Wizara ya mazingira ihamasishe upandaji miti ya asili na matumizi ya gesi kupikia

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Tunaomba wizara ya Mazingira ihamasishe urejeshaji mazingira ya asili
Mazingira ya asili yakirudi ndege wa asili watarudi,wanyama wa asili watarudi mimea,majani na uoto wa asili utarudi.Na hali ya hewa ya asili itarudi.

Mojawapo ya kuhakikisha hivyo vinarudi ni kuhamasisha upandaji miti ya asili kwenye maeneo husika.

Ni aibu kuwa baada ya miaka 55 ya uhuru bado tuna vitalu vya miti ya kikoloni kama mitiulaya,mi-ashoki tree,miarobaini,mikaratusi nk miti ambayo hamna ndege yeyote hata wale wa hovyo kama kunguru,bundi au popo hawawezi weka hata kiota chao cha makazi na kuzaliana.

Miti hiyo ya kikoloni haifai kufanyiwa kampeni ya upandaji miti maeneo mbali mbali.Vyuo vyetu vya kilimo na wataalamu mbali mbali wahangaikie ukuzaji na uoteshaji miti ya asili na vitalu vya miti ya asili.Ni aibu mbele ya nyumba ya mtu hata ofisi ya serikali kuwa na mti wa kikoloni badala ya mti wa asili.

Pia wizara ihamasishe matumizi ya gesi ya kupikia vijijini na mijini.Bei ya gesi ipunguzwe na kodi ziondolewe ili kuwezesha watu wengi zaidi kutumia gesi ya kupikia kunusuru misitu na pia kuwezesha watanzania wengi kufaidi gesi yetu iliyogunduliwa.

Kampeni ya upandaji miti ya asili iendane na kampeni ya utumiaji wa gesi ya kupikia.

HAPA KAZI TU

yehodaya123@gmail.com
 
Back
Top Bottom