Wizara ya maliasili na utalii, kuweni serious kutangaza vivutio vyetu

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,902
Kwa mtazamo wangu naona kama tokea uhuru hatujawahi kuwa serious kabisa kutangaza vivutio vyetu vya utalii.

Huwezi kuniambia kwamba pamoja na vivutio vyote hivi tulivyonavyo bado pato la taifa halijachangiwa vilivyo na hii sekta kama inavyotakiwa kuwa.

Serengeti, Ngorongoro Manyara, Mikumi, Uduzungwa, Saadani, Gombe, Zanzibar, Kilimanjaro, Olduvai, nakadhalika nakadhalika nakadhalika.

Kuna nchi zinazokaziwa kamoja tu lakini zimeligeuza kua kivutio cha utalii na fedha zinaingia, sisi tunavyo mpaka na vya ziada vingine tunawaachia na kuwaazima majirani zetu wavifanye vyao kabisa sisi tumekaa kimya tu tunalalamika.

Nadhani kuna umuhimu waziri wa wizara husika kwa kushirikiana na wadau wa utalii, waamue kushindana katika soko kukuza utalii, mapato kama gesi na madini yanaweza kua surplus tu kama tukiwekeza ipasavyo kwenye hii sekta.
 
Sekta ya utalii inashindwa kuwa na ufanisi kwa sababu ya ufisadi. Watu wanaangalia ni namna gani wao kwanza watakavyoweza kufaidika na maliasili na vivutio. Kenya iliwahi kuzitumia channel za super sports kwa ajili ya kurushia matangazo ya utalii. Sisi tuliishia kuangalia tu hayo matangazo kama vile hatuhusiki. Ipo haja kwa Rais Magufuli kuwashikia bango hawa jamaa wote wanaohusika na utalii. Maslahi ya makampuni makubwa hayawezi kufanana na maslahi ya wananchi wengi. Madalali wa makampuni ya wazungu hawawezi kumfikiria mlalahoi anayepaswa kufaidi rasilimali tulizojaaliwa kwa kupitia mfumo wa kodi na mapato mengineyo yatokanayo na utalii.
 
Kitengo kinachohusika na kutangaza utalii wetu kivunjwe na kuundwa upya. Hakuna wanachofanya.

Kuna mdau mmoja wa utalii alinisikitisha alipo nieleza jinsi wenzetu wa Kenya wanavyotupiga bao kwenye maonyesho ya utalii sehemu mbalimbali duniani. Katika maonyesho hayo ambayo ni ya kujitangaza, wakenya wanakuwa aggressive sana. Watanzania ambao tumewaamini kutoka TANAPA wanageuka wa watalii. Hawakai kwenye mabanda kutangaza vivutio vyetu licha ya kupewa posho nene, kulala 5star hotels na kusafiri vip class.

Mhe. Magembe ana kazi ya kufanya katika wizara maana kuna uozo kila idara. Mpaka sasa licha ya idara ya misitu kuigusa, amefanya nini? Baadhi ya watumishi katika wizara yake wanadai mhe. ni mtu wa kujirusha. Kaza buti mhe., na wananchi tunataka mrejesho katika kuisafisha wizara yako. Tutakupima ndani ya siku mia moja tangu uwe waziri umefanya nini. Kama rais atapimwa sembuse mawaziri.
 
Kuna haja ya kureview mikataba ya baadhi ya sekta za serikali,watu wamejisahau sana
 
Wala si hivyo ndugu yangu ili kuwepo ari kubwa ya kutangaza vivutio vyetu miaka ya nyuma na inge endelea vile mpaka leo tungekua mbali mno,mbali ya ofisi za balozi zetu nje kulikuwa na ofisi Ujerumani,Italy,Japan na marekani nyingine zime nitoka ofisi hizi zilizo jitegemea zilifanya kazi kubwa sana kuhamasisha utalii Ulaya na Marekani chini ya wizara ya maliasili na Utalii na matokeo yake makampuni makubwa ya utalii Duniani yali leta sana watalii nchini pamoja na kuwa mahitaji muhimu nchini na uchumi kuwa mbaya ndio ilikuwa kikwazo tofauti na sasa, kwa uchache Makampuni hayo toka Italy ni Turisanda,Galasia viagi,Tui nakadhalika, Marekani Covos, Ujerumani Raizen Bose, Arazen nakadhalika, ambayo group moja ilikuja na zaidi ya watu mia mbili bahati mbaya utalii uli anza kubomoka kwa ofisi hizo kufungwa, ubadhilifu na hatimaye kufa kwa shirika la utalii Tanzania (Tanzania Tourist Corporation) na pia hoteli zake zote kubinafsishwa, kuvunjwa kwa shirika la huduma za usafiri kwa watalii(State travel services) kitengo cha safari za baharini na michezo ya baharini(seafaris) kwa nchi yenye neema kama hii hapakuwa na sababu ya makampuni muhimu kama yale kutoweka na hata Wakenya wange tukamatia mbali ila ndio kama inavyo zungumzwa kupanga ni kuchagua.
 
Back
Top Bottom