b191
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 742
- 1,031
Habari wanajamvi.
Hivi karibuni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipiga marufuku kwa Shule binafsi kuchuja (Screening). Binafsi siungi mkono tamko hili. Labda nitoe sababu chache;
1. Mchujo katika shule za Setikali, hata Serikali imekuwa ikifanya mchujo katika Shule zake (Screening). Mfano, mtihani wa Kidato cha pili huwaondoa wale wote walio chini ya Alama 30. Hapa ni kwa shule zote binafsi na zile za Serikali.
2. Makundi, Serikali imekuwa ikiwagawanya wanafunzi kulingana na viwango vyao vya ufaulu. Baadhi ya shule ni maalumu kwa wale wenye DARAJA LA KWANZA na baadhi ni maalumu kwa wale wenye DARAJA LA PILI pia DARAJA LA TATU wana-shule zao. Mfano, huwezi kukuta mwanafunzi mwenye DARAJA LA TATU akienda kusoma SHULE kama MZUMBE ai ILBORU.
3. Mkataba, FOMU za kujiunga na shule ni mkataba kati ya MZAZI, MWANAFUNZI na SHULE. Mzazi akienda Shule kabla ya kufanya jambo lolote hupewa FOMU ambayo ina maelekezo ya Shule ikiwa ni pamoja na ALAMA ZA UFAULU. Mzazi anao wajibu wa kukubali au kukataa masharti ya shule. Hapa Mzazi anaweza kukataa kwa kutompeleka mwanae katika shule husika. Hata katika shule za Serikali kuna masharti ambayo mzazi au mwanafunzi akikiuka huondolewa shuleni.
Binafsi siwaungi mkono wazazi wanaolalamika kuhusiana na watoto wao kufanyiwa mchujo kwani wao wenyewe kwa hiari yao walikubaliana na masharti ya shule husika. Serikali pia iziache hizi shule binafsi ziendelee kuendesha Elimu kwa ufanisi mkubwa bila kukiuka sheria za nchi kwa sababu yanayofanyika kwenye shule binafsi hufanyika pia kwa shule za Serikali.
Nawasilisha.