Wizara ya kazi na ajira mmefikia wapi utekelezaji wa agizo lenu?

ndugu yako

Senior Member
Mar 30, 2013
193
96
Mnamo tarehe 27/01/2014 Waziri wa kazi na ajira Bibi Gaudentia Kabaka alitoa tamko hili:-

WIZARA YA KAZI NA AJIRA

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUSITISHA UTARATIBU WA KUKODISHA WAFANYAKAZI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA

1. Wizara ya Kazi na Ajira imekua ikipokea malalamiko toka kwa wadau mbalimbali kuhusu utaratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini.

2. Wizara imefanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili na kubaini kuwa utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka
1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002]. Kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hii, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na ushauri elekezi kwa watafuta kazi, kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira. Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine.

3. Aidha, uchunguzi umebaini kwamba utaratibu huu ni ujanja unaotumiwa na baadhi ya Waajiri na Mawakala kwa lengo la kukwepa kodi na kujipatia faida kwa kukwepa kutoa haki za msingi za wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria za Kazi. Baadhi ya makampuni yanayokodisha wafanyakazi yamefanyiwa uhakiki na TRA na kubainika kukwepa kodi ya mapato ya ajira (PAYE) na na kodi ya mapato ya kampuni kinyume na Kifungu cha 7 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 [Sura 332 kama ilivyorejewa Mwaka 2008].

4.Uchunguzi huu umebaini athari mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoajiriwa kwa utaratibu huu. Athari hizo ni pamoja na:

Wafanyakazi kukosa haki ya hifadhi ya jamii kama vile likizo ya uzazi na matibabu kinyume na Sheria mbalimbali za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;

Uwepo wa ubaguzi katika malipo ya mishahara kwa kazi ya aina moja kinyume na kifungu cha 7(10) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6 ya mwaka 2004 ambacho kinamtaka mwajiri kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi bila kujali jinsia zao wanalipwa mishahara linganifu na ya haki kwa kazi yenye uzito na thamani sawa;

Kukosa fursa za kujiendeleza kielimu na mafunzo;

Kukosekana kwa usalama na uhakika wa ajira ;

Wafanyakazi kulipwa mishahara ya kima cha chini kinyume na sekta wanayofanyia kazi.

5. Kwa taarifa hii, Wizara ya Kazi na Ajira imeamua kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakala kuwaajiri wafanyakazi wanaowatafutia kazi. Aidha, Mawakala na Kampuni husika waliopo katika utaratibu huu kwa sasa wanapaswa kuwahamisha wafanyakazi waliokodishwa kutoka kwa Wakala kwenda kwa Kampuni husika. Waajiri na Wakala wanatakiwa kukamilisha zoezi hili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira kabla au ifikapo tarehe 28/02/2014.

6. Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kama kuna wafanyakazi wa Kigeni wanaohusishwa katika utaratibu wa kukodishwa ili hatua zinazotahili ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwataka waombe vibali vya ajira kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Na.7 ya mwaka 1995 na Sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999. Wageni watakao kidhi vigezo wataajiriwa na kampuni walipokodishwa; ambazo kwa wakati huo zitakua ndiyo mwajiri wao.

7. Wizara ya Kazi na Ajira inawaelekeza Wakala wa Huduma za Ajira nchini kwamba, kwa utaratibu wa sasa watapaswa kuwasilisha barua za maombi ya usajili wa Uwakala kwa KAMISHNA WA KAZI kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002] ili waweze kufanya shughuli za Uwakala wa Huduma za Ajira kisheria. Maombi haya yawasilishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa tangazo hili. Baada ya muda huo Wakala asiye na kibali cha Kamishna wa Kazi hatoruhusiwa kuendesha shuguli za huduma za ajira nchini. Aidha, Mawakala watakaopata leseni ya Kamishna wa Kazi yatakua yakitangazwa ili yatambuliwe na Umma.

8. Nasisitiza, maelekezo haya yatatolewa kwa Makampuni na Wakala waliohusishwa katika uchunguzi kwa ajili ya utekelezaji.

IMETOLEWA NA

GAUDENTIA MUGOSI KABAKA (MB)

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA
27/01/2014


Baada ya tamko hili wengi ambao ni wahanga wa haya makampuni tulifurahia tukijua kuwa ukombozi wetu umefika.
Baada ya muda wizara ilitoa orodha ya haya makampuni yaliyoomba usajili.
Baada ya hiyo orodha wizara imekuwa kimyaaaa.

Tukirudi upande wetu waajiriwa wa haya makampuni hasa hasa sisi wa ISON (Zaman iliitwa SPANCO), Infinity na NFT hatujaona faida yoyote zaidi ya kuongezeka kwa vitisho vya kupoteza kazi (wengne wameishapoteza, mwezi uliopita NFT imefukuza/imepunguza wafanyakazi 40)

Tangazo hili la wizara badala ya kutoa mwanga limeongeza giza na giza hili limekuwa likichochewa zaidi na waajiri, mfano kwa sasa inasemekana kuwa HRs wa tigo wamekuwa wakiwatumia baadhi ya viongozi wa call centres na branches kueneza habari kuwa hili tangazo ni la uongo na wala wao kama kampuni hawana na wala hawatakuwa na mpango wa kutuajiri moja kwa moja.

Lakini pia haya makampuni ya uwakala yamekuwa yakitumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kupuuzia hili tangazo mfano yamekuwa yakitoa mikataba ya muda mfupi kama vile mwezi mmoja hadi miez mitatu huku wafanyakazi wengne wakiwa hawana mikataba kabisaa.

Haki zetu za kuhakikishiwa usalama kazini wameendelea kuzipuuza mfano wafanyakazi wa ISON na Infinity hawana bima za afya n.k.

Wizara ya kazi na ajira tunaomba mtusaidie kidogo kuharakisha huu mchakato ili watu tuwe na amani na utulivu maana tumechoka na vitisho vya kufukuzwa kazi kila kukicha huku kampuni ya tigo (mwajiri mkuu) akichochea vitisho hivi!
 
Hiyo kauli ilikuwa siasa tu maana kelele/malalamiko yazilizidi mnoo.
Hizo kampuni za uwakala znamilikiwa na wao wenyewe.
 
Usiwaamini sana wanasiasa na viongozi wa dini ktk maisha yako..

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Sasa kama nisipo waamini wabasiasa na viongoz wa dini mnataka niwaamini akina nan?!
 
Serikali inabidi isimamie haya makampuni yanayohusika na uwakala wa ajira. Yamekuwa ni makampuni yanayoendesha unyonyaji kwa kiasi kikubwa sana. Mengi ya Makampuni hayo ambayo yanamilikiwa na wageni yamefikia hata hatua ya kukataa kuwapa haki za msingi wafanyakazi. Mfano wa Kampuni ya NFT ambayo imekuwa na unyonyanji mkubwa sana kwa wafanyakazi walioajiliwa chini ya kampuni hii.

Wafanyakazi wake wamekuwa hawalipwi LIKIZO ZA UZAZI na pia hata Mara wajifunguapo wamekuwa hawapewi yale masaa ya kuwahi kwenda kunyonyesha watoto hivyo hufanya kazi kwanzia saa moja mpaka saa kumi na moja jioni.

Kama sikosei Rais alitoa tamko Fulani kuhusiana na suala la makampuni haya ya uwakala wa ajira kuwanyonya wafanyakazi na kutaka yaangaliwe upya.

Hamna ambacho kimefanyika.sana sana wafanyakazi ambao wanakuwa chini ya mawakala hawa huwa wana fikiriwa miaka yote kama ni Vibarua haijalishi wamekaa miaka mingapi katika kampuni husika. Mimi binafsi nina ushahidi Mkubwa kuhusiana na Kampuni inayoitwa NFT.

Nina ndugu ambaye ameajiriwa Tigo kupitia wakala huyu wa NFT tunaiomba serikali ipate muda wa kuongea na wafanyakazi ambao wameajiriwa kupitia Wakala huyu.

Wafanyakazi hawa wanakosa Malipo ya Likizo ya uzazi, wanakosa muda wa kuwahi nyumbani kunyonyesha mtoto/ watoto pamoja na wao kufanyishwa kazi masaa mengi zaidi ya walioajiriwa na Kampuni husika moja kwa moja.

Ushahidi wa mambo haya upo na sasa imefikia hatua sisi Watanzania tunanyanyasika sana na Serikali yetu haijui au haitaki kulichukulia hatua jambo hili.

TUNAOMBA PAMOJA NAKUWA NA SHIDA YA AJIRA SERIKALI ILIANGALIE JAMBO HILI KWA KINA. NA MAKAMPUNI AMBAYO YANAAJIRI WAFANYAKAZI KUPITIA KAMPUNI HIZI wasiwanyanyase wafanyakazi wao.

Zaidi zaidi mambo haya wadau tusaidiane kuyapeleka katika vyombo vya sheria.
 
Kuna hawa spanco sasa wanajiita Ison wana walipa Call center agent 230000 na kazi ilivyo ngumu afadhari tusiwe na viongozi kuliko kuwa na viongozi wasio tujari.
 
Hiyo kauli ilikuwa siasa tu maana kelele/malalamiko yazilizidi mnoo.
Hizo kampuni za uwakala znamilikiwa na wao wenyewe.

Me ninafanya kazi kwenye call centre agent. Napokea simu 150 kati ya hizo 150 naongea na watu 50 tu hao 100 nawakatia simu ili twende sawa na mwenye wateja kwa sababu anajua tunavyonyanyasika na yupo kimya.
 
Leo asubuhi nilimsikia mh. Waziri Kabaka akilitolea ufafanuzi hili suala kupita Cloud fm radio katika kipindi cha Power Breakfast, Nadhani waziri atakuwa hajui kuwa haya matamko tumechoka kuyasikia na sasa tunahitaji action ya serikali tu.
 
Hivi hili swala limefikia wapi?
Au serikali hiii imekaa kimya tui hadi pale makubwa yakitokea ndio itazima moto?
Kama serikali ilitoa tamko, inakuaje hawakulitekeleza?
 
Back
Top Bottom