Wizara ya Kilimo na unyeti wake kwa maslahi ya Taifa

Wizara ya Kilimo na unyeti wake kwa maslahi ya Taifa

karango

Senior Member
Joined
May 19, 2013
Posts
162
Reaction score
25
Jamani sijui huwa kwa nini naamini hivi, ili tujukwamue hapa tulipo sasa, tunahitaji Waziri wa Kilimo mkwelina mchapa kazi.

Tunahitaji mtu ambae atamshauri vizuri JPM bila unafiki wa kisiasa kufufua mazao yote ya biashara na mkulima apate kipato kinachojibu changamoto za maisha kwa mfano kahawa waziri aliyepita alidhubutu kuruhusu shamba la kahawa kuuziwa mwekezaji ili eti alime MAPARACHICHI ni aibu kwa taifa letu, je kwa akili hiyo waziri kama huyo anaweza kusema kahawa imekufa kwa sababu wizara ya biashara haijatafuta masoko? wizara ya viwanda haija fungua viwanda vya pembejeo na kuchakata kahawa?

Wizara ya elimu haijaandaa vijana kwa ajili ya kufanya kazi kwenye viwanda vinavyohusu kahawa na biashara zake? wizara ya fedha haijatoa fungu la kufufua kahawa wakati ushauri wako walime maparachichi? wizara ya vijana na ajira haijaajiri watu kwenye mashaba, viwanda na biashara zinazohusu kahawa.

Huo ni mfano tuu wa jinsi wizara ya kilimo inavyoweza kusisimua wizara karibu zote ndio maana nasema tunahitaji kichwa cha nguvu na nashauri apewe unaibu waziri mkuu ili aweze moja kwa moja kuwaface mawaziri wote wanao mwangusha.

Mfano mwingine ni kusema KILIMO KWANZA alafu unaachia maji yanaenda baharini, siku moja nilikuwa ikwiriri niltamani maji yote yazuiliwe kwenda baharini utete yote na Ikweriri yote ijeuzwe ukanda wa kilimo cha umwagiliaji alafu tuone huyo waziriwa biashara atashindwa kutafuta masoko?

Tushauri mabwawa kila kata tuone waziri wa ujenzi hataandaa barabara ili kuvifikisha vyakula mjini. Tuombe mungu tumpate waziri wa kilimo ambae atakuwa mokozi wetu na tusiahau kilimo peke yake kinaweza kuajiri 80% ya watanzania.
 
Back
Top Bottom