Wizara ya elimu vipi juu ya mtaala mpya wa kkk kwa madarasa ya awali 1 na 2

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,447
Wizara na serikali ilifanya mabadiliko ya sera, ikafuatiwa na mabadiliko ya mtaala wa darasa la kwanza na la pili wa mwaka 2015 ambao unazingatia lugha rahisi kujifunza na umahiri wa mtoto kiujuzi na si kitaaluma ambapo ulifuta masomo ya taaluma na kuanzisha masomo ya umahiri au ujuzi.
Hii ilitikana na dhana ya enhri ,1994 amabye anataja vigezo vya mtoto kujifunza kutokana na vipengele rahisi hususani kwenye kusoma.

Serikali hii ma wizara.ya.elimu mwaka 2013 walitoa tender Kwa kampuni ya marekani kufanya utafiti wa darasa la pili nchi nzima sijui walitumia mabilion mangapi sijui, walitafiti halmashaur 20 za Tanzania katika maeneo yaliyotokana na ufahulu wa darasa.la saba 2012 kwa shule zilizofanya vizuri na zisizofanya vizuri.
Utafiti ambao ulipima KUSOMA KISWAHILI, KUSOMA ENGLISH, KUHESABU NA UTAWALA NA USIMAMIZI KATK SHULE ZA MSINGI . Na kutoa majibu ambayo yaliakisi uhalisia kwa namna yake ambao pia taarifa yake iko ktk lugha ya kiingereza ambayo tafiti yenyewe haipatikani kirahisi na workshop ya wizara ya mwaka 2014 ya kujadili itafiti huo bado haukumuhusisha mdau mwalimu wa la kwanza la pili japo ulifanywa Kwa la pili tu,

Wakati mtaala unaanzishwa tayari serikali kupitia mdau wake wa maendeleo USAID walikuwa wanaendelea na program ya TZ21 kwa mikoa ya mtwara na zanzibar ambapo program hii iliifumbua vizur serikali juu ya madarasa ya awali na kushauriwa kufanya utafiti ambao umezaa matunda ya mtaala mpya wa darasa la kwanza na lapili.
Pia program hii ya tz21 ilitoa mafunzo kwa walimu wa wasimamizi wa walimu na elimu kasoro wadau ambapo ulianzisha namna mpya ya ufundushaji hususani somo la kiswahili drs la kwanza na la pili kabla ya mabadiriko tangu 2013 april hadi 2015 ambapo program hii ilifungwa.

Wakati.wizara na serikali zinatoa mtaala mpya wa drs la kwanza na la pili Feb 2015 ilienda sambamba na kutoa mafunzo kwa walimu kwa kuanza na mtwara walimu wote wa la kwanza na lapili, baada hapo wakaelekea dodoma kwa walimu takribani 1800 ambapo wazir kawambwa alilamika baadhi ya walimu kuvamia na idadi kuzidi pia walimu wakuu kwenda badala ya walimu mahususi Kwa mafunzo ya muda wa siku 10, sitasema juu ya maposho.

Baada ya mafunzo wawezeshaji walitoa ahadi ya kuwa VITABU VYA MTAALA HUO VINAENDELEA KUANDALIWA NA KUCHAPWA, NA KUANZA KUSAMBAZWA MAY 2015 licha ya ahadi hiyo nzuri walimu hao hawakuchukuliwa maoni yao juu ya vitabu, ambapo mkikumbuka vema wakuu vitabu vilivyotumika wakati mnasoma viliandaliwa na tet Kwa msaada wa wadau wasimamizi.na walimu wa madarasa hayo, kitabu cha mwisho cha tet cha kusoma na kuandika kilimshirikisha mwalimu kutoka naliendele mtwara, picha itafuata

Kufikia mwezi July vitabu vilisambazwa kwa kuanza na halmashaur ya mtwara mikindani ambapo masomo ni 5 na vitabu vilivyotolewa havikuzidi 10, licha ya vitabu kutolewa mpaka mwezi august vitabu hivyo vilikuwa havitumiki kutokana na uzembe wa mwalimu mkuu kutiwasiliana na walimu pia walimu kushindwa kuendana na mabadiliko ya mtaala na kuishia kusema" sijui nilishindwa ya tz 21 nitaweza haya"
Na hakuna msaada kwao kwani walimu wakuu na wataaluma washule hawakuhzdhuria mafunzo hayo hivyo wakishindwa wao na wote shuleni waneshindwa.

Licha ya hayo pia hakuna afisa elimu aliyepewa mafunzo hayo ya mtaala mpya zaidi ya walimu wa la kwanza na la pili, hivyo halmshaur zote usitegemee kukuta mtaalamu wa kkk au mratibu wa kkk au mtaalamu wa mtaaala mpya.

Ni wazi serikali ili kurupuka kwa maana mpaka sasa sio halmashauri zote za mtwara au kwingine zina vitabu hivyo.

Na kuna tetesi vitabu hivyo si bora na watu huko tet wamepoteza vibarua kutokana na hilo,
Mpaka sasa najiuliza maswali yafuatayo kama mdau wa elimu
1. Ni maudhui gani yatapimwa mwaka huu kwenye mtihani wa taifa wa darasa la pili ambao mpaka sasa waziri amedai q atatoa zawadi kwa walimu ambao madarasa yao yatafanya vizuri ikiwa wanatumia mtaala na mihtasari na miingozo ya masomo pekee bila ya vitabu?
2. Ni hupi mfumo wa mtihani huo wa darasa la pili ikiwa hata uwezo wa zoezi mwalimu haujui pamoja na namba za maswali, aina za maswali, na namna ya ufanyaji na ujazaji majibu? Je karatasi gani zitatumika Kwa wanafunzi hawa wa miaka nane na saba hadi tisa? Je karatasi zitaendana na daftari zao za vyumba, mistari mikubwa na midogo? Je mtihani wa kusoma utafanyajwe? Kama ni kila mwanafunzi je mtihani wa wanafunzi 50 kwa wasimamizi wawili watatumia muda gani?
3. Bado najiuliza japo hapo juu nimeuliza maswali mengi bado nataka kujua muda wa mtihani mmoja?
4., aina ya usimamizi na usahishaji wa mitahani hii?
5. Ni lini serikali itatoa mwongozo wa mtaala huu mpya kwa walimu na wanafunzi hawa yatima wa mtaala mpya?
6. Mh. Wazir bado nataka ajue kama wametumia muda wa mwaka 1 na nusu mpaka sasa je vitabu mlivyosema kwenye sera ya 2014 Kwa ngazi za elimu kuwa ktk lugha ya kiswahili mtatumia miaka mingapi?
7. Bado pia najiuliza Kwa nini walianza na mtaala wa darasa la kwanza na la pili bila mabadiliko ya mtaala wa darasa la awali ambao tayari umefutwa na sera mpya ya.elimu ya mwaka 2014 ambayo inasema awali ni mwaka mmoja na mtaala wa awali wa 2005 unasema awali ni miaka miwili? Pia umri wa watoto umetofautiana pia masomo yamebadilika walimu wa awali watafundishaje ikiwa mwaka huu wametoa wanafunzi kwenda la kwanza na mwakan kutoa wengine?
Nilimuuliza mwezeshaji mmoja wa kkk kutoka tet "akasema walisahau ataenda kushauri,,,"

Nachojaribu kutambua ni kuwa serikali ilikurupuka pia bado wizara na taasisi zake hazijielewi, bila kusahau waziri hazijui changomoto zake na ndio maana katika hotuba yake ya bajeti ansema vitabu hivyo vinaendelea kusambazwa na kuacha kusema kweli pia kutoainisha mipango mizuri katika bajeti yake kulingana na mapendekezo ya sera na kukimbia kwenye elimu za juu ambazo tayari zinamapungufu makubwa zitakazotumia muda mrefu kurekebishwa.
Ni vema angetambua kuanzisha msingi ni bora kuliko kupaka rangi bati lililotoboka ili lisivuje( shule 33).

Pia ni vema serikali na wizara ikatambua 1 kuanzisha mafunzo ya wataaluma na wakuu wa shule mapema iwezekanvyo ili wawe msaada kwa walimu wa madarasa haya chini
2. Kuanzisha mtaala wa awali mapema
3. Kuendelea na mchakato wa mtaala wa elimu msingi Kwan imebaki miezi saba wanafunzi.wa darasa la pili wawe la tatu wasikose tena vitabu kama miaka hii miwili inayoishia.
4. Wakae na walimu pamoja na azaki watatue kero hizi za mabadiliko ya mitaala
5. Waanzishe waratibu wa kkk kuanzia wizaran, vyuoni, mikoani, hamashaur na kwenye klasta TRC ili wawe wasaidizi wa walimu kwa umahiri
6. Waanzishe utawala wa elimu ya awali, yaani elimu awali iwe na organization yake kama mkuu, mshauri na walimu ndani ya shule
7. Waanzishe kozi za kkk kuanzia cheti, shahada na stashahad a then uzamili na uzamivu wa kkk tanzani
8.kulekebisha miundombinu ya madarasa.Na vifaa vya.madarasa haya ambayo kimsingi ni ya mahitaji maalumu ikiwemo choo, madawati mbao za kuandikia, vifaa vya mivhezo na vya kufundishia.

MWISHO NAISHIA KWA KUSEMA
PROF. NDALICHAKO WAACHIE WANASIASA SIASA YAO TUPAMBANE KUJENGA KILE ULICHOKIITA FADHILA ZA WALIMU WAKO.

Mwalimu wa la pili
 
Hongera kwa bandiko lako kiongozi nikikumbuka kipindi cha nyuma nasoma kutoka la kwanza kwenda la pili ilikua utat kama kichwani bado hazichagi na pia kuingia la 3 ilikua mtihani pia ila miaka ya karibuni mtoto hajui vizuri kusoma anavushwa kwenda la pili-tatu eti ataelewa kadri anavyopanda madarasa na inatokana na kubadili mitaala ya elimu bila kuzingatia ubora.
Sitasahau kipindi hicho nipo darasa la upili mwalimu anatutoa nje tuliokuwa hatujui kusoma na kuandika vizuri tupite tunazunguka madarasa yote tukikimbia na kuimba sisi mabogazi...sisi mabogazi.....ilikuwa inaleta changamoto japo ilikuwa inauma lazima ufanye bidii asee
 
Umesema vema kuna shule nyingi sana manispaa ya mtwara mikindani hasa zilizo pembezoni mwa mji watoto wa std 1&2 ni mbukwa kbsa , walimu wakuu wanashindwa kuongoza hizo shule kwa kuwa wanajuana na baadhi ya maofisa ktk ngazi ya elimu wilaya na mkoa, kuna walimu wakuu hata sifa ya uongozi hawana kila siku ni vituko WEZI,kuwaimbisha watoto,na michezo ya ajabu ajabu, walimu wakuu si wabunifu, ila hii inatokana na 10% .hivyo hata huo mradi wa kkk wa 21st unashindwa kusimamiwa vema.
 
Tatizo pia ni kwamba walimu hawana dawati la kuzungumzia ambalo lingetatua kero hizi za kitaalamu katika elimu maana yake ile bodi iliyoahidiwa ikiundwa haya mambo tusingefikisha hapa yangeisha huko huko lakin serikali na wizara zimekuwa ziksuasua
Naomba wazir kama mtaalamu athibitishe utaalamu Kwa kuunda bodi hii isiwe siasa
 
Back
Top Bottom