MVB Jr
JF-Expert Member
- Sep 16, 2016
- 489
- 1,554
Wakuu hii ni ramani ya bagamoyo inayoonyesha mgawanyiko wa hali ya udongo na umahsusi wa udongo kwa ajili ya uzalishaji wa kundi fulani la mazao.
Hii ramani ni moja kati ya nyingi zilizoandaliwa na wizara ya kilimo kama rasilimali kwa taifa na kuwa uploaded kwenye website yao kwa minajili ya kutaarifa umma wa watanzania na wakimataifa juu ya hali ya udongo katika maeneo mbalimbali ya nchi na ubora wa udongo kwa ajili ya uzalishaji wa kundi fulani la mazao.
Cha ajabu hizi ramani hazina ubora kabisa, ukizingatia funguo za baadhi ya ramani kusomeka kwa shida sana au kutosomeka kabisa. Picha hizi zipo kichoyo sana, kupelekea niamini walilazimishwa kuziupload na bahati mbaya aliyewalazimisha hakuhakiki utekelezaji wake..!
Binafsi nitoe wito kwa wizara ya kilimo kuzirekebisha hizi ramani, maana hii ni rasilimali nyeti na yenye maslahi mapana kwa taifa na jamii ya kimataifa kwa ujumla. Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ni aibu kama wizara kupandisha taarifa isiyo na ubora kama rasilimali.
Nawasilisha.