Wizara ya Fedha na Mipango yawaasa Watanzania kuchangamkia ununuzi wa hisa za awali za Vodacom.

kamati ya ufundi

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
416
439
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

TAARIFA KWA UMMA
WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA UNUNUZI HISA ZA AWALI ZA VODACOM

Serikali imewataka watanzania kuchangamkia fursa ya ununuzi wa asilimia 25 ya hisa za awali za kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom zinazouzwa kwa watanzania pekee ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2016 kwa lengo la kuwawezesha watanzania kuwa wamiliki makampuni ya simu za mikononi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi Beng’i Issa amesema hi ni fursa kubwa na muhimu kwa watanzania kuwa sehemu ya wamiliki wa makampuni ya simu za mikononi kupitia ununuzi wa hisa hizi za awali.

‘’Ni uwekezaji ambao ni salama sana na hauna hasara, kwa kuwa ukiwa hutaki kuendelea kuwa mwanahisa unauza hisa zako na kurudisha pesa zako na unaweza kupata faida’’.

Ununuzi wa hisa hizi utawawezesha Watanzania kuwa wamiliki wa kampuni, watapata gawio la faida, wanaweza kutumia hisa kama dhamana za mikopo benki na wanaweza kuziuza hisa wanapokuwa na shida ya fedha.
Hisa hizi zinauzwa kwa mtanzania mmoja mmoja, watumishi walioajiriwa, wastaafu, makampuni yanayomilikiwa na watanzania, mashirika ya kitanzania, VICOBA, SACCOS, vikundi vya kijamii, wanawake na vijana. Aidha hisa moja inauzwa kwa shilling 850 na kiwango cha chini cha ununuzi ni hisa 100 na hakuna kikomo cha juu cha ununuzi wa hisa.

Baraza linatoa rai kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii Nchini, Taasisi za fedha, Vikundi vya fedha vya kijamii kuwezesha wanachama na wateja wao kununua hisa hizi za awali.

Ununuzi wa Hisa hizi unapatikana kupitia matawi ya benki ya NBC, NMB, CRDB nchi nzima, mawakala wa soko la Hisa la Dar es Salaam, M-PESA na matawi mbali mbali ya benki za biashara nchini.

Baraza linawahamasisha watanzania wote kuchangamkia fursa hii muhimu ili kushiriki kikamilifu katika kumiliki uchumi wao na kufikia ndoto ya kuwa Taifa la uchumi wa kati kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Mwaka 2025.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linashirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari kama radio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii kuhamasisha watanzania kunua hisa hizi za awali.

Imetolewa na;
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango
 
Naamini hii ni fursa iliyotudondokea watanzania nawashauri tusivunge Bali tujikite katika uwekezaji huu.
Hakika Vodacom inalipa unapofanya uwekezaji wowote..... Nunua hisa sasa [HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG] kwa maisha ya baadae
 
Mimi naamini katika uwekezaji kuna mafanikio makubwa nawashauri watanzania wenzagu kuwekeza na mtandao wa Vodacom kwa kununua hisa zao ili kuwa watanzania wa kwanza kunufahika na mtandao huu.
 
Mimi naamini katika uwekezaji kuna mafanikio makubwa nawashauri watanzania wenzagu kuwekeza na mtandao wa Vodacom kwa kununua hisa zao ili kuwa watanzania wa kwanza kunufahika na mtandao huu.

Mtu mwenye akili timamu na anajua biashara hawezi kununua hisa za vodacom.
 
Tangazo lao linadai "ununuzi wa hisa una changamoto nyingi. ............"

Kauli hii nadhani ndio mlango wa kupishania baada ya kula hasara "utawekewa hiyo cd"

Serikali si inunue zote hizo kwa niaba ya wananchi?
 
1. Ipo wapi NICOL??
2. Serikali haitoi nuru ngavu kwa wawekezaji.
3. Poleni TPSF!
 
1. Ipo wapi NICOL??
2. Serikali haitoi nuru ngavu kwa wawekezaji.
3. Poleni TPSF!
 
kwenye mpesa mnavyotufanyia hela ikitumwa inachelewa kufika matokeo yake tunashughulikia ndio maana hata hizo hisa tunaogopa kununua
 
Serikali si inunue zote hizo kwa niaba ya wananchi?[/QUOTE]

Dalili zinaonyesha kuwa uwezekano huu unaweza kuwepo iwapo tarehe 11.05 kiwango cha mauzo hakitafikia!!!
 
Back
Top Bottom