WIZARA YA ELIMU: Mabadiliko kwenye elimu yetu Tanzania

Tella Mande

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
494
674
Nimekuwa nikisikia matamko ya wenye mamlaka kwenye sera, miongozo na watoa fedha kwenye sekta ya elimu nashangaa.

Bado utasikia wapo wanafunzi wa msingi na sekondari wasiojua kusoma na kuandika.

Wanaotoa fedha unasikia wakijisifu kujenga madarasa. Hongereni.

Mimi huwa najiuliza, hivi mfuma rasmi wa elimu yetu mbona kama unaanzia hewani na sio mwanzo?

Ingekuwa kwenye sheria, sera na miundombinu kwa elimu ya chekechea iwe rasmi na kila shule iwe na madarasa ya awali tofauti na sasa shule za msingi zinaanzia darasa la kwanza badala ya darasa la awali.

Iwe mjini au vijijini unaposema shule ya msingi ianze na madarasa ya awali ambapo mtoto atafundishwa kusoma, kuandika, kuhesabu na lugha ya kiswahili. Zipo shule sehemu kubwa ya wanafunzi wanachojua ni kilugha chao. Kiswahili kinakuwa kwazo kwenye elimu, sembuse kiingereza.

Baadhi ya masomo ya darasa la 1 na la 2 yanapaswa kuwa darasa la awali. Hii itatoa hata nafasi kwa wanafunzi kusoma masomo yatakayowasaidia baadae.

Na wewe ongeza la kwako
 
Back
Top Bottom