Wizara ya Maliasili na Utalii leteni uhalisia ya ongezeko la watalii nchini

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Wana jamvi
Salaam

Moja ya madhara na makosa makubwa yaliowahi kufanywa na wizara hii ni kuongeza kodi ya vat 18% ghafla katika huduma za utalii nchini, Aidha Wizara ilitakiwa ikae na wadau wote wa utalii kuona faida na hasara ya kuongeza Vat huku huduma za utalii zikiwa bado mbovu mfano mahoteli kutokua na ubora halisia wa kinyota, ubovu wa barabara katika vivutio,
Aidha kumekua na malalamiko kutoka kwa wadau hususani kuporomoka kwa idadi ya wageni baada ya tangazo la ongezeko la VAT 18%, juzijuzi tumemsikia Waziri wa Fedha akisema idadi ya wageni imeongezeka sasa kivipi wizara husika jitokezeni na takwimu ili kuondoa mapishi ya taarifa
 
Lofa katika ubora wake.

Anahubiri serikali ilete maendeleo lakini hataki kabisa kulipa kodi. !!

Hiyo serikali itakunya pesa??
 
Mi nadhani Waziri wa fedha angeanza kututangazia makusanyo ya kodi ya TRA mwezi November na December yalikuwaje...

Kuhusu utalii kwa sasa sio msimu wa utalii, msimu ni kuanzia May hadi November. Lakini ukifuatilia hotuba ya waziri aliongelea wageni walioingia nchini kwa ujumla na sio watalii. Wageni walioingia nchini ikiwemo wale jamaa wa Burundi wanaoenda kusalimia Waha wenzao Kigoma, Masai anayevuka Namanga kwenye harusi ya nduguye, Mkurya wa Kenya anayeenda Tarime kutoa posa, Mnyamwanga wa Zambia anayeenda Tunduma kufanya kibarua cha kulima nk
 
Back
Top Bottom