Wizara ya Elimu(Pokea ushauri huu)

Wizara ya Elimu(Pokea ushauri huu)

okakaT

Member
Joined
Oct 30, 2017
Posts
33
Reaction score
9
Nawashukuru sana wizara ya Elimu Tanzania kwa jitihada zote wanazochukua ili kufanikisha elimu bora inapatikana kwa watanzania kwa garama nafuu(Elimu bila malipo kwa elimu ya awali mpaka secondary),kuwahisha mikopo kwa wanye vigezo vya kupata mikopo hiyo(Taassisi ya mikopo elimu ya juu) na kadhalika na kadhalika.

USHAURI
Tumekuwa tukipata matokeo tote katika level zote za elimu kwa njia ya either kuingia kwene mtandao wa internet Kupitia tovuti ya NECTA,NACTE na kadhalika.Asanteni sana kwa ili,Ila sio Sehemu zote za nchi zinafikika kirahisi kwa njia zote hizo ambayo ni changamoto Moja wapo ndani ya wizara.Niwasihi sasa kuwasiliana/kushirikiana na mitandao/mashirika ya simu kama vile vodacom,airtel,tigo na kadhalika ili waweze kuwaunganisha wanafunzi kwa level zote kupata matokeo ya kwa njia ya SMS kwa kutumia index number zao ambazo zinaweza kwa watu wa mitandao Wanaweza kutengeneza namba maalum kama SMS engine kwa kuunganishwa na hizi index namba kwa kupakua matokeo kwa njia ya SMS.

PILI:kuhusu utangazwaji wa matokeo.
Wizara inao watu kupitia Elimu zote kwa maana ya wanafunzi wanaofanya Mitihani Darasa la saba,CSEE,ACSEE nakadhalika,ni wakati sasa wa wao kama either makatibu,wakurugenzi na nafasi husika kusimama mbele ya viombo vya habari Radio na Television ili kusema / kuzungumzia mtizamo wa kupanda kushuka kwa matokeo kwa muhadhara ambao una watu sio wote Ila wanaokubalika kwa idadi kutoka pande mbali mbali za wizara na nchi kwa ujumla wake.
Wananchi watizame na waruhusiwe kuhoji/kuuliza maswali kwa njia mbalimbali kwa maendeleo ya Elimu yetu.
Nawashukuru sana kwa jitahada zote mnazozifanya na nawatakia baraka na afya njema katika kutekeleza sasa na baadaye kwa maendeleo endelevu ya Elimu kwa Watanzania.
 
Nitalifanyia kazi.... umesema unaitwa nani?
 
Back
Top Bottom