Nimekutana leo na mkandarasi kutoka nchi za NORDIC ambaye kampuni yake inajenga moja ya barabara nyanda za juu kusini TZ. Anasema wanaibiwa mafuta (diesel),cement na kila kitu kinachoweza kuchukuliwa, ila juzi jioni ndio alichoka kabisa- mzee mmoja aliyekuwa anamwamini sana, akamfanya msaidizi wake wa nyumbani,alitoa mpya. Mkandarasi huyu alialika wageni wake nyumbani kwa chakula cha jioni,akaweka mvinyo mezani, wageni walipoanza kunywa, wakawa wanakunja uso, hivyo akalazimika kuonja mvinyo ule,na wa mshangao mkubwa, akagundua kuwa chupa zote nne mvinyo umepunguzwa halafu badala yake wakajaza maji.Kule ndani wanaishi watu wawili tu maana ni kambini,maana yake ni kwamba kumbe hata yule mzee ni mwizi., alikuwa nakunywa mvinyo wa bosi wake na kujaza maji badala yake.
Nikiwa naangalia taarifa ya habari TBC nikasikia tena wakaguzi wa maduka ya madawa, wamewakamata wauguzi wa Hospitali za serikali wenye maduka ya madawa ya binadamu huko Songea, wakiwa wanauza madawa waliyoyaiba hospitalini kwa mwajiri wao-kwenye maduka yao binafsi!
Swali, hivi hii hali ya watu kuiba kwenye sehemu za kazi kwa kiwango hiki, ni kwetu tu hapa TZ tu au ni tatizo pia kwa nchi nyingine? kama ni sisi tu litaishaje jamani?
Hii ni hatari sana sana kwa uwekezaji-kwa wawekezaji wazalendo(wa ndani) na hasa wawekezaji wa nje, ambao wanaweza kupeleka mitaji mahali pengine. Lakini pia kwa ajili ya fursa za ajira kwa vijana wetu,waajiri wataogopa kuwaajiri wa Tz. Mi naona tutafakari halafu tuchukue hatua