orangutan
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 757
- 773
Hello Wakuu,
Natumai mko poa. Kuna kasumba moja imezoeleka miongoni mwa walimu wengi wa ngazi zote (Shule ya msingi hadi sekondari), tabia ya kuchukia kufanya kazi vijijini na badala yake kung'ang'ania kufanya kazi mjini. Walimu wengi sana huwa wanapangiwa vituo vya kazi maeneo mengi ya vijijini ambayo ndio yana upungufu mkubwa sana ya wanataaluma hao.
Badala yake hawa walimu huamua kwenda kuripoti tu na baada ya hapo wanaanza kupambana kufa na kupona wahamishiwe vituo vya mjini kwa namna yoyote hata ikibidi kutoa rushwa ya namna yoyote.
Mwalimu wa kiswahili anakuwa yuko radhi ahamishiwe shule ambayo tayari ina walimu wa somo hilohilo zaidi ya saba. Mwisho wake wanaanza kugawana topics sasa, wewe utafundisha riwaya mimi ntafundisha tamthilia. Yuko radhi kuikimbia ile shule aliyopangiwa ambayo haina hata mwalimu mmoja wa somo husika.
Matokeo yake ni kwamba shule nyingi za mijini zina mrundikano mkubwa wa walimu ambao wengine hawana hata vipindi kazi yao ni kupiga umbea tu na kuota jua nje ya ofisi za staff, na kuvizia wanafunzi wa kike (sexual predation). Umewahi kuona sehemu walimu ni wengi hadi ofisi ya staffs haitoshi ilhali kuna shule huko vijijini ina walimu wawili au watatu tu? Basi hali ndivyo ilivyo kwenye shule nyingi hapa nchini.
Naiomba serikali ya mheshimiwa JPM na wizara husika iliangalie hili kwa jicho la tatu (kama ilivyowashughulikia wenye vyeti feki) na walimu wote waliosongamana mijini wahamishiwe sehemu zenye uhitaji huko vijijini haraka iwezekanavyo. Ambae hajisikii kufanya kazi shule za bush aache kazi akakae nyumbani.
Hili likifuatiliwa kwa umakini naamini tatizo la upungufu wa walimu viijini litakuwa limepunguzwa kwa kiasi kikubwa na viwango vya ubora wa elimu vitaongezeka huku vijijini kwetu.
Nawasilisha.