Wizara ya Elimu itachezea Elimu yetu mpaka lini?

okonkwo jr

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
2,419
1,737
Habari wapendwa katika bwana,

naomba niende kwenye hoja yangu bila kupoteza muda
Nimekuwa mdau wa Elimu kwa kipindi kipatacho miaka kumi sasà, lakini chakushangaza Sera yetu ya elimu inampa mamlaka afisa yeyote wa ngazi ya juu kufanya lolote analoona linafaa juu ya elimu na mfumo mzima wa elimu yetu

Kwa Leo nitajikita kuchambua swala LA wanafunzi wa kidato cha kwanza kurudia mtihani mwezi wa pili tarehe 28, jambo ambalo limeniacha na maswali yafuatayo;

Je gharama za kuratibu zoezi zima zinatoka wapi au ndo baraza la mitihani linatafuta mahali pa kulia pesa kwakuwa serikali imekuwa na sera ya kubana matumizi na wao wameona wabuni njia ya kupiga pesa
Kwa kuanzisha Zoezi fek?


Je gharama zilizo tumiwa na wazazi kuwaandaa watoto wao kwa mwaka wa masomo nani atazirudisha ikuwa motto atafeli huo mtihani?

Je huenda ni mbinu iliyoundwa na wateule wa kaka yangu mh.J.P.Magufuli kutaka kumfitinisha na wananchi wake ili ionekane kuwa no maagizo toka juu?

Je wakati baraza linatutangazia matokeo hawakujua kuwa matokeo hayo hayakuwa na ubora na Leo hii miezi minne imepita wanakuja na Sera kuwa hawana imani na matokeo ya mtihani walioutunga na kusimamia hatua zote wao

He serikali imeandaa wanasaikolojia wakutosha ili kuwanisihi watoto watakao feli huo mtihani na kuruxishwa nyumbani, he wazazi nao nani atawanasihi kwa mshituko watakao upata?

Mwisho naomba nitoe rai yangu kwa baraza LA mitihani kuwa waache kuchezea mfumo wa elinu yetu, lakini pia naomba kuwe na Sera ya elimu imbayo itatuongoza na sio kuongozwa na fikira za watu wachache, si hivyo tu pengine pia baraza LA mitihani lisitumike kisiasa katika kuvuruga elimu yetu, tofauti na hilo lakini pia naomba baraza lijitathimini juu ya matokeo ya kidato cha pili ambapo kwa mwaka huu tumeona Mtoto anaingia kidato cha tatu kwa ufaulu wa D mbili

Msimamo wangu juu ya jambo hili la kuwafanyisha mtihani mwingine watoto wetu na pinga sana wawaache waendelee na watawachuja kwenye mtihani wa kidato cha pili mwaka kesho

Pia gharama za kuratibu zoezi hili naomba zipangiwe kazi nyingine na baraza la mitihani liache Mara moja kuchezea kodi zetu wananchi
 
huu mtihani Unaatungwa kama mtihani wa taifa Au kila shule ina andaa mtihani wake? Agizo la serikali la kuto kurudia darasa ikoje maana mlisema mtu asirudie darasa mbona nyie mwafukuza nyumban? ELIMU ILIKUWA ZAMANI Tuuuuu
 
huu mtihani Unaatungwa kama mtihani wa taifa Au kila shule ina andaa mtihani wake? Agizo la serikali la kuto kurudia darasa ikoje maana mlisema mtu asirudie darasa mbona nyie mwafukuza nyumban? ELIMU ILIKUWA ZAMANI Tuuuuu
Kulingana na tamko lao wanasema watatunga wao
 
Back
Top Bottom