Wizara yamjibu Zitto kuhusu ununuzi wa ndege

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,996
Akizungumza na JAMHURI, Katibu Mkuu anayeshughulika na Sekta ya Uchukuzi, Dk. Leonard Chamriho, amesema kumekuwapo mchakato wa wazi katika kuwapata wazabuni wawili ambao kimsingi ndio watengenezaji wa ndege hizo kubwa.

“Kutokana na ukweli kwamba watengenezaji wa ndege aina hiyo ni wawili tu, tuliamua kutumia ‘restricted tender’ ambayo kimsingi Sheria ya Ununuzi na Ugavi inaturuhusu kufanya. Tulifanya hivyo kutokana na mazingira yenyewe tuliyonayo,” amesema Dk. Chamriho.

Amesema, katika zabuni hiyo zilijitokeza kampuni mbili za utengenezaji wa ndege, ambazo ni Boeing na Air Bus.

Ameliambia JAMHURI kuwa kampuni zote ziliruhusiwa kuwasilisha taarifa za bidhaa zao mbele ya jopo la wataalamu. Dk. Chamriho anasema wote walionesha ugumu wa kupatikana ndege kwa haraka, lakini pamoja na vingine vilivyozingatiwa, ilikuwa gharama pamoja na mahitaji ya ndege hiyo kwa wakati ambao inahitajika.

“Ninakumbuka Air Bus walituambia wataweza kutupatia ndege hiyo kuanzia mwaka 2023, huku wakitupatia chaguo la kukodi ndege kama hiyo. Hatukuhitaji kukodi maana tunayo historia mbaya katika mikataba ya kukodi ndege.

“Boeing wao walisema wanaweza kutupatia slot ndani ya Juni 2018; kutokana na mazingira tukalazimika kuendelea na mazungumzo na Boeing, walitutaka kuweka fedha za dhamana ya kutengeneza ndege hiyo. Tuliwalipa dola milioni 10 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 22).

“Baada ya kulipa malipo hayo, tulipewa muda wa mwezi mmoja kujadiliana kuhusu masharti ya mkataba wetu wa kununua ndege hiyo pamoja na vipimo (specification) kwa mujibu wa mahitaji yetu,” Katibu Mkuu, Dk. Chamriho ameliambia JAMHURI.

Amesema Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi ameshiriki katika kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri.

“Balozi Masilingi alifanya ziara makao makuu ya Boeing na kukutana na rais wa kampuni hiyo, mazungumzo yao yameleta ahuane kubwa sana katika majadiliano mpaka kufikiwa kwa makubaliano ya mkataba,” amesema.

Kuhusu muda wa majadiliano hadi kufikia makubaliano ya kusaini mkataba, Katibu Mkuu huyo anasema iliwachukua “muda wa kutosha” kujadiliana na hatimaye kusaini mkataba wa ununuzi wa ndege.

Hadi makubaliano hayo yanafikiwa kati ya Boeing na Serikali, kulikuwa na majadiliano ya kimkataba yaliyoongozwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Wakala wa Ndege za Serikali; Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

Dk. Chamuriho amesema baada ya kutiliana saini, ulifanyika utaratibu kwa ujumbe wa Boeing kwenda kumwona Rais John Magufuli. “Walikwenda kufanya ‘courtesy call’, hiyo ilikuwa baada ya makubaliano yetu kukamilika”.

Hata hivyo Dk. Chamriho, hakuwa tayari kuliambia JAMHURI, serikali imelipa kiasi gani, huku akisisitiza kwamba, serikali haikulipa kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye mtandao wa Boeing.

“Pale kwenye mtandao wao wameweka list price, baada ya majadiliano bei ilipungua, lakini kwa mujibu wa mkataba tulioingia na kampuni hiyo, sitakiwi kusema tumekubaliana kiasi gani, lakini kwa hakika maana sisi tulikuwa na fedha mkononi, gharama ilipungua,” amesema Dk. Chamriho

Taarifa ambazo JAMHURI limezipata na kuthibitishwa na vyanzo vyetu, zinasema Air Bus, baada ya kukosa zabuni walianza kutoa vitisho vikiwamo vya kuishitaki Tanzania kwa Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya (EU), wakidai kuwa kulikuwa na utapanyaji fedha katika ununuzi wa ndege hiyo.

Aidha, Air Bus na wapambe wake walikwenda mbali zaidi hata kumchongea Dk. Chamuriho kwa Rais Magufuli.

Katibu Mkuu alishitakiwa kwa Rais Magufuli, kupitia barua iliyoandikwa na Air Bus kwenda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Katika barua hiyo, walimtuhumu Dk. Chamuriho kutowapatia kandarasi na badala yake kuwapatia Boeing zabuni hiyo ya mabilioni ya shilingi.

Alipoulizwa na JAMHURI kuhusu tuhuma hizo, Dk. Chamriho alisema ni kweli alishtakiwa kwa Rais Magufuli, kutoa upendeleo kwa kampuni ya Boeing.

“Uchunguzi umeshafanyika, nadhani waliochunguza walipata ukweli wa tuhuma hizo dhidi yangu, lakini pamoja na hayo nililazimika kuandika maelezo na naamini ukweli umebainika,” amesema Dk. Chamriho.

Katibu Mkuu huyo anawataja Hadi Akoum, Makamu wa Rais wa Air Bus, anayeshughulikia mauzo katika bara la Afrika na ukanda wa Bahari ya Hindi, pamoja na Jerome Charieras, Mkurugenzi wa Mauzo pamoja na uhusiano wa wateja, ambao walikwenda kulalamika wakihoji Boeing kupewa zabuni hiyo badala ya wao.

Anasema katika mazungumzo yao walionesha kwamba hata Boeing hawataweza kukamilisha kwa wakati, na kwamba nafasi waliyonayo ni sawa na Air Bus yaani mwaka 2023.

Dk. Chamriho amesema wakazidi kumshawishi kwamba Boeing wataiuzia Tanzania ndege zilizokataliwa za ‘Terrible Teens’.

Katika mazungumzo yao walikuja na hoja kwamba walikuwa na mkataba na Air Tanzania (ATCL) pamoja na Senangol ya China, ambayo iliingia mkataba na ATCL mwaka 2012, huku wakisisitiza kwamba walishachukua fedha ya kiasi cha Dola za Marekani Milioni 2.5, (Zaidi ya Sh Bilioni 5) kama sehemu ya mkataba wao na washirika hao wawili.

Dk. Chamuriho amesema, aliwajibu kwamba sehemu ya mkataba huo hauna uhusiano na ununuzi wa ndege mpya aina ya Boeing 787-800 Dreamliner, isipokuwa hiyo ilikuwa inanunuliwa na Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA).

“Waliniambia kutorishwa kwao na mchakato, lakini wakasema lolote linaweza kutokea kwa nchi za Kiafrika…nikawauliza mnamaanisha nini? Kwamba nimepokea rushwa? Wakasema inawezekana, nikawataka waondoke ofisini kwangu, maana kwangu hiyo ilikuwa ni dharau kubwa,” amesema Dk. Chamriho.

Mbali na ajenda hiyo, wakamwambia hapakuwa na ushindani wa wazi, na kwamba Tanzania imekuwa ikipokea misaada kutoka EU na hivyo watakwenda kuishtaki huko na katika Benki ya Dunia.

JAMHURI limewasiliana na Hadi Akoum kwa barua pepe ili kuthibitisha baadhi ya tuhuma zao, mpaka tunakwenda mtamboni hakuwa amejibu.

Masuala muhimu katika mkataba

a) Dhamana: Kuna dhamana ya uwezo wa ndege (aircraft performance), kuna dhamana ya aina ya ndege iliyochaguliwa (aircraft model applicability), kuna dhamana ya mwonekano na vifaa/nakshi vilivyochaguliwa kuwekwa ndani ya ndege.

b) Bei ya ndege: Bei ya mwisho ya ununuzi wa ndege inatokana na bei iliyotolewa kampuni (listed price), na ukitoa punguzo (concessions).

C) Bei ya kampuni kwa jumla inahusisha bei ya umbo la ndege (airframe), bei ya injini, bei ya vitu vya nyongeza vinavyochaguliwa na mnunuzi (optional features), bei ya mifumo ya burudani ndani ya ndege (inflight entertainment system), na punguzo.

Mengine ni punguzo litokanalo na majadiliano (Basic credit memorandum), punguzo la kimkakati (Strategic relationship memorandum), na punguzo la kumwezesha mteja kukidhi mahitaji ya utumiaji wa ndege (Goods and services memorandum).
 
Hajasema lolotekuhusu kununua ile range kimeo??? Mbona hapo ameparuka?? Na bei ya punguzo iliyo ndani ya offer kwa zile mbovu?? Hajui hiyo ndege ajili ya international trips?? Abiria hasa wanaojitambua wataogopa kupamnda na romours zikienea wameliwa!!!! Sijui watafanya nini na hasara hiyoo!!!
 
Kama serikali hii ya awamu ya 5 imejipambanua kwenye kupambana na kila aina ya rushwa na ubadhilifu..

Kwanini inaficha Final Price ya hii ndege after concessions??

Ni kitu ambacho watanzania ni haki yetu kufahamu pesa tunayolipia ndege hii kwa maana ya final price kwasababu hizi ni pesa zetu walipa kodi wa Nchi hii.

Hii ndege sio hisani ya mtu fulani..
Ni pesa zetu watanzania..
Ivyo tuelezwe final price.
 
Kwa hiyo airbus ndiyo wamevumisha taarifa baada ya kunyimwa tenda?

(Refu ukisoma unasahau ya juu)
Kuna uwezekano mkubwa ni hao Airbus wamemlisha Zitto ''matango pori''!

Kuna mapambano makali ya kibiashara katika haya makampuni.

Kwa wasiofahamu hii vita wanaweza kusoma hii article,

LINK>>Neither Boeing nor Airbus can win tit for tat war

The World Trade Organisation’s ruling that Boeing received billions in illegal subsidies from the US is a solid counter-punch from Airbus in the pair’s painfully long trade dispute, but it is a long way from resolving their battle. In fact, it is unlikely either will ever emerge as the winner.

Instead, they arguably find themselves in a weaker position, while facing an even bigger threat to their dominance from China.

The world’s two biggest plane-makers have been at each other’s throats for dominance of the civil aviation market for decades, but 12 years ago the battle spilled over into a bitter tit-for-tat row over allegations of illegal subsidies.
 
Awamu hii ya Magufuli watu walio zoea kukuza Udaku watakimbia hadi vivuli vyao!!
Mimi ningependa watupatie mrejesho wa Bombedia
walizisema sana
Sasa je nikweli zile tuhuma !?
Kwanini watu wakimbilie Boing kabla ya kujua nini matokeo ya tuhuma zile za Bombedia!!!
Watanzania kwa nini tunayumbishwa na kuchezewa na wanasiasa Uchwara!!

Sasa limekuja suala la muda
eti ndege ni yamwaka 2009!!
Hivi watu wazima kichwani!!
kama ni yamwaka 2009 imefanya kazi wapi!!
leo china wanarusha ndege tena wakijinadi ni mpya
imeanza kutengenezwa 2007 miaka 10 sasa.
Ukiishiwa hoja nibora ukae kimya
 
..mashirika mengi ya ndege yanachukua muda mrefu kuleta faida.

..serikali[kupitia kodi za wananchi] italazimika KULIBEBA kwa muda mrefu shirika letu la ndege.

..tunawaiga Rwanda lakini shirika lao la ndege linaendeshwa kwa hasara na majuzi wamemfukuza ceo wa shirika hilo. hali ni hiyo hiyo kwa shirika la ndege la Kenya.

..ni afadhali mabilioni yaliyotumika kununua ndege yangewekezwa ktk sekta nyingine ya uchumi ambayo ina faida ya uhakika.
 
Kuna uwezekano mkubwa ni hao Airbus wamemlisha Zitto ''matango pori''!

Kuna mapambano makali ya kibiashara katika haya makampuni.

Kwa maelezo hayo
90% ni hao hao
sasa unaanzaje kuwa amini hawa watu!!
Kama umeishiwa sibira ujiunge na yule anaye lilia kuongea msibani!
 
Na kwenye hili suala la hii ndege lazima kuna something fishy..Kelele zimesaidia sana.

Maana sasa hivi ndio serikali wanajipinda mpaka kutoa misuli kujaribu kunyoosha mambo. Pale mwanzoni mlikuwa kimya.

Nafikiri baada ya kurekebisha mambo na Boeing ndio mnapumua sasa..

Ukweli utajulikana tu.
 
Hajasema lolotekuhusu kununua ile range kimeo??? Mbona hapo ameparuka?? Na bei ya punguzo iliyo ndani ya offer kwa zile mbovu?? Hajui hiyo ndege ajili ya international trips?? Abiria hasa wanaojitambua wataogopa kupamnda na romours zikienea wameliwa!!!! Sijui watafanya nini na hasara hiyoo!!!
Nasoma maswali mengi tu umeuliza lakini tatizo hayana mantiki yoyote kwa mtu mwenye common sense achilia mbali mtu mwenye fikra pana.

If you have nothing to say, say nothing-Mark Twain

If you have nothing to write, write nothing.

Hata kitendo cha kusoma tu thread na kuondoka kimantiki utakuwa umetoa mchango wako.
 
..mashirika mengi ya ndege yanachukua muda mrefu kuleta faida.

..serikali[kupitia kodi za wananchi] italazimika KULIBEBA kwa muda mrefu shirika letu la ndege.

..tunawaiga Rwanda lakini shirika lao la ndege linaendeshwa kwa hasara na majuzi wamemfukuza ceo wa shirika hilo. hali ni hiyo hiyo kwa shirika la ndege la Kenya.

..ni afadhali mabilioni yaliyotumika kununua ndege yangewekezwa ktk sekta nyingine ya uchumi ambayo ina faida ya uhakika.
Ndege ni kama miundombinu mingine tu, ukiacha faida inayopatikana moja kwa moja, kuna faida lukuki zinapatikana indirectly kwa nchi kuwa na usafiri wa anga wa uhakika.
 
..mashirika mengi ya ndege yanachukua muda mrefu kuleta faida.

..serikali[kupitia kodi za wananchi] italazimika KULIBEBA kwa muda mrefu shirika letu la ndege.

..tunawaiga Rwanda lakini shirika lao la ndege linaendeshwa kwa hasara na majuzi wamemfukuza ceo wa shirika hilo. hali ni hiyo hiyo kwa shirika la ndege la Kenya.

..ni afadhali mabilioni yaliyotumika kununua ndege yangewekezwa ktk sekta nyingine ya uchumi ambayo ina faida ya uhakika.

Matusi,Kejeli, Porojo
vilizidi mkitoa mfano kwa hao hao Rwanda,
Kanchi kadogo
kanchi kametoka kupigani vita
kanatushinda litanzania lina kila kitu Miaka 50 hatuna hata ndege moja!!
Mtulie awamu hii Mkose hoja na muishie kulilia kuongea msibani
maana Upinzani nchi hii hakuna ni wanafiki na wachumia tumbo tu
 
Back
Top Bottom