nisaidieni, kweli Serikali inalijua hili?

Kariakoo ukinunua kitu cha thamani ya Mil 2 unapewa risiti ya laki tatu tena na kufokewa juu! Jamani huu si ni wizi?

Serikali itafanya nini kudhibiti hili?
Hauko serious mkuu huwezi nunua bidhaa ya 2m harafu ukapewa receipt ya laki 3 ukaridhika eti kisa umetukanwa? Swali la kwanza hyo bidhaa ilkuwa inapatkana duka hilo peke yake kwamba usingeweza kuipata duka jingine? Kama ndivyo ulishindwa kutoa taarifa police juu ya wizi huo? Maana we ndiye uliyeibiwa au ulitaka TRA waote ndoto juu ya uharifu huo?
 
Hakuna serikali inayoweza kutimiza majukumu yake bila kukusanya kodi zote stahiki.

Itakuwa kazi kubwa kuwafikisha watanzania katika utamaduni wa kulipa kodi ipasavyo. Hakuna njia ya mkato lazima zoezi la kuhakikisha kila anayestahili kulipa kodi anafanya hivyo.

Wenzetu walifanikiwa kwa kutoa adhabu mbili muhimu. Kumfilisi mhusika na kwenda jela. Ikifanyika kwa wafanya biashara angau watano tu pale Kariakoo, wengine wataifyata mikia mikia yao na kuanza kulipa kodi. Zoezi hilo lifanyika kila sehemu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom